Kumbe kulazimisha kupitisha Sheria ya Kinga ya Kushtakiwa kwa Spika wa Bunge na Jaji Mkuu, sababu zake zilikuwa hizi?

Hii Kali kweli kweli yaani umeanza kutoa ( kuandika ) Uzi Wewe na hapo hapo ukaanza tena Kuuchangia Wewe huyo huyo. Kazi ipo hakyanani duh!
nani kakupa haki ya kupanga namna ambayo uzi huu unatakiwa uwe
Toa sura ya beberu kwa avatar yako kisha uendelee kusifu na kuabudu usim crash mtoa mada sie tumemwelewa sana
 
Hebu twende kwenye nchi jirani ya Kenya tu, tuone kama yule Jaji wao Mkuu Profesa Malaga, kama anaweza kukubali mhimili wake wa mahakama uchezewe kama unavyochezewa hapa kwetu?

Mara ngapi mmeona Profesa Maraga akimkemea waziwazi Rais Uhuru Kenyatta kutokana na kutaka kuuchezea mhimili wake wa Mahakama?

Hebu tujaribu ku-imagine hilo jambo linawezekana hapa TZ yetu?
 
Nadhan itakuwa mwisho wa dunia,kinachoshangaza zamani kulikuwa na viongozi wenye uthubutu wa kunena ukwel lkn leo wap!!wte wametumbukia ktk kusifu na kuabudu ili kulinda ugali wao
Hebu twende kwenye nchi jirani ya Kenya tu, tuone kama yule Jaji wao Mkuu Profesa Malaga, kama anaweza kukubali mhimili wake wa mahakama uchezewe kama unavyochezewa hapa kwetu?

Mara ngapi mmeona Profesa Maraga akimkemea waziwazi Rais Uhuru Kenyatta kutokana na kutaka kuuchezea mhimili wake wa Mahakama?

Hebu tujaribu ku-imagine hilo jambo linawezekana hapa TZ yetu?
 
Tatizo huwa mkiweka mbele ukada na ukamanda huwa mnajitoa ufahamu na kujivika makengeza msione uhalisia...

Sikujuwa kama unaweza kuandika huu upotolo. Inajulikana kwamba serikali inatafuta trillon 2 za wafadhiri ambazo hazipatikani bila baadhi ya kamati za bunge kuwa na wenyeviti wa upinzani. Hiyo ndiyo shida kubwa.

Kwanza unasema kila mtu anataka viti maalum, kwani mwaka huu tu ndo kuna viti maalum chadema mbona miaka yote kila mtu anataka na utaratibu ulikuwa unafutwa.

Unasema kwani alitolewa Nusrat peke yake kwahiyo ukikiukwa utaratibu usisemwe kwakuwa ukiukwaji umehusisha watu wengi, hao wengine si walibebwa na huyo aliyetakiwa kwenda kuapishwa haraka.

Hivi ubunge wa viti maalum wa CHADEMA DPP ana maslahi gani hadi ahakikishe watu wanatoka usiku hao aliokuwa anapeleka Certificate wasipewa dhamana kinyume na sheria na kukaa ndani siku 133, hivi unaona ni sawa mtu anawekwa ndani siku zote hizo halafu serikali inasema haina nia ya kuendelea na kesi maana yake alikuwa anaonewa bila kosa lolote.

Mtu ameteuliwa na kuapishwa kulinda katiba na sheria za nchi anafanya madudu kama hayo halafu ati unatetea huo ujinga ni lazima nawewe uwe ni mjinga mwenzao.

Ati unasema Halima Mdee ni smart mtu smart atafukuzwa kwenye chama na kuanza kuhangaika mahakamani ana usmart gani. Unasema ni smart kwa sababu hakutaka kusema nani aliwaruhusu kwenda kuapa hayo si ndiyo alitakiwa akasema kwenye CC. Ameshasaliti chama sasa anatapatapa siku ya kuapa alimshukuru mkiti wa CHADEMA mbona alimkana mchana kweupe na amenywea hana tena hoja.

Ati kama amepewa pesa zingeonekana kwenye account Kwani ni lazima pesa chafu za rushwa ziwekwe kwenye account yake. Anaona watanzania wajinga. Hivi kitu gani anachkipigania ambacho ameshindwa kufanikisha walipokuwa wabunge wengi bungeni hadi wakawa na kambi rasmi ya upinzani, sasa hivi hata kuwa na kambi rasmi hawawezi ni kipi watakifanya kama siyo kupigania njaa.

Ati kushiriki kwrnye chombo cha kutunga sheria, Kwani muda wote anaoshiriki si ndiyo zimepitishwa hizi sheria za za hovyo za kuwawekea kinga watu wawe wanakiuka katiba na kujidai kwa watangulizi wao kuwa sheria zimebadilika, kwakuwa wakisigina katiba hakuna cha kuwafanya.

Hili ya wabunge wa viti maalum wa CHADEMA ni jambo la hovyo halijawahi kutokea inabidi watu wavuliwa madaraka kwa kukiuka viapo vyao wote waliohusika hasa huko NEC, DPP, Magereza na ofisi ya spika. Maana ni mambo ya hovyo ambayo hayatakiwi kuachwa kufanyika katika nchi hii iliyoshiriki kukomboa nchi zingine barani Africa. Watu wawajibishwe tuondokane na hii aibu.
 
Well said mkuu, ubarikiwe sana
Sikujuwa kama unaweza kuandika huu upotolo. Inajulikana kwamba serikali inatafuta trillon 2 za wafadhiri ambazo hazipatikani bila baadhi ya kamati za bunge kuwa na wenyeviti wa upinzani. Hiyo ndiyo shida kubwa...
 
Kwenye nchi yoyote duniani, inayoweza kusema inaendesha utawala bora, ni lazima iruhusu mfumo wa mihimili 3 mikuu ya nchi, ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama kujiendesha katika kutoingiliana katika uendeshaji wa shughuli zao, katika kile kinachoitwa "checks and balance"....
Hatuna utawala wa sheria bali tuko kwenye hali ya vurugu - "anarchy". Hali hii inaashiria machafuko. Tusubiri kuona.
 
Hawa ni majangili wanaojua kuwa wanafanya uhalifu hivyo kujiwekea kinga hapo baadae watakapotakiwa kuwajibika. Ndugai ni mwizi, kama mnakumbuka alikula pesa nyingi bila taratibu pale alipokwenda kutibiwa maradhi yake kule India na ushahidi ukatolewa na Controller na Auditor General kwenye report yake; lakini kwa kushirikiana na muhalifu mwenzie JIWE wakamuondoa CAG bila kufuata sheria...
Haya ni makusudi wala siyo kutoelewa katiba au maradhi aliyenayo.
 
Sikujuwa kama unaweza kuandika huu upotolo. Inajulikana kwamba serikali inatafuta trillon 2 za wafadhiri ambazo hazipatikani bila baadhi ya kamati za bunge kuwa na wenyeviti wa upinzani. Hiyo ndiyo shida kubwa...
Hongera sana.

Umeongea hoja za msingi sana, kiasi ambacho wakiona wale wa "Praise & worship team" watajifanya kama vile hawakuona vile
 
Back
Top Bottom