Ninavyomkumbuka Rais Ali Hassan Mwinyi (1925 - 2024)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
NINAVYOMKUMBUKA RAIS ALI HASSAN MWINYI (1925 - 2024)

Toleo hili la March 1993 linalomwonyesha Rais Mwinyi yuko kwenye meli inayopigwa mabomu ilikuwa ni ''lead story'' yangu katika jarida la Africa Events likichapwa London.

Sababu ya mimi kuandika makala hayo ni Ahmed Saleh Yahya wakati huo akiwa mhariri wa Africa Events alikuja Dar es Salaam na tukawa na mazungumzo kuhusu matatizo aliyokuwa anapata Rais Mwinyi kutoka vyombo vya habari vya Tanzania.

Ahmed Saleh akishangaa inawezekanaje Rais Mwinyi akashambuliwa hata na magazeti ya chama chake yeye akiwa Mwenyekiti na na kushambuliwa na gazeti la serikali yeye akiwa ndiye Rais wa nchi?

Rais Mwinyi akishambuliwa sana na magazeti.

Sidhani kama atapata kutokea rais aliyetaabishwa na magazeti kumshinda yeye.

Ahmed Yahya akaja Dar es Salaam kutoka London akaniuliza hii iinawezekana vipi?

Mimi nikamueleza kwa nini inakuwa hivyo.

Siasa za Tanzani ni za aina yake kwa watu fulani na kwa viongozi makhsusi.

Hapo tuko katika hoteli moja maarufu inaitwa Chef Pride iko Chagga Street na ndiyo ilikuwa kijiwe changu nikija Dar es Salaam kutoka Tanga nilipokuwa nafanya kazi.

Basi niko hapo na Sheikh Ahmed tunashusha chai kababu na sambusa tunazungumza siasa za Tanzania na ukatili wa wahariri dhidi ya Rais Mwinyi.

Ahmed Yahya aliponipigia simu kuniambia kuwa yuko mjini na ananiomba tunywe chai pamoja nikajua lipo jambo.

Waamerika wana msemo, ''There is no free lunch in America.''

Ukiona mtu kakualika anakununulia chakula jua utalipa kwa njia nyingine.

Nasema haya kunogesha barza.

Nimekula sana biriani za marehemu Ahmed Yahya London bure na hakunituma kazi.

Sheikh Ahmed akaniomba niandike makala moja kama njia ya kumsaidia mzee wetu.

Ndiyo nikaandika hiyo makala na wakati huo Africa Events walikuwa wameacha kuchapa makala zangu kwa muda mrefu.

Makala hii walichapa kama makala ya ''Special Correspondent.''

Hiki ni kisa kingine Insha Allah iko siku ikipatikana fursa nitakieleza.

Kilichonifurahisha mimi katika toleo hili ni hiyo, ''caricuture'' yaani kibonzo cha Rais Mwinyi yuko juu ya chombo kinataka kuzama baada ya kupigwa bomu na kushika moto.

1709245710774.jpeg
 
Najaribu kukuelewa unapoelekea mzee wetu, je, imeishia hapa au story inaendelea? Kusema ukweli mzee mwinyi aliongoza nchi kwa misukosuko mingi sana
 
Kuna siku utasema mutume Muhamad pia alinyanyswa na wakristu
Muislamu ndugu yake ni muislamu kwa mujibu wa Quran imefundisha kuwachukia wasio waislamu ila wao kutwa kulalamika wakati kwenye Quran zipo hizo aya
 
Back
Top Bottom