KUMEKUCHA - 5: Ushindi wa Nani Igunga na kwanini.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KUMEKUCHA - 5: Ushindi wa Nani Igunga na kwanini..

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 28, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kumekucha-5.png
  Uchaguzi wa Igunga utaamuliwa siku chache zijazo. Mshindi atashinda siyo kwa uzuri wa hoja tu bali pia kwa mbinu na mikakati. Kama nilivyosema kwenye makala nyingine uchaguzi wa Igunga utaamuliwa na idadi ya watu watakojitokeza kupiga kura. Naamini kabisa kuwa hadi hivi sasa kwa kuangalia mwelekeo wa joto la uchaguzi ushindi unaweza kwenda kwa yeyote. Lakini ni CCM na CDM ambao wanaweza kujikuta wote wawili wanapoteza Igunga - yote kutegemeana na idadi ya wanaojitokeza kupiga kura.

  Ila CCM Ishinde:

  Ila chama cha Mapinduzi kishinde Igunga formula ile ile lazima itumike nayo ni kuhakikisha idadi ndogo zaidi ya watu wanajitokeza kupiga kura. Ila inachohitaji ni idadi kubwa ya wanachama wake wajitokeza katika ile idadi ndogo ya wapiga kura. Hii ndiyo kanuni iliyotumika kwa kiasi kikubwa mwaka jana. Kati ya watu 170,000 waliojiandikisha kupiga kura ni kama watu 49,000 tu waliojitokeza kupiga kura sawa na asilimia kama 23 hivi. Lakini katika hao mgombea wa CCM Rostam alishinda kwa asilimia 73 akikusanya kura 35,000 hivi. Kama "trend" hii itarudiwa basi CCM yaweza kuwashangaza watu kwa kushinda siyo kwa wizi kama wengi wanavyofikiria bali kwa kutumia mbinu ya suppression of votes - yaani kugandamiza upigaji kura. Hii - kwa mtu anayefuatilia - imeshaanza na kwa kweli naamini inafanikiwa sana. Baadhi ya mbinu ambazo zinatumika kwa kiasi kikubwa ni za Kisaikolojia.

  • - Kutishia umwagikaji damu - hii ni mbinu ya kuwafanya watu wahofie kujitokeza kupiga kura
  • - Kutishia uwezekano wa kutokea vurugu siku ya kupiga kura - hii ina lengo la kuwatisha kina mama na wazee kwenda kupiga kura
  • - Vituo kuwa mbali sana na maeneo ya makazi - hii inawafanya watu wafikirie mara mbili kwenda kupiga kura hasa kama kuna uwezekano wa hayo mambo mawili ya kwanza.
  • - Kutokana na mawili ya kwanza kumwaga polisi na hata jeshi ili kuonesha kuwa kuwa hali ya hatari yaweza kutokea - lengo ni kuwafanya watu wawe na hofu ya kujitokeza - hii inawatisha vijana hasa wasichana ambao kukurukakara za polisi hawajazizoea.
  • - Udini - hii ni mbinu nyingine mbaya sana hasa kwenye mazingira ya Igunga ambapo wagombea karibu wote ni Wakristu. Hii ni mbinu ya kugandamiza kura za Waislamu na hivyo kuwafanya wengi wao wasite kujitokeza kupiga kura Igunga. Lakini pia inaweza kutumika - naamini kihalali kabisa - kuongeza kura za CCM kwa kutaka zipigwe kura za kundi (group voting). Bahati mbaya kura za namna hii pia huwa zinamatokea yasiyotakiwa - tuliona kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana - kwamba makundi mengine nayo yatapiga kura za kidini.
  • - Msaada mkubwa huja siku ya kupiga kura hasa kama NEC inaanza kuwa na matatizo na hivyo watu wanakuja kupiga kura na kukutana na matatizo kibao na kuamua kukata tamaa kwa sababu wanashughuli zao mbalimbali.

  KIMSINGI: Ili CCM iweze kushinda kwa kuwepo wapiga kura wachache hofu inahitajiwa. Hivyo, siku hizi zinavyokwenda matuko na kauli za kuwatia hofu wananchi wasijitokeze kwenda kupiga kura kwa hofu ya kudhurika au kujikuta kwenye matatizo. Hofu hii itawazuia kina mama na wanawake kwenda kupiga kura. Lakini pia itawatisha wazee na baadhi ya vijana ambao wamelelewa katika "amani" kama hali ya kutokuwa na vurugu na hivyo matukio mbalimbali yaliyoripotiwa sana kabla ya uchaguzi yatawafanya waone kabisa kuwa siyo Utanzania kwenda na kuwa sehemu yenye vurugu. Endapo upigaji kura utakuwa chini ya asilimia 25 (kama mbinu hizo zitafanikiwa sioni upigaji kura zaidi ya asilimia hiyo), CCM itashinda kwa karibu asilimia 60.

  Ili CDM ishinde
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaweza kushinda vizuri kabisa na kuweka historia nchini. Lakini kushinda kwake kutategemea sana idadi ya watu watakaojitokeza kupiga kura. Hivyo siku hizi chache zilizobakia CDM ina kazi kubwa ya kuwatia moyo wapiga kura wajitokeze kupiga kura "no matter what". Hapa patakuwa pagumu. Haitoshi kuwataka watu wasubirie kura wazilinde kazi kubwa iko katika kuwafanya watu watoke majumbani mwao kwenda kupiga kura bila kutishwa na mtu yeyote. Kwa maneno mengine CDM ni lazima iwahakikishie watu usalama na utulivu kwenda kupiga kura.

  - CDM iihakikishe kuwa inashirikiana na polisi kuhakikisha usalama na isikubali polisi watumie mbinu za kuwatisha wananchi
  - CDM ihamasishe vijana - hasa mwanzo wa siku yenyewe wajitokeze kwenda kupiga kura. Kama watu wanaogopa kuanza kutoka mapema ni rahisi sana kwa watu wengine nao kufuatia. Hivyo, viongozi na makada wa CDM watumie muda mwingi uliobakia kuhamasisha watu kupiga kura na kuwaambia wasiogope kupiga kura siyo tu kwa sababu ni haki yao (kitu ambacho wengi wanakijua) bali kwa sababu ndio sauti yao na wasikubali kunyamazishwa iwe kwa baruti au suti.
  - CDM kuhamasisha watu kusaidiana kusafirishana kwenda kwenye vituo vya kupigia kura. Hii ni pamoja na watu wenye baskeli, vibajaji au magari yao. Ikumbukwe kuwa Sheria inakataza kukodisha (kwa malipo) magari kwenda kupiga kura; lakini haikatazi magari kutolewa bure kwa ajili ya shughuli hiyo - one of those loopholes za sheria ya gharama za uchaguzi. CDM ihakikishe kwa upande wake kuwa yeyote anayetaka kupiga kura siku hiyo anapiga kura hata kama kwa kusindikizwa, kubebwa, kuendeshwa au kushikwa mkono.


  KIMSINGI ili CDM iweze kushinda ni lazima iwape wananchi ujasiri na kuwatia moyo wajitokeze kwa wingi kupiga kura. Wasitishwe, wasiogopeshwe wala wasihofia lolote. Tanzania bado ninchi huru na kila mtu ana haki kama mwingine. Suti, polisi, jeshi au watu wenye ving'ora hawana haki zaidi kuliko wananchi wengine. Hivyo, kazi kubwa iko kwa CDM kuwahamasisha watu kupiga kura - haijalishi kama inahamasisha wanachama wake - kwani haiwezi kushinda kwa kura za wanachama. Bila KUHAMASISHA WATU kujitokeza kupiga kura na kuweza CDM itakuwa na kazi nzito kweli ya kushinda.

  Hivyo, endapo watu watajitokeza kupiga kura kwa kiwango chochote kufikia asilimia 30 au zaidi CDM itashinda kwa kiasi cha 53-57%

  Ili CUF ishinde

  Kwa upande wa CUF ushindi wake unategemea kwa kiasi kikubwa idadi wapiga kura isibadilike sana kama ilivyokuwa mwaka jana. Kwa CUF endapo upigaji kuta urakuwa kama mwaka jana ni wazi kwamba kura zitakazoleta mabadiliko sana zitakuwa ni zile za CDM. Mwaka jana CUF ilipata kama kura 11,000 endapo CCM na CDM zitagawana sana kura zile 40,000 hivi na CUF ikaendelea na kiasi kama hicho basi inaweza kushinda kwa kushangaza watu lakini kwa less then 50 percent.

  Kinyume na watu wanavyofikiria CUF ina faida ambayo CDM haina:

  a. Mgombea wake alisimama kugombea mwaka jana na hivyo jina lake tayari linajulikana na tayari alijitengenezea mashabiki
  b. Mgongano wa CCM na CDM waweza sana kuinufaisha CUF zaidi kwani kama upigaji kura ukifikia hata hiyo 50,000 (kitu ambacho binafsi sitarajii) vyama vya CCM na CDM vinaweza kugawana hata kura 35,000 kati yao!!!

  LA MSINGI hapa ni kuwa CUF inaweza kujikuta inashinda kiti hicho kwa kupata kura chache zaidi kulinganisha na wagombea wengine wakijumlishwa.

  Hata hivyo, kama yaliyotokea kwenye kura za Urais ni ishara ni wazi kuwa Igunga wako huru zaidi kumchagua mtu wanayemtaka kuliko inavyofikiria. Kwa hiyo la kuangalia Igunga ni matokeo ya CUF kwani ndio yataamua kama CCM au CDM inashinda au vyote viwili ambavyo vimepiga kelele sana kujikuta vikiwa nje. Msemo wa "Vita vya Panzi..." waweza kuwa kweli.

  Zaidi kuhusu Igunga na Habari jisomee kijarida chako ukipendacho siku chache kabla ya Uchaguzi Mdogo wa Igunga. Kumbuka wakati wengine wamelala.....
   

  Attached Files:

 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mkuu hebu weka data zako sawa kwanza hiyo asilimia 23% nafikiri ni 29% na RA alipata angalau kura 37,000 si 45,000, Mahona kura angalau 11,000.
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huu uchambuzi wa leo wa Igunga, aliofanya M.Mwanakijiji kwa upande wangu naona kuna ukweli kiasi kikubwa.

  Lakini sidhani kama wengi wetu humu watakubaliana na huu uchambuzi wa siasa za Igunga
   
 4. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kama kweli akutakuwa na uchakachuaji wenye siasa uchwara watalia
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  thanks nimesahahisha nilitaka kuweka 35,000 pale nilikuwa natumia kumbukumbu ya kichwani tu. Niliandika kwa kirefu hili la mahesabu kwenye ile thread nyingine.
   
 6. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,791
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji,

  Sasaivi ni anga kwa anga.
  Tutakomaa nao hadi kieleweke, vijana wana hamasa ya kuona kura yao haiibwi na vibaka.


  Peoples......................Power
   
 7. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,791
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji,

  Hivi ukitazama kwa umakini inawezekana kweli kura zikawa 11,000 na mwingine 35,000 na matokeo ndiyo yakawa hayo! hayo wasifuri sifuri watu wamejiwekea kutimiza wajibu tuu
  Nina wasi wasi sana inawezekana haya matokeo yalikuwa ya kupanga tu, kwa sababu mshindi alikuwa anafahamika.
  Ukweli wa mambo unakuja, tuko makini mkuu
   
 8. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  It's kinda hard to comprehend,
  IN 2010 55,370 people who voted in Hai district.
  Presidential, JK had 35,910, Slaa had 18,513: JK won almost twice as much.
  PARLIAMENTARY, CCM had 23,349 while CDM had 28,585. the difference was 5,236.
  Spoilt votes were astonishingly 176 and 3043 respectively, Hai had one of the best voter turnarround.
  Can someone explain what went on (conclude statistically).
  I think CDM stole some votes here.
   
 9. Michese

  Michese JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ngoja tusubiri tu tuone!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  wanaweza wakajikuta wanalinda kura kiduchu; kubwa ni kuwahimiza watoke kupiga kura kwanza.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  labda Mbowe hakumpigia sana kampeni Dr. Slaa kuwa Rais; alifanya kampeni zaidi ya yeye kuwa Mbunge so the statistics make sense.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Fikiria kama CCM itapata 20,000 tu ya hizo ilizopata mwaka jana; hiyo ina maana gani kwa CDM na CUF?
   
 13. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji asante kwa analysis yako.

  Mapema niliwahi kufanya analysis yangu kuwa kama wapigakura watajitokeza kama walivyokuwa uchaguzi uliopita 50,000 Chadema itashinda kwa 46% kura 23,000 na CCM itapata 35% kura 17,500, CUF 11% kura 5,500, kifupi ni kuwa Chadema kitachukua nusu ya kura ya kila chama CCM na CUF walizopata kwenye uchaguzi uliopita, safari hii wakijitokeza watu wengi zaidi kupiga kura itakuwa advantage kwa Chadema.

  Nikirudi kwa analysis yako kwa vile CCM inategemea wazee na wanawake kitendo chochote cha kuwatia hofu aidha kwa kumwaga polisi au kutumia vijana kuanzisha fujo wazee hasa kina mama wengi hawatajitokeza hivyo kuipunguzia CCM kura. Kwa hali hiyo CDM kitakuwa na advantage kubwa kwa vile ni vijana wengi watakaojitokeza.

  Suala la udini pia halitaisaidia sana CCM kwa sababu kura za waislamu ni fixed ambazo hizo hizo CUF inaziwinda achilia mbali chache watakazopata CDM, kwa msingi huo huo wa udini kuna kura za wakristo zitakazobaki zitaonekana kama sympathy kwa Chadema au counter attack, bila kusahau wagombea wote wa vyama vikuu vitatu ni wakristo hivyo kuwafanya waislamu wengi kutokuwa na interest kwa yeyote na kuwafanya hata wengine kutokwenda kabisa kupiga kura. Hiyo ndiyo analysis yangu.
   
 14. J

  Jonathan Kiula JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
   
 15. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #15
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Kura alizopata mgombea wa CUF zilikuwa ni za wapinzani wote.Ngoja nichukulie mfano huu....Kuna wanaCDM waliompigia Mahona (CUF) simply CDM haikuwa na mgombea,na sasa kwakuwa CDM ina mgombea,watampigia na hvyo kuufanya mtaji wa Mahona (CUF) kupungua so unapofanya tathmini hilo nalo ni la kuzingatia.
   
 16. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Kaka mageuzi yanapotokea hakuna atakayeamini..Mungu yu mwema siku zote
   
 17. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #17
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Kura alizopata mgombea wa CUF zilikuwa ni za wapinzani wote.Ngoja nichukulie mfano huu....Kuna wanaCDM waliompigia Mahona (CUF) simply CDM haikuwa na mgombea,na sasa kwakuwa CDM ina mgombea,watampigia na hvyo kuufanya mtaji wa Mahona (CUF) kupungua so unapofanya tathmini hilo nalo ni la kuzingatia.@Mzee Mwanakijiji
   
 18. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #18
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Amen...@Mageuzi
   
 19. M

  Malabata JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thanks mzee Mwanakijiji 4 ur analysis! Im passing
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
   
Loading...