Chamoto
JF-Expert Member
- Dec 7, 2007
- 8,339
- 17,586
Namkumbuka Rais Mwinyi kwa mengi, moja wapo ni pale alipoanzisha kipindi chake cha kiswahili RTD (Radio Tanzania Dar es salaam). Moja ya somo alilofundisha lilihusu tarakimu. Alisema, "katika tarakimu za kiswahili, kuna baadhi zina maneno yenye asili ya kibantu na nyingine kiarabu.
Tofauti na zile za asili ya kiarabu, zile za kibantu huwa zinaweza kutamkwa kwa uwingi". Mfano 1,2,3,4,5,8 ni tarakimu za kibantu, hivyo tunaweza sema watu wawili, watatu nakadhalika lakini hatuwezi kusema watu wasita au watisa, kwasabau hayo ni maneno yenye asili ya kiarabu".
RIP Rais Mwinyi.