Elections 2010 KUMEKUCHA - 5: Ushindi wa Nani Igunga na kwanini..

Tatizo letu limelala hapo kwenye kufikiri kwenye kujiokoa kila kinachoparamiwa ni kitu salama. kuna methali ya kiswahili inayosema 'mfa maji haishi kutapatapa.

Mimi sijaona kama nao CDM wako makini kwa wanachokifanya na wala kama wanajua kwa usahihi wapi wanataka kutupeleka kama chama tawala baada ya CCM. Mfano maandiko mengi humu ndani yanaonyesha kwamba wana JF wanaamini kwamba Waislamu(Viiongozi wao?) wanaishabikia CCM kuliko CDM. Lakini sijaona karipio kali kutoka kwa viongozi wa CDM dhidi ya tabia ya sehemu kubwa ya washabiki wao kudhania CDM ni chama kilicho dhidi ya uislamu.

Viongozi wengi wa CDM (Mbowe amejitoa) wanaamin kwamba Peoples powers inamaanisha ni matumizi ya nguvu kwenye kudai "haki" na "Ukamanda" ni ukakamavu kwenye kutokutii sheria na mapambano na Polisi hata bila ya sababu za msingi. hata humu ndani ukisema CDM wamekosea utarukiwa kama kibaka aliyekamatwa akitaka kuiba simu Kariakoo.

CDM kama chama hakina Oganaizesheni ya uhakika kwenye mambo yake ya kila siku na hakuna anayeonyesha kujali.Ukiwauliza watu CDM Makao Makuu ni kiasi gani fedha chama kitatumia kwenye uchaguzi wa Igunga na chaguzi ndogo za Madiwani inawezekana hawajui kabisa kwani fedha nyingi za kuendeshea chama ama "wanakopeshwa" na Mbowe au wanapewa "msaada" na Mzee Ndesamburo.
Ndugu yangu Kigarama, unapoamua kuwa mkweli siku zote, ujue pia kuna price to pay, yaani kuna Vigharama utaingia. Hivyo unapoikosoa Chadema humu kwenye jf, pia ujiendae kupokea malipo ya ukosoaji huo!.

Niliwahi kuposti hii...
[h=3]
CCM Imechokwa
; CHADEMA Haijajipanga!
[/h]
Nilichoambulia niliambulia lakini kwa vile huu ndio ukweli wangu, kila unapotimia nitakuwa nakumbushia.

 
Asante kwa masahihisho.

a. Kwenye demokrasia na kwa mtindo wa mfumo wetu wa uchaguzi mtu yeyote kama anajua kujumlisha anaweza kumjulisha na kujua matokeo kabla ya kutangazwa. Huu ni mfumo unaotumika hata baadhi ya nchi japo wenzetu huwa wanatumia zile exit polls (kuwahoji waliokwishapiga kura) na kutoka hapo wanaweza kukisia matokeo ya jumla yatakuwaje.

b. Kosa kubwa liko kwa vyombo huru vya habari kwani vinategemea tume navyo kutangaza matokeo badala ya kuweka watu wao kila kituo au kufuatilia kila kituo na kujumlisha. Kwa kutumia vyombo vya habari huru kuweza kutangaza mshindi (to call the election) inazuia watu wengine kuchakachua kwa sababu vyombo vya habari itabidi vielezee tofauti ya hesabu yake na ile ya tume. Kosa kubwa la mwaka jana - hasa kwenye kura za urais - ni kuwa vyombo vya habari vilikatazwa kutangaza matokeo ya Urais kwa kadiri walivyoyapata. I believe it was one of the most shameful moment ya uhuru wa habari nchini.

Binafsi nimejiweka sawa hapa kuwa nitatangaza matokeo ya Igunga kwa kadiri yanavyokuja.

1. Kutokana na maelezo yako hapo juu ina maana umekubaliana na hoja kuwa wizi wa kura upo?
2. Kwenye hoja yako hapo juu kipengele b. naomba nikusahihishe kuwa chombo chenye mamlaka kisheria kutangaza matokeo ni NEC kwa maana hiyo uhuru wa vyombo vya habari hautakiwi kuingilia/kukiuka sheria za nchi i.e vyombo vya habari haviko juu ya sheria.
3. Kumbuka wewe huna mamlaka kisheria ya kutangaza matokeo so ukifanya hivyo itakuwa kwa kujifurahisha tu kama alivyofanya Zitto kwenye Uchaguzi B'haramulo
 
Ndugu yangu Kigarama, unapoamua kuwa mkweli siku zote, ujue pia kuna price to pay, yaani kuna Vigharama utaingia. Hivyo unapoikosoa Chadema humu kwenye jf, pia ujiendae kupokea malipo ya ukosoaji huo!.

Niliwahi kuposti hii...

CCM Imechokwa
; CHADEMA Haijajipanga!



Nilichoambulia niliambulia lakini kwa vile huu ndio ukweli wangu, kila unapotimia nitakuwa nakumbushia.


Nimeisoma hiyo thread kama CHADEMA wangeichukulia serious leo Igunga tungeshuhudia chama siyo kundi la watu Maarufu wanaojitahidi kumsaidia mtu aliyegombea kwenye chama chao. watu wengi huwa hatujali kama kwa kuwatumia watu maarufu na siyo mfumo wa chama tunajenga madikteta badala kujenga mifumo mbadala.

Najua kwa hakika kwamba kabla ya RA kujiuzulu Igunga haikuwa kwenye mpango mkakati wa vyama vyote vilivyoko igunga. Si CCM, CUF au CHADEMA ambavyo kwenye ratiba zao za mwaka huu kulikuwa na safari ya igunga kwenda kuimarisha chama kwa kiwango cha Gharama hizi wanazozitumia kwenye uchaguzi huu.

Hata Igunga kwenyewe mikakati ya uchaguzi haipangwi tena na viongozi wa vyama hivyo wa Ngazi ya wilaya bali na "wataalamu' kutoka makao makuu ya vyama hivyo Dar es salaam. Wakati mwingine huwa najiuliza hivi vurumai yote hii ni kwa ajili ya Mbunge wa Igunga au ni kwa sababu ya hadhi ya hawa kina Mbowe na kikwete.

Si CCM wala CDM ambao kwa sasa wanaonekana kuukimbia mtego wa kuamini kuwa kazi pekee ya siasa ni kushinda uchaguzi. Nimempenda sana Makongoro Nyerere ambaye amesema wazi kwamba uchaguzi wa Igunga ni kazi ya uongozi wa CCM ngazi ya Mkoa na Wilaya.
 
Kwa kweli, matokeo yanavyozidi kuonesha sasa hivi ndivyo ambavyo nilikuwa nadhania. Wapigaji kura wamekuwa wachache sana na kama nilivyosema hiyo itainufaisha CCM zaidi. Na kwa sababu suala la matokeo litaamuliwa kwa namba naamini hakuna atakayepata kura zaidi ya asilimia 50. CCM so far wana edge.
 
CUF:

1. Uchaguzi huu pia una maana kubwa sana kwa chama cha CUF kwani mgombea wao akipata say chini ya 10% of the votes ndiyo kitakuwa kimepoteza relevance machoni pa watanzania.

2. Habari ya ndoa ya CUF na CCM imeonekana kuresonate vizuri sana huko Igunga, na hii ndiyo hasa sababu ya CUF ku-retract kuishambulia CHADEMA kama walivyoonekana mwanzo. Wapiga kampeni wa CUF wakiiandama CHADEMA hata logically inaonekana aah! si ni CCM B hao.

3. Habari kwamba huku ni kwao Lipumba na CUF kuwa na influence mkoa wa Tabora inatakiwa ithibitishwe na uchaguzi huu otherwise watajikuta wanaingia ile ligi ya akina TLP, DP, UDP etc.

Naona nilichokisema mwanznoni kuhusu CUF kinatimia, Prof. Lipumba sijui ataficha wapi uso wake!!!!!! Annywayz ndiyo siasa lakini..., CUF ndiyo imeenda hivyo ligi yao sasa ni ile ya akina TLP, DP, UPDP, SAU etc.
 
Back
Top Bottom