Kumbe kulazimisha kupitisha Sheria ya Kinga ya Kushtakiwa kwa Spika wa Bunge na Jaji Mkuu, sababu zake zilikuwa hizi?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Kwenye nchi yoyote duniani, inayoweza kusema inaendesha utawala bora, ni lazima iruhusu mfumo wa mihimili 3 mikuu ya nchi, ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama kujiendesha katika kutoingiliana katika uendeshaji wa shughuli zao, katika kile kinachoitwa "checks and balance"

Hali ni tofauti kubwa kwa hapa nchini, ambapo Mhimili wa Serikali, mkuu wake ambaye ni Rais, aliwahi nukuliwa akisema kuwa mhimili wake ndiyo uliojichimbia zaidi chini na kuifanya hiyo mihimili mingine miwili ya Bunge na Mahakama, kuwa si lolote wala chochote!

Nimekuwa nikijiuliza hivi kulikuwa na mantiki gani ya kupeleka muswada wa kuweka kinga ya kushitakiwa kwa wakuu wa hiyo mihimili miwlii. ikiwa wao ni watumishi wa Umma, ambao wanasitahili kuwajibika pale wanapokosea?

Jibu la swali hilo nimelipata baada ya kufuatilia mienendo ya hiyo mihimili miwili katika siku za karibuni.

Nianze na Bunge letu. Hivi hiki kiburi cha Spika wetu, Job Ndugai cha kuyapinga hadharani maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA kuhusu kuwavua uanachama wa chama chao angeyapata wapi kama siyo hiyo kinga aliyopata ya kushitakiwa na mahakama yoyote hapa nchini?

Hivi inakuwaje Spika wa Bunge Job Ndugai ayakatae hadharani maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya chama kinachotambulika kihalali cha Chadema ya kuwavua uanachama kwa wale wabunge 19, ambao waliamua kujipeleka wenyewe kuapishwa, bila kufuata utaratibu wa kupitishwa na chama chao cha Chadema?

Hivi huyu Ndugai anataka kuuambia Umma wa watanzania kuwa ameamua kuisigina kwa makusudi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 71(1)(e) ambayo inaeleza wazi kuwa mbunge yeyote anapovuliwa uanachama wake na chama kilichomdhamini ubunge wake "automatically" na ubunge wake unakoma?

Mfano wa pili ni kwa huyu DPP wetu, Biswalo Mganga, ambaye naye ameamua kuisigina Katiba yetu ya nchi kwa kumtoa mahabusu, Nusrat Hanje, usiku wa tarehe 23/11/2020, tena bila "release order" yake kuidhinishwa na Hakimu aliyehusika na kumpeleka ndani mtuhumiwa huyo, kwa lengo moja tu la "kumwahisha" ili akale kiapo cha kuwa Mheshimiwa Mbunge kesho yake ya tarehe 24/11/2020?

Tulitegemea Mkuu wa Mhimili huo wa Mahakama ambaye ni Jaji Mkuu, ajitokeze hadharani na kukemea vikali kitendo hicho cha kuidhalilisha mahakama yake, lakini "ububu" wa Jaji Mkuu huyo ndiyo ninaoweza kuusema kuwa mhimili wake umewekwa "mfukoni" na mhimili wa serikali!

Kwa mifano hiyo miwili inatosha kuuthibitishia Umma wa watanzania kuwa muswada ule wa kuwawekea kinga ya kushitakiwa, uliopelekwa "chap chap" na utawala huu wa serikali ya awamu ya tano, mwaka huu kabla ya kulivunja Bunge, ulikuwa na lengo la kuwafanya hao wakuu wa mihimili hiyo miwili "waisalimishe" kwa mhimili mmoja ambao umejichimbia zaidi chini, mhimili wa serikali.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Hata hiki kiburi alichoonyesha Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali, Biswalo Mganga, kuwa.anaweza kuwafungulia mashtaka kina Mbowe, eti kwa kuuongezea maneno wimbo wa Taifa, wakati wakiuimba pale Mlimani City, kwa kuongezea "ngu ibariki na Chadema" katika kikao chao katikati ya mwaka huu ni kutumia vibaya madaraka yake.

Kwa kuwa yeye amepewa madaraka hayo ya DPP, siyo kujifanya "mungu mtu" bali kuwatumikia kwa usawa wananchi wake.

Kama kweli yeye ni DPP anayetekeleza majukumu yake kwa weledi, ni kwanini hamkamati Spika wa Bunge, Job Ndugai na kumsweka ndani, ambaye amedhihirika kuwa ameisigina waziwazi Katiba ya nchi ibara ya 71(1)(e) kwa kuamua kuipinga hadharani?
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,149
2,000
Hii Kali kweli kweli yaani umeanza kutoa (kuandika) Uzi Wewe na hapo hapo ukaanza tena Kuuchangia Wewe huyo huyo. Kazi ipo hakyanani duh!
 

Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,974
2,000
Hawa ni majangili wanaojua kuwa wanafanya uhalifu hivyo kujiwekea kinga hapo baadae watakapotakiwa kuwajibika. Ndugai ni mwizi, kama mnakumbuka alikula pesa nyingi bila taratibu pale alipokwenda kutibiwa maradhi yake kule India na ushahidi ukatolewa na Controller na Auditor General kwenye report yake; lakini kwa kushirikiana na muhalifu mwenzie JIWE wakamuondoa CAG bila kufuata sheria.

Kama spika wa Bunge Ndugai huapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi yetu lakini inaonesha kuwa hata hiyo katiba yenyewe aliyoapa kuilinda ama haielewi au anaidharaau; mfano mmoja ni pale anaposema atawalinda kuwa wabunge wale waliofukuzwa uanachama na vyama vyao [ Sio hawa Covid`19 bali hata Mwambe alipofukuzwa na Chadema}.

Katiba yetu inasema wazi bunge letu litakuwa na wabunge wa aina gani; hatuna wabunge wa kujitegeme , wote wanatokana na kuwa wanachama wa yama vya siasa. Sasa ujasiri wakuwatetea wabunge wasiokuwa na vyama anautoa wapi? Huyu mgogo nadhani maradhi yamempanda kichwani hajui alisemalo!!!
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Hawa ni majangili wanaojua kuwa wanafanya uhalifu hivyo kujiwekea kinga hapo baadae watakapotakiwa kuwajibika. Ndugai ni moisi, kama mnakumbuka alikuwa pesa nyingi bila taratibu pale alipokwenda kuitbiwa maradhi yake kule India na ushahidi ukatolewa na Controller na Auditor general kwenye repor yake; lakini kwa kushirikiana na muhalifu mwenzie JIWE wakamuondoa CAG bila kufuata sheria...
Kama Taifa hatujawahi kuwa na Spika wa ajabu wa aina ya Spika Ndugai, tokea enzi ya Bunge la Chama kimoja, enzi za Mwalimu Nyerere
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Hivi DPP unakubalije huu udhalimu unaofanywa na Jeshi la Polisi za kuwabambikia kesi watu wote wanaotoa mawazo mbadala ya kupinga baadhi ya mambo yanayotekelezwa na utawala huu wa awamu ya tano na kuwafanya wananchi hao wasote rumande kwa siku nyingi?

Inaonyesha wazi kuwa na wewe ni "syndicate" wa hao wanaowaonea hawa wananchi ambao wanatumia haki yao ya kidemokrasia, ndani ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 18(1)
 

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
820
1,000
Salary Slip
Inaweza isiwe kesho, lakini ni lazima hata katika kipindi cha miaka 10 ijayo watajibu tu makosa yao ya jinai waliyoyafanya wakati wakiwa madarakani
Makosa ya matumizi mabaya ya ofisi, madaraka au kuvunja katiba huwa hayachachi.
Ndio maana Waziri Yona na Mramba walifungwa jela baada ya kutoka madarakani.
Wafuatao jela ni suala la muda tuu, labda waamue kufa muda ukifika;
Ndugai
Biswalo
Sirro
Mwigulu Nchemba
Mahera wa NEC
Mabeyo
Mambosasa
Katibu wa Bunge
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom