Kumbe kulazimisha kupitisha Sheria ya Kinga ya Kushtakiwa kwa Spika wa Bunge na Jaji Mkuu, sababu zake zilikuwa hizi?

Hawa ni majangili wanaojua kuwa wanafanya uhalifu hivyo kujiwekea kinga hapo baadae watakapotakiwa kuwajibika. Ndugai ni mwizi, kama mnakumbuka alikula pesa nyingi bila taratibu pale alipokwenda kutibiwa maradhi yake kule India na ushahidi ukatolewa na Controller na Auditor General kwenye report yake; lakini kwa kushirikiana na muhalifu mwenzie JIWE wakamuondoa CAG bila kufuata sheria...
Najiuliza yote haya anayotokea ya kuvunja katiba waziwazi tena hadharani viongozi wetu wastaafu Marais waziri mkuu jaji mkuu wako wapi? Mbona nchi imeachwa iendeshwe kiholela bila kufuata katiba na taratibu? Kwa wale tuliopata kummwona baba wa taifa alivyokuwa akikemea vitendo vya kukiuka katiba tunapata hisia kuwa sasa nchi imekosa mwenyewe.p
 
Wastaafu???hukumbuki walishaambiwa na mfalme waache kuwashwawashwa????
Najiuliza yote haya anayotokea ya kuvunja katiba waziwazi tena hadharani viongozi wetu wastaafu Marais waziri mkuu jaji mkuu wako wapi? Mbona nchi imeachwa iendeshwe kiholela bila kufuata katiba na taratibu? Kwa wale tuliopata kummwona baba wa taifa alivyokuwa akikemea vitendo vya kukiuka katiba tunapata hisia kuwa sasa nchi imekosa mwenyewe.p
 
Kwenye nchi yoyote duniani, inayoweza kusema inaendesha utawala bora, ni lazima iruhusu mfumo wa mihimili 3 mikuu ya nchi, ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama kujiendesha katika kutoingiliana katika uendeshaji wa shughuli zao, katika kile kinachoitwa "checks and balance"...
Tuwekee sheria na vifungu ambavyo vinapinga hawa viongozi kushitakiwa. Tuache kuzua mambo kwa ushabiki tu. Tuwe na ukweli tunapotoa mada.
 
Kwenye nchi yoyote duniani, inayoweza kusema inaendesha utawala bora, ni lazima iruhusu mfumo wa mihimili 3 mikuu ya nchi, ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama kujiendesha katika kutoingiliana katika uendeshaji wa shughuli zao, katika kile kinachoitwa "checks and balance"...

Tatizo huwa mkiweka mbele ukada na ukamanda huwa mnajitoa ufahamu na kujivika makengeza msione uhalisia.

Ipo hivi, na ukweli ndio huo.

Dunia kote mhimili wa serikali ndio mkuu na ndio uliojichimbia zaidi. Zingine ni nadharia tu lakini uhalisia ndio huo. Hata kwenye hizo nchi zilizoendelea hali ipo vile. Ulishawahi kuona bajeti ya IKULU inapita bungeni kama ilivyo kwa bajeti ya mahakama na bunge? Ulishawahi kuona CAG akikagua Ikulu? Ukweli ndio huo aliosema Rais Magufuli na ili hii mihimili miwili ifanye kazi inategemea nguvu na uwezeshaji toka Serikali kifedha, kimiundo mbinu na kiutendaji. Kwa hayo machache tu itoshe kukuonyesha kuwa achana na nadharia ukweli ndio huo kwamba kati ya mihimili hiyo mitatu Serikali ndio yenye nguvu mengine ni nadharia tu. Hakuna cha checks na balance.

Kuhusu kutoshitakiwa kwa wakuu wa mihimili hiyo mitatu ni uamuzi walipitisha wabunge hakuna aliyelazimishwa. Ikiwa CCM walio wengi waliona inafaa wakapitisha hiyo imetoka. Inatokea spika akafanya makosa akiwa kazini bila kukusudia au pengine kwa kukusudia ili kulinda maslahi na usalama wa nchi. Unataka akitoka madarakani ashitakiwe kwa yeye kujitolea kuchukua maamuzi mazito yaliyopelekea kuimarisha usalama wa nchi? Nikupe mfano..... Askari wa Marekani hawezi kushitakiwa popote hata ICC kwa kosa alilolifanya akiwa kwenye operesheni ya kivita nje ya Marekani hata kama ataua na kubaka huko. Hizo ndizo namna siasa za dunia zinavyokwenda na sio nadharia. Inategemea Mazingira, wakati na mahitaji. Hebu askari wa nchi nyingine jaribuni kubaka na kuua bila akili kesho utamwona Bi Besounda wa the Hague anabisha hodi.

Suala la akina Hanje:
Hivi ni Hanje pekee ndio alitoka siku ile? Mbona Twaha Mwaipaya alitoka siku hiyo hiyo na muda uleule na alifutiwa makosa yaleyale lakini haongelewi? Akili amefungwa kwa Hanje pekee? Au ni huo ubunge? Nani kawaambia hakuwa na release order? Ulishaenda gerezani ukaikosa hiyo order? Tatizo mnapojadili kitu ruhusuni bongo zenu zifanye kazi msiruhusu ukhaki au ukijani utawale akili zenu na kujikuta mnaropoka tu bila mpangilio. Ikiwa ni ubunge wa Hanje na wenzake 18 muujadili kwa analysis za kutosha. Mfano, Halima ni kiongozi mkubwa sana Chadema pia kati ya wale 19 kuna wake na wapenzi wa viongozi wa ngazi za juu Chadema.

Imekuwaje wachaguane, wakusanyane hadi wakubaliane kwenda Dodoma kuapa, wawasiliane na Spika kuapishwa, wasafiri kwenda Dodoma kuapa, waapishwe ndipo viongozi wa Chadema wakurupuke kwenda kutoa taarifa vyombo vya habari. Hapa kuna jambo halisemwi, haliko wazi. Pia jinsi mambo yanavyokwenda na maamuzi yanavyofanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba na utratibu wa Chama, hawa wabunge 19 wanaandaliwa mazingira mazuri kuwa wabunge hadi 2025 wakiwa wanachama wa hiari na kupitia Mahakama. Sio CC ya Chadema inayoandaa hayo mazingira bali kuna viongozi wachache wanaoshinikiza maamuzi hayo yafanyike ili kuwapa uhalali wabunge 19 kusalia na ubunge wao kwa namna tofauti. Kumbuka Halima Mdee na wenzake 18 walichokifanya wakati anaongea na waandishi.

Hakutaka kuuharibu huo mchakato hata kidogo na wala kuleta majibizano na CC au uongozi wa Chadema unalijua au usiolijua kwa undani jambo hili. Was very smart!!! Kwa mtu mwenye akili timamu alimwelewa vizuri sana, sio kwamba hajui kuwa Baraza kuu litatupa madai yao. Anajua sana, ila ni lazima mchakato upitie huko kabla ya kuchukua hatua muhimu zaidi. Kwa hiyo suala la Hanje mnalidandia mbele bila kujua nini kilicho nyuma yake.

Hizo nafasi 19 zinatolewa macho na viongozi wote hata aliyeko Ubelgiji na yule aliyekimbilia Kenya nao wanazitaka wana watu wao. Lilikuwa ni suala la kuwahiana nani anapata. Kuna watu wamepigwa na wengine wanafurahia kimoyomoyo wamepata lakini wakija mbele za wanachama wanajidai wakali na kupotosha Henje katolewa usiku bila release order. Kwanini Henje katolewa usiku na sio Twaha Mwaipaya na wengine? Mbona hatuelezwi hao wengine waliotoka?

Turuhusu akili zifanye kazi, tusiruhusu khaki na kijani, au Ufipa na Lumumba vitushikie akili.
 
Najiuliza yote haya anayotokea ya kuvunja katiba waziwazi tena hadharani viongozi wetu wastaafu Marais waziri mkuu jaji mkuu wako wapi? Mbona nchi imeachwa iendeshwe kiholela bila kufuata katiba na taratibu? Kwa wale tuliopata kummwona baba wa taifa alivyokuwa akikemea vitendo vya kukiuka katiba tunapata hisia kuwa sasa nchi imekosa mwenyewe.p
Viongozi wastaafu wanaogopa kuambiwa wanawashwawashwa!
 
Tatizo huwa mkiweka mbele ukada na ukamanda huwa mnajitoa ufahamu na kujivika makengeza msione uhalisia.

Ipo hivi, na ukweli ndio huo...
Nchi imeshatomborojoka hii, haiwezi pona kwa maneno kama ya kwako.

Nilitaka nikujibu hoja zako lakini nikaona nitapoteza muda.

Ukiona viongozi wakubwa wanadharau katiba hadharani na bado wewe unawatetea- matatizo ya ubongo wako ni makubwa sana.
 
Kwenye nchi yoyote duniani, inayoweza kusema inaendesha utawala bora, ni lazima iruhusu mfumo wa mihimili 3 mikuu ya nchi, ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama kujiendesha katika kutoingiliana katika uendeshaji wa shughuli zao, katika kile kinachoitwa "checks and balance"...
Uvunjaji wa katiba hauna kinga hata kwa JPM.
 
Tatizo huwa mkiweka mbele ukada na ukamanda huwa mnajitoa ufahamu na kujivika makengeza msione uhalisia...
Naona umekuja kindaki ndaki ili kulinda na kutetea uvunjifu wa sheria na haki unaofanywa na mamlaka. Mihimili ipo na kila na kila mhimili unatakiwa ufanye kazi kwa mujibu wa katiba ya nchi inavyosema.

Sasa naona umekuja na polojo zako kutetea uovu ukichukua reference za Marekani. Uovu ni uovu tu. Hatuhitaji kufuata maovu ya taifa lolote lile ilikuendeshea nchi yetu. Ila tunachukua yale mema yanayofaa na yenye afya kwa ustawi wa jamii yetu.

Hivyo jitahidi kuwa mkweli unapokuja kuzungumza jambo lolote lile kwa maslahi ya taifa letu. Shida ipo kubwa sana katika mihimili yetu na hasa kukosa heshima mbele ya katiba tuliyojiwekea wenyewe ili ituongoze.

Viongozi wameshindwa kuilinda kwa maslahi yao binafsi.
 
Back
Top Bottom