Nakumbuka huyu dada mcheza filamu zetu za kiswahili Yvonne Cherry a.k.a Monalisa aliulizwa na Salama kwenye kipindi cha Mkasi..inakuwaje yeye Monalisa mkongwe wa filamu hana kitu, wakati waigizaji wapya wanaibuka na wanakuwa na neema kwa muda mfupi.. Monalisa alijibu anaamini kabisa hiyo neema yao haitokani na sanaa, lazima iko namna.. Pia mimi mwenyewe nashangaa hawa wadada wa filamu mbwembwe nyingi..filamu gani ya kitanzania ya kukupa pesa nyingi wakati wanaodurufu hizo kazi pembeni wengi tu. Kwanini wawe wadada tu wenye pesa na sio wakiume? Siamini kama jinsia yao ndio inayo wapatia kipato hicho kingi cha ziada