Haji Manara atangaza muda sio mrefu atafanya Press ya kuachana kabisa na mchezo wa mpira

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Akiwa kwenye tamasha la Wasafi jana pale Arusha, Haji Manara ameahidi siku si nyingi ataita Press kwa ajili ya kuwaaga watu wa mpira.

Amekaririwa akiongea laivu kuwa mpira umemtengezea sana uadui, hajui amewakosea nini washabiki wa mpira, anahofia usalama wa familia yake, anasema mpira uko damuni mwake lkn umevamiwa, anajua kuuelezea, kuuchambua, kuuandika, kuucheza na hata kuufundisha lkn kwa tathmini aliyoifanya anaona bora aendelee na maisha mengine.

Amesema ana kazi nyingi za kufanya za kumuingizia kipato ikiwemo Manara TV na kwamba mpira haujampa manufaa yoyote maishani mwake.

Amesema haitaji ukuu wa wilaya wala ukuu wa mkoa wala uwaziri kwa sababu hana uwezo wa kuhamasisha mifugo wala nn, ila in few next days ataitisha Press kuachana kabisa na mambo ya mpira.

Hamtanisikia tena kuongelea mambo ya Simba wala Yanga, nikiacha nimeacha kabisa, si mnanijua, ni kama ninapoachaga mke sirudii tena.

In my point of view, ukiona amefikia hapo jua huko aliko sasa ameshatibuana nao.
 
Kuucheza πŸ˜‚

Kuuandika πŸ˜‚πŸ˜‚

Kuuchambua πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Kuufundisha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Kuuelezea πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Mpira haujaninufaisha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nilijua tu kama issue ya yeye kuomba kurudi Simba ikishajulikana na wahafidhina wa Yanga itageuka balaa jipya. Sasa ndiyo yameshakuwa haya.

Ila siku Try Again akiondoka kwenye ile nafasi pale Simba, basi mtarajie Manara akifanya press nyingine ya kutangaza kurudi kwenye mpira na atarudi Simba.

Ova
 
Hapo alipo anatamani sana angepata misifa ya kuhamasisha game ya Simba na Al ahly.

Anatamani aje apate nafasi walau ya kupiga picha na Rais wa FIFA

Kawekwa kando hata kwenye hamasa za timu ya Taifa, ni mwendo wa kimyakimya hadi anatamani kususa.
 
Kaona nafasi imeshazibwa na Ally Kamwe na ni kama Yanga wamemsusa kimtindo, akimaliza mda ataanza kujikomba tena kwa simba trust me!

Alipokuwa msemaji wa Simba nilianzisha hadi threads humu kwamba huyu jamaa hafai kuwa msemaji wetu Simba,kila saa ni kutukana na kukejeli Yanga,kuzungumzia wapinzani ni 98% na kuzungumzia timu na malengo ya timu 2% ,alipoondoka nilifurahi sana
 
Akiwa kwenye tamasha la Wasafi jana pale Arusha, Haji Manara ameahidi siku si nyingi ataita Press kwa ajili ya kuwaaga watu wa mpira.

Amekaririwa akiongea laivu kuwa mpira umemtengezea sana uadui, hajui amewakosea nini washabiki wa mpira, anahofia usalama wa familia yake, anasema mpira uko damuni mwake lkn umevamiwa, anajua kuuelezea, kuuchambua, kuuandika, kuucheza na hata kuufundisha lkn kwa tathmini aliyoifanya anaona bora aendelee na maisha mengine.

Amesema ana kazi nyingi za kufanya za kumuingizia kipato ikiwemo Manara TV na kwamba mpira haujampa manufaa yoyote maishani mwake.

Amesema haitaji ukuu wa wilaya wala ukuu wa mkoa wala uwaziri kwa sababu hana uwezo wa kuhamasisha mifugo wala nn, ila in few next days ataitisha Press kuachana kabisa na mambo ya mpira.

Hamtanisikia tena kuongelea mambo ya Simba wala Yanga, nikiacha nimeacha kabisa, si mnanijua, ni kama ninapoachaga mke sirudii tena.

In my point of view, ukiona amefikia hapo jua huko aliko sasa ameshatibuana nao.
Uwe na akili HAJAWAHI KUONGEA UKWELI HAJI TOKA AMEZALIWA
 
Back
Top Bottom