Elections 2010 KUMEKUCHA - 5: Ushindi wa Nani Igunga na kwanini..

Kura alizopata mgombea wa CUF zilikuwa ni za wapinzani wote.Ngoja nichukulie mfano huu....Kuna wanaCDM waliompigia Mahona (CUF) simply CDM haikuwa na mgombea,na sasa kwakuwa CDM ina mgombea,watampigia na hvyo kuufanya mtaji wa Mahona (CUF) kupungua so unapofanya tathmini hilo nalo ni la kuzingatia.@Mzee Mwanakijiji

Kama hii ingekuwa kweli watu wengi zaidi pia wangejitokeza kumpigia mgombea wa Urais wa CDM. lakini Dr. Slaa alipata kama kura 6000 hivi Igunga na mgombea wa Uais wa CUF alipata kiasi gani?
 
Pamoja na haya yote, tuweke na factor ya kuongezeka kwa uelewa/kufunguka kwa wananchi kwamba ilivokuwa 2010 possibly c ilivo leo watu wamezidi kuelewa kumbe inawezekana kabisa ccm kushindwa inaweza kupunguza kura walizopata mwaka jana kupitia rostam.
 
Yaani CCM ingekuwa ni chama cha mastrategistS na wanaoongozwa na principles basi wangekubali kuupoteza uchaguzi huu, lakini sio sasa. Wangekubali toka mwanzo kwa vitendo. Kwanza wangemfukuza Rostam, pili wasingemteua Kafumu kugombea na ufunguzi ule usingefanywa na Mkapa. Hapa ndiyo wangeipigilia vizuri ile dhana yao ya kujivua gamba na kweli vigogo mafisadi wangetishika na wengine wangejiondoa wenyewe. Sasa ilipofika mahali wakaanza kukompromize principles, mara ooh Nape, Kilango, Sitta, Mwakyembe wasiende huko. RA yuleyule waliyemwita Gamba wakampigia magoti awepo ufunguzi wa kampeni ni Bao lakudumu walilojipiga CCM.

CCM: Kwa mambo yalivyoenda mpaka sasa CCM ishinde au isishinde imeshajimaliza
1. CCM wamepoteza ile commanding lead kwenye uchaguzi, uchaguzi wowote kuanzia sasa itakuwa ndiyo mwendo huu, sasa tusijeshangaa siku JK anenda kumpigia kampeni diwani wa Kawe.

2. CCM haiaminiki tena, hata wale waliokuwa sometimes in sometimes out, kwa matukio hayo ya Igunga ndiyo basi tena.

3. CCM is not for us but against us, hii ndiyo msg inayoresonate kwa vijana wa kitanzania.

4. CCM ni lazima inunue affection kwani ile natural is gone, gone in Igunga.

5. Uchaguzi huo wa Igunga ni mwanzo tena wa migogoro mingine, utawasikia watakapoanza kutuhumu wenzao watakaodaiwa kuhujumu.

6. Stori ya Gamba ndiyo imeenda hivyo, I will alwayz remember ile thread yako ya Mapacha watatu should stay put, CCM hana cha kuwafanya.

CUF:

1. Uchaguzi huu pia una maana kubwa sana kwa chama cha CUF kwani mgombea wao akipata say chini ya 10% of the votes ndiyo kitakuwa kimepoteza relevance machoni pa watanzania.

2. Habari ya ndoa ya CUF na CCM imeonekana kuresonate vizuri sana huko Igunga, na hii ndiyo hasa sababu ya CUF ku-retract kuishambulia CHADEMA kama walivyoonekana mwanzo. Wapiga kampeni wa CUF wakiiandama CHADEMA hata logically inaonekana aah! si ni CCM B hao.

3. Habari kwamba huku ni kwao Lipumba na CUF kuwa na influence mkoa wa Tabora inatakiwa ithibitishwe na uchaguzi huu otherwise watajikuta wanaingia ile ligi ya akina TLP, DP, UDP etc.

CHADEMA:

1. Amini usiamini na tuweke mbali ushabiki, chama chenye advantage kubwa uchaguzi huu ni CHADEMA all they need hata ikitokea bahati mbaya hawajashinda ni kupata kura very close na atakayetangazwa mshindi. Ikumbukwe kuwa wao hawakusimamisha mgombea hapo 2010 lakini kwa fair analysis wameihenyesha CCM mpaka aibu.

2. CHADEMA wakitangazwa washindi uchaguzi huu basi ndiyo itakuwa referendum 2015 na chaguzi nyingine kabla ya hapo zitakuwa na ahueni kidogo maana inaonyesha mbinu za CCM zimeshajulikana. Hii itafanya hata zile kesi za kipuuzi puuzi za kupinga matokeo ya wabunge wa CDM zisiingiliwe na watawala maana inajulikana wazi kwamba nafasi kwa CCM ni ndogo mno hata kama kutafanyika re-election.

3. CHADEMA baada ya uchaguzi huu itakuwa imejiongezea mtaji mkubwa kisiasa hasa kwa yale majimbo ambayo bado ni loyal kwa CCM.

Hivyo basi kwa majumuisho ya hoja, atakayetangazwa mshindi kwenye uchaguzi huu bado ni kitendawili. Lakini kama nilivyoainisha hapo juu CCM ndiyo ataibuka looser atangazwe awu asitangazwe mshindi unless it is a clear margin of say more than 30%. Any signs of that?
 
I think the opposite is true.
Voter turnout kubwa ni advantagous kwa CCM.
Sababu zilizotolewa hazimuaffect a typical CDM voter, CDM wapo very open na upenzi wao na vijana ni wengi, kwa hiyo kuwatisha si rahisi.
Kutishwa na kuwekewa vituo mbali, au foleni huwa zinamdiscourage mpiga kura wa CCM. Wengi ni wazee na kina mama ambao watapenda kupiga kura ila kama kuna issue ndogo wanakaa tu nyumbani.
 
Igunga ina mapungufu mengi sana kwa sasa hivi kwa tasmin iliyofanywa. Hamna maboresho yoyote yaliyofanya na NEC.
  • Waliotimiza miaka 18 after october 2010 hawawezi kupiga kura
  • Madaftari ya kudumu ya wapiga kura hayajaboreshwa
  • Hamna hakiki iliyofanywa kwenye daftari ya wapiga kura
  • Wale wapiga kura waliopoteza shahada zao hawajafanyiwa marekebisho.
  • Vp watu kutoka nje ya Igunga wakipiga kura nani atafahamu
Na mengine mengi...ila ngoja tuone, manake hata zile sharia za uchaguzi naona vyama vyote viliikaataa, isitoshe naona hata hawa TAKUKURU sijui wamefia wapi...CCM wanagawa wali na sukari kule ila nothing happened, je siku ya uchaguzi itakuwaje?
 
Asante Mwanakijiji kwa uchambuzi makini wa namba, asilimia na hoja. Mimi narudia ule ubashiri wangu nilioutoa mara tuu baada ya RA kujivua gamba.

CCM itashinda kwa kishindo kwa sababu watu wa Igunga ni watu wa ajabu sana!. Nimesema ni watu wa ajabu sana kwasababu nawafahamu fika ndugu zangu Wanyamwezi (mtanisamehe sana!), sio watu wa msimamo!. Natamani wangekuwa kama watu wa Tarime kwenye ule uchaguzi mdogo, lakini very unfortunately, they are not!. Kwa Wanyamwezi ninaowafahamu mimi, T.shirt, kofia, doti ya kanga na shibe ya siku moja tuu inatosha kumaliza kila kitu kesho yake!

RA alipojivua gamba, nilisema mbunge mpya wa Igunga, ni yule tuu atakayenyanyuliwa mkono na RA. Pia nikasisitiza, hata CCM ikimvua gamba, AC na EL, chama chochote watakacho simama, hata kiwe unknown vipi au insignifant vipi, watashinda simply kwa sababu watu wao, wanawaambudu!. Hawa ni miungu watu. Niliangalia jinsi walivyopokelewa kwao baada ya kuyafanya walioyafanya, ni kama walivyompokea Jairo pale wizarani kwake, kama mfalme fulani!, RACHEL nao ni wafalme maeneo yao, hivyo kwa Igunga, mwana mfalme ni Dr. Kafumu, tena sio tuu ni mwana mfalme, bali ni mwana wa mungu mtu, RA!.

Nimefuatilia ule utabiri wa idadi ya wapigakura wa uchaguzi wa 2010 Igunga, wale wengine wote ambao hawakujitokeza, wengi wao ni waumini wa mungu yule yule, hivyo 2010 hawakuona haja ya kujitokeza kwa sababu walisha muaminia mungu mtu wao kwa ushindi wa asilimia 100%, wale waliojiotokeza, walijitokeza tuu ili kumuendorse!. Kwa vile kwa sasa mgombea wa mungu wao na chama chake ambacho wanaamini ndio kimeubwa kuitawala milele, anapokumbana na kitisho cha Chadema, then this time, watajitokeza kwa wingi, mamia kwa maelfu, kwenda kuokoa jahazi!, nani hapendi pilau, tisheti na kofia!.

Nilibahatika kushughudioa chaguzi ndongo kadhaa na ikiwemo Busanda na Biharamulo na kushuhudia jinsi wananchi wa mijini walivyohamanika na Chadema, lakini siku ya siku, kilichofuatia sote tunakijua, na matokeo mliyaona, hivyo kwa Igunga, sio tofauti ya Biharamulo na Busanda.

Angalizo, nawaombeni sana, wana JF wenzangu, msihamanike na umati kwenye mikutano ya kampeni, wengi kwenye umati hizo sio wapiga kura.

Kwa kawaida, mimi hujitambulisha kama mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo binafsi ningependa sana kuona Chadema ikiongeza jimbo, lakini nimeishajiandaa kupokea taarifa za maumivu!.

Pasco.
 
Una tatizo hapo; vijana wengi sidhani kama wamepiga kura; wengi waliotimiza miaka 18 kuanzia Oktoba hadi Septemba mwaka huu hawapigi kura. Wengi waliokuwa shule wameenda shule au vyuoni. Watakaoamua kupiga kura ni watu wazima zaidi kuliko vijana. Vijana ni washingiliaji zaidi.. kama kungekuwa na uandikishwaji tena wa wapiga kura basi vijana wengi wangejitokeza.
Sijui hao vijana waliofikisha miaka 18 kuanzia octoba10 na sept.11 ni asilimia ngapi lakini ni insignificant ukilinganisha na vijana waliojiandikisha uchaguzi uliopita kati ya 170,000. Ukitaka kuangalia hivyo basi kuna factors nyingi sana itabidi ku-consider mfano wazee wangapi wamefariki, waliopoteza vitambulisho nk nk. Tuongelee waliopo ambao walipiga kura(50,000) na ambao hawakupiga kura wale 120,000 lets say at least quarter of 120,000 yaani 30,000 wajitokeze + 50,000 waliopiga mwaka jana to make 80,000 voters. Sasa kati ya hao 80,000 tuangalie ni asilimia ngapi ya vijana watakaopiga kura.

Nakubaliana na wewe kuna walio mashuleni sijui ni asilimia ngapi ila kumbuka umri wa kuwa shuleni ni 18-22(wapiga kura) zaidi ya hapo vijana wengi ni jobless wako mitaani-Igunga. Mimi bado nafikiri vijana watakuwa wengi ikichangiwa na elimu iliyotolewa huko na mwamuko wa uelewa wa mambo ya siasa unavyozidi kukua, hata huo ushangiliaji unaousema ni hamasa na kampeni tosha kuwafanya watu waliojiandikisha kujitokeza siku ya kupiga kura. Hata hivyo haya yote tunayojadili yanategemea iwapo uchaguzi unakuwa free and fair.
 
Hata kama CDM haitashinda Igunga mm sijali .

"When Nature has work to be done, she creates a genius to do it. "

The guy who changed this world by inventing electricity did million of trials but succeed only once. And now here we are . ELECTRICTY.

We will try , and try and try until they can not afford not to accept us ....Peoples pawaaaaaaaa
 
Brother i give you credit for this......UNTIL THEY CAN NOT AFFORD NOT TO ACCEPT US
 
Sijui hao vijana waliofikisha miaka 18 kuanzia octoba10 na sept.11 ni asilimia ngapi lakini ni insignificant ukilinganisha na vijana waliojiandikisha uchaguzi uliopita kati ya 170,000. Ukitaka kuangalia hivyo basi kuna factors nyingi sana itabidi ku-consider mfano wazee wangapi wamefariki, waliopoteza vitambulisho nk nk. Tuongelee waliopo ambao walipiga kura(50,000) na ambao hawakupiga kura wale 120,000 lets say at least quarter of 120,000 yaani 30,000 wajitokeze + 50,000 waliopiga mwaka jana to make 80,000 voters. Sasa kati ya hao 80,000 tuangalie ni asilimia ngapi ya vijana watakaopiga kura.

Nakubaliana na wewe kuna walio mashuleni sijui ni asilimia ngapi ila kumbuka umri wa kuwa shuleni ni 18-22(wapiga kura) zaidi ya hapo vijana wengi ni jobless wako mitaani-Igunga. Mimi bado nafikiri vijana watakuwa wengi ikichangiwa na elimu iliyotolewa huko na mwamuko wa uelewa wa mambo ya siasa unavyozidi kukua, hata huo ushangiliaji unaousema ni hamasa na kampeni tosha kuwafanya watu waliojiandikisha kujitokeza siku ya kupiga kura. Hata hivyo haya yote tunayojadili yanategemea iwapo uchaguzi unakuwa free and fair.

Fikiria hivi kati ya watu lakini na sabini elfu waliojiandikisha waliopiga kura ni arobaini na tisa elfu hivi; kati ya hao elfu thelathini na saba hivi waliichagua CCM sawa na asilimia zaidi ya sabini ya waliopiga kura. Sasa hawa vijana wako wapi? Na ni vijana wanafanya shughuli gani? Unafikiri wana msisimko zaidi Igunga sasa hivi kuliko wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Urais mwaka jana? Unafikiri kwamba kuna uwezekano wa watu hata kukaribia hamsini elfu kupiga kura this time? I doubt it. I stand to be corrected.
 
Mwanakijiji nakupa BiG yES,nathani hata matokeo ya urais wa Zambia kwa kuchaguliwa chama mbadala yameongeza msisimko kwa wapigakura wa Igunga kuyakaribisha mabadiliko.Hata hivyo time will tell
 
Mzee mwanakijiji

Heshima yako mkuu uchambuzi wako mzuri sana lakini nina hoja juu ya uchambuzi wakokama ifuatavyo

1.Uchambuzi huu unatokana na maono yako binafsi na huja fanya utafiti wowote unaweza kutupa taswila halisi ya sample ulio tumia,methodology uliyo tumia na assumption ulizo tumia kufikia hitimisho

2.Siasa Zatanzania hazitabiliki hata kidogo kwa sababu hatuna ukabila,urangi na udini ulio wazi kabisa ingawa wakubwa wanajaribu kuutumia kama kete ya kisiasa

3.Uchambuzi wako hauja chukulia hata kidogo misingi ya mageuzi na harakatizake kisiasa katika taifa hili na hauja eleza hata kidogo upepo wa mageuzi uliopo nchini kwa sasa na mwelekeo uko vipi juu ya upepo huu

4.Uchambuzi wako hauja eleza hata kidogo mabadiliko ya kifikra katika jamii yaleo ukilinganisha na mwakajana ambapo umeweka msingi mkuu wa hoja yakoya kura na wagombea Igunga.

5.Na kama utazungumzia mageuzi ya kifikra katika jamii hii toka mwakajana 2010 wakati wa uchaguzi mpaka leo utajua nichama gani kime wekeza katika hili,ukitambua hili hutapata shida kujua mshindi igunga ninani kwasababu hoja ya msingi unayo

6. Bila ushabiki wowote huwezi kupata shida kujua wananchi wa naamini chama gani na chenye mlengo gani juu ya taifa hili kama utakosa kabisa mwelekeo na kutambua nichama gani wananchi wanakiamini jiulize kwanini siri za serikali zinavuja sana na zina vuja kuelekea chama gani

Naomba kuwakilisha
 
Yaani CCM ingekuwa ni chama cha mastrategistS na wanaoongozwa na principles basi wangekubali kuupoteza uchaguzi huu, lakini sio sasa. Wangekubali toka mwanzo kwa vitendo. Kwanza wangemfukuza Rostam, pili wasingemteua Kafumu kugombea na ufunguzi ule usingefanywa na Mkapa. Hapa ndiyo wangeipigilia vizuri ile dhana yao ya kujivua gamba na kweli vigogo mafisadi wangetishika na wengine wangejiondoa wenyewe. Sasa ilipofika mahali wakaanza kukompromize principles, mara ooh Nape, Kilango, Sitta, Mwakyembe wasiende huko. RA yuleyule waliyemwita Gamba wakampigia magoti awepo ufunguzi wa kampeni ni Bao lakudumu walilojipiga CCM.

CCM: Kwa mambo yalivyoenda mpaka sasa CCM ishinde au isishinde imeshajimaliza
1. CCM wamepoteza ile commanding lead kwenye uchaguzi, uchaguzi wowote kuanzia sasa itakuwa ndiyo mwendo huu, sasa tusijeshangaa siku JK anenda kumpigia kampeni diwani wa Kawe.

2. CCM haiaminiki tena, hata wale waliokuwa sometimes in sometimes out, kwa matukio hayo ya Igunga ndiyo basi tena.

3. CCM is not for us but against us, hii ndiyo msg inayoresonate kwa vijana wa kitanzania.

4. CCM ni lazima inunue affection kwani ile natural is gone, gone in Igunga.

5. Uchaguzi huo wa Igunga ni mwanzo tena wa migogoro mingine, utawasikia watakapoanza kutuhumu wenzao watakaodaiwa kuhujumu.

6. Stori ya Gamba ndiyo imeenda hivyo, I will alwayz remember ile thread yako ya Mapacha watatu should stay put, CCM hana cha kuwafanya.

CUF:

1. Uchaguzi huu pia una maana kubwa sana kwa chama cha CUF kwani mgombea wao akipata say chini ya 10% of the votes ndiyo kitakuwa kimepoteza relevance machoni pa watanzania.

2. Habari ya ndoa ya CUF na CCM imeonekana kuresonate vizuri sana huko Igunga, na hii ndiyo hasa sababu ya CUF ku-retract kuishambulia CHADEMA kama walivyoonekana mwanzo. Wapiga kampeni wa CUF wakiiandama CHADEMA hata logically inaonekana aah! si ni CCM B hao.

3. Habari kwamba huku ni kwao Lipumba na CUF kuwa na influence mkoa wa Tabora inatakiwa ithibitishwe na uchaguzi huu otherwise watajikuta wanaingia ile ligi ya akina TLP, DP, UDP etc.

CHADEMA:

1. Amini usiamini na tuweke mbali ushabiki, chama chenye advantage kubwa uchaguzi huu ni CHADEMA all they need hata ikitokea bahati mbaya hawajashinda ni kupata kura very close na atakayetangazwa mshindi. Ikumbukwe kuwa wao hawakusimamisha mgombea hapo 2010 lakini kwa fair analysis wameihenyesha CCM mpaka aibu.

2. CHADEMA wakitangazwa washindi uchaguzi huu basi ndiyo itakuwa referendum 2015 na chaguzi nyingine kabla ya hapo zitakuwa na ahueni kidogo maana inaonyesha mbinu za CCM zimeshajulikana. Hii itafanya hata zile kesi za kipuuzi puuzi za kupinga matokeo ya wabunge wa CDM zisiingiliwe na watawala maana inajulikana wazi kwamba nafasi kwa CCM ni ndogo mno hata kama kutafanyika re-election.

3. CHADEMA baada ya uchaguzi huu itakuwa imejiongezea mtaji mkubwa kisiasa hasa kwa yale majimbo ambayo bado ni loyal kwa CCM.

Hivyo basi kwa majumuisho ya hoja, atakayetangazwa mshindi kwenye uchaguzi huu bado ni kitendawili. Lakini kama nilivyoainisha hapo juu CCM ndiyo ataibuka looser atangazwe awu asitangazwe mshindi unless it is a clear margin of say more than 30%. Any signs of that?

Uchambuzi wako unaleta mantiki fulani , safi sana..!
 
Kwa uchambuzi wako M.Mwanakijiji, inaonesha wazi kuwa CCM imepoteza uhalali wa kuongoza. kama kila idara inayohusika kuhamasisha watu kupiga kura ingefanya kazi ipasavyo,na wananchi wasingetishiwa usalama wao(Kiufupi uchaguzi ulio katika mazingira ya amani, haki na huru,tangu kampeni mpaka kutangazwa matokeo), basi anguko la ccm ni dhahiri. Hii inaonesha kuwa CCM haikubaliki. Kama haikubaliki, lakini inashinda kwa hila, tutaendelea na hali hii mpaka lini?

Vyovyote matokeo yatakavyokuwa, CDM imedhihirisha kuwa CCM haiko salama hata kwenye ngome zake. Leo hii hata uchaguzi ufanyike Dodoma, CCM haiko salama, hii ni hatua nzuri inayoonesha CCM imeshadhoofika, ni kiasi cha kuzidi kuibana kwa kila namana iwezekanayo.
 
raia mmoja amenitumia sms kuniomba nianze kuonyesha interest ya ubunge Dodoma.....nimeshangaa sana...anasema mchakato ulishaanza mtaani kwao na wameona ni vyema wanitumie habari hii----- bado natathmini...

Mwanakijiji, una akili kama Mnyika, lakini.... mmesahau kuwa Rostam nyuma ya pazia hataki CCM ishinde?---- sasa gawa zile kura zake into 2!
 
Kama hii ingekuwa kweli watu wengi zaidi pia wangejitokeza kumpigia mgombea wa Urais wa CDM. lakini Dr. Slaa alipata kama kura 6000 hivi Igunga na mgombea wa Uais wa CUF alipata kiasi gani?

Dr Slaa alipata Kura 8,874 na Lipumba alipa kura 3,181 na Jk 34,000 kwenye uchaguzi wa 2010
Mahona alipata kura 11,321
Mwanakijiji ukijaribu kufanya tathni ya akina utaona Dr Slaa alipa kura nyingi kuliko Lipumba, na CDM haikuwa na Mgombea hivyo wale waliompenda Dr ilibidi wampe Mahona. Sasa wenye Nyumba wamerudi.

Jumla ya wapiga kura wenye vitambulisho vya kupigia kura igunga ni 170,000 na ushee hivi. Huwa wanajitokeza kama theluthi moja ya wapiga kura wote.

Kweli Igunga kuna kazi kweli kutabiri. ILa kwa Utabiri wangu kama Dr Slaa alizoa kura 8000 kwa kufanya mkutano mmoja au miwili itakuwaje leo kamfanyia mgombea wake mikutano zaidi ya 40.

Nina amini CDM itaondoka mshindi kwa asilimia 45 ya kura zote zitakazopigwa.
 
Nilibahatika kushughudioa chaguzi ndongo kadhaa na ikiwemo Busanda na Biharamulo na kushuhudia jinsi wananchi wa mijini walivyohamanika na Chadema, lakini siku ya siku, kilichofuatia sote tunakijua, na matokeo mliyaona, hivyo kwa Igunga, sio tofauti ya Biharamulo na Busanda.

Pasco una hoja lakini kumbuka kitu kimoja dynamics za siasa zimebadilika mno toka chaguzi zile za busanda na biharamulo, wakati ule kumbuka Chadema ilikuwa na wabunge wangapi?????? Umaarufu wa JK ulikuwaje????? CCM yenyewe ilikuwaje? Gamba lilikuwa wapi?

Kwa kukumbusha tu:

1. CHADEMA ilikuwa na wabunge nadhani watano na ni kipindi hiki hizo tuhuma za kwamba ni chama cha wachaga na kifamilia zilipamba moto, leo CHADEMA ina wabunge 48 karibu mara kumi zaidi ya wakati ule. Wabunge hao wametoka maeneo mbalimbali ya nchi.

2. JK that time alikuwa maarufu kweli, mtu wa watu, mpole, handsome, leo vipi?

3. CCM ya wakati ule na kipindi kile huu uchaguzi wa Igunga wasingekuwa wanahaha namna hii, mkuu suala si mikusanyiko ya watu tu kipindi kile hata kuwasikiliza wapinzani kwenye majimbo kama Igunga ilikuwa ni kama mtu anavunja sheria ya nchi.

4. Sekeseke ya Biharamulo wakati ule ndiyo imefanya CHADEMA iliitwae jimbo lile mwaka jana, pia Busanda matokeo ya mwaka jana yalikuwa too close.

5. Kingine kikubwa ni kwamba Igunga si kisiwa yaliyotokea mwaka jana waliyaona na kuyasikia na hawakuwa nyuma kumchagua Dr. Slaa.

"Mkuu Pasco unapoona chama kikongwe kama CCM pamoja na advantages zote kilichonazo eti wanaahirisha kampeni in such a heated environment kusubiri helikopta mbazo hata hivyo hazikuja, jua kwamba hali si shwari and something is very very wrong"

Hivyo basi mimi binafsi naona matokeo haya lolote linaweza kutokea, ila CHADEMA ina advantage kubwa sana hata isipotangazwa mshindi cha msingi tu wawe wa pili na wawe close na yule wa kwanza. Karata za uchakachuaji za CCM inabidi isiwe tu kuihakikishia CCM ushindi bali na kuisukuma CHADEMA iwe ya tatu. Lakini kwa hali halisi ilivyo hilo haliwezi kutokea. CCM wakitangazwa washindi ndiyo kwaaanza watazidi kuwaongea hasira wananchi. Wasiposhinda watazomewa na itakuwa ndiyo their beginning of their end. In short CCM imebanwa btn a rock and a hard place. Let's wait and see
 
Mwanakijiji uchambuzi mzuri ila kuna mambo kadhaa nimeshindwa kukuelewa na kuna assumptions kadhaa hujazi consider kwenye analysis yako sijui ni makusudi au kwa kutokujua..

1. Dhana ya "vote suppression"
:
kwenye hili umedai CCM itajitahidi sana kupunguza kura kwa njia ya vitisho ili kina mama, wasichana na wazee wengi wawe discouraged kwenda kupiga kura. Je suala hili litawanufaisha vipi CCM wakati wapiga kura wao wengi ni wazee na kina mama ?

2. Kura za vijana:
Kwenye uchambuzi wako umekubaliana na dhana ya CDM kuungwa mkono na Vijana lakini ukadai kuwa vijana ni "washangiliaji tu" ukizingatia kuna kundi la vijana ambao wametimiza miaka 18 tokea oktoba 2010 mpaka oktoba 2011 ambao hawajajiandikisha hapo hapo ukadai kuna wengine kwa wakati huu watakuwa mashuleni na vyuoni. Kwenye hili nakubaliana na wewe lakini pia ukashindwa kuelezea role ya vijana kwenye uhamasishaji wa kupiga kura za mabadiliko: Vijana ambao wengi wao wana uelewa kiasi kutokana na elimu waliyopata iwe ya kata au yoyote ile wanaweza kutumika kuwashawishi wazee na mama zao kwenye upigaji kura ambao utakuwa against ccm.
 
Back
Top Bottom