Kumbe ninaishi na mwizi

Kumbe ninaishi na mwizi

smartass

Member
Joined
Jun 12, 2014
Posts
32
Reaction score
5
Habari wana jf
mimi ni mgeni humu najitokeza leo kuomba ushauri
nilipata mpenzi takriban miezi mitatu iliopita katika mtandao maarufu sana unaokutanisha wake kwa waume wanaohitaji marafiki na wapenzi.

mwanaume huyo ni mtu wa africa magharibi
1. kila nikimuuliza shughuli anazofanya hapa dar es salaam hataki kusema (ni msiri sana)
2.hulala kutwa nzima jioni ndio hutoka kuelekea kusikojulikana.(hata vocha ikiisha hatoki kununua dukani mpaka niwepo ndio nikamnunulie).
3.nimeskia tetesi kwamba ni mwizi wa njia ya mtandao na anatafutwa. Ni mstaarabu mpole huduma zote anatoa kama tumefunga ndoa vile. hizi habari nilizopata ndio nashindwa kuamini kipi niache kipi, sitaki kua negative.

akili yangu haipo sawa hizi habari zimenipa hofu kiasi ambacho nashindwa cha kufanya.
naomba ushauri bila kebehi /kashfa
 
Mpwa wangu, hii nchi ni yetu sote, wakiathirika kwa kuibiwa ndugu zako unajiskiaje? Please achana nae atakuingiza matatizoni bure kwenye nchi yako halali. Do you think unaweza kwenda na kufanya haya kwao? suala la kupewa huduma zote ni ujinga sana, simama nenda katafute riziki yako mwenyewe, unapewa huduma kwa pesa za wizi? What is huduma? kwanini wewe usimpe hio huhuma? Usipende vya bure bhana
 
Binadamu asiyetoka nje, duh! Huyo si msafi, hakufai!
 
nyie nao... mnapishana kila siku na wagogo njian mnawaacha mnatafuta kwenye mitandao!!! ukipenda boga penda na ua lake
 
Jaribu kuchunguza simu zake na mawasiliano yake kwa ukaribu,
 
hiyo id yako inamekaa kimagumashi ndg.,.nikiivunja vunja napata "smart+ASS".embu toà kauli!!
 
1.Mwizi kwa njia ya mtandao!
2:Anashinda Amelala!

Ulishawahi kumuuliza usiku akitoka hua anaenda wapi?

Hayo kwanza ndo ntakushauri.

Alafu ID yako duuu labda mii ndo nimeilewa vibaya.
Smart -ass
 
Kama humpendi ila unafurahia huduma tu nakushauri achana nae

but if unampenda na huwezi kujua anafanya kazi gani ni bora uachane nae unless akupe ukweli nini anafanya!
 
Pamoja na kuwepo uwezekano wa kuwa mwizi, si ajabu anaishi nchini kiharamu. Katoe taarifa polisi haraka.
 
Habari wana jf
mimi ni mgeni humu najitokeza leo kuomba ushauri
nilipata mpenzi takriban miezi mitatu iliopita katika mtandao maarufu sana unaokutanisha wake kwa waume wanaohitaji marafiki na wapenzi.

mwanaume huyo ni mtu wa africa magharibi
1. kila nikimuuliza shughuli anazofanya hapa dar es salaam hataki kusema (ni msiri sana)
2.hulala kutwa nzima jioni ndio hutoka kuelekea kusikojulikana.(hata vocha ikiisha hatoki kununua dukani mpaka niwepo ndio nikamnunulie).
3.nimeskia tetesi kwamba ni mwizi wa njia ya mtandao na anatafutwa. Ni mstaarabu mpole huduma zote anatoa kama tumefunga ndoa vile. hizi habari nilizopata ndio nashindwa kuamini kipi niache kipi, sitaki kua negative.

akili yangu haipo sawa hizi habari zimenipa hofu kiasi ambacho nashindwa cha kufanya.
naomba ushauri bila kebehi /kashfa

Mbona tunaishi na nyie na mnatupiga mizinga na hatuwaiti majambazi?!
 
smartass (matak0 majanja?), kwani unaishi naye kwako au hotel alikopanga? wewe aliyekwambia kwamba ni mwizi wa mtandaoni ni nani na alijuaje? kwa hiyo hiyo mitandao anavyotoka jioni ndiyo anaenda kuivunja au? kama ni raiya wa kigeni most likey anaishi nchini kiharamu, na kama anafanya shughuli zisizo halali basi most likely ni dawa za kulevya, mwizi wa mtandaoni ni ngumu kujua kama anatafutwa mara nyingi anajikuta amekamatwa tu! kama anaishi kwako ni hatari sana maana unatunza mgeni asiye nchini kisheria unavunja sheria na una kesi ya kujibu, utafungwa! kama anaishi hotel na wewe umeona umejipatia ondoka faster rudi kwenu/kwako, utajikuta jela!
 
zimeandikwa kilugha cha kwao na anafuta incoming na outgoing calls/msgs
 
Back
Top Bottom