Kumbe ilikuwa jeuri ya madawa!!

Kumbe ilikuwa jeuri ya madawa!!

Kinachoniuma mimi zaidi ni jinsi Watanzania tunavyopekuliwa kama majambazi sugu pale tunapojulikana kwamba sisi ni Watanzania. Image ya nchi na raia wake kwa kweli imekuwa chafu kupita kiasi. Mtu mpaka unafika mahali unaogopa kujitaja kwamba wewe ni Mtanzania. Laiti JK angekuwa proactive na kuchukua hatua mapema pale alipopewa majina inawezekana hali isingekuwa hivi kwa sasa.

Hope hii vita itafanikiwa ili kuisadia kurudisha heshima ya nchi na watu wake.

Tiba

Yaani! Nimenyanyasika majuzi Addis Ababa kuliko maelezo. Sasa nimeelewa sababu!
 
Kwakweli serikali iliangalie hili kwa umakini, image ya watanzania imeharibika sana kwenye sura ya kimataifa. Tunasumbuliwa sana wabongo kwenye viwanja vya ndege jamani tena mpaka tunadhalilishwa mbele ya kadamnasi, mabegi yetu yanafunguliwa na yanabinuliwa upside down mpaka nguo za ndani zote zinamwaga chini katika check up points za airports.Kwakweli serikali iseme sasa basi.
 
kwahio kwako wewe mtu anaepeleka watoto shule nzuri za gharama ni muuza unga,mtu anaeendesha magari ya kifahari ni muuza unga,mtu anaejenga ghorofa ni muuza unga....acha ku-generalize watu wanaishi vizuri kwa shughuli halali wengi tu....sio lazima wewe ujue mtu anafanya nini kila mtu na maisha yake

Usipaparuke twende taratibu, unaonekana hujauelewa huu uzi. Sijasema wote wanaoishi maisha mazuri na wenye magorofa au utajiri wowote ni wauza unga. Maisha ya utajiri yalikuwepo tangu enzi za Suleiman ambapo hata hao wauza unga hakuna aliyeufikia utajiri wa Suleiman. Soma uelewe. Sihitaji kujua maisha ya mtu.
 
Kwakweli serikali iliangalie hili kwa umakini, image ya watanzania imeharibika sana kwenye sura ya kimataifa. Tunasumbuliwa sana wabongo kwenye viwanja vya ndege jamani tena mpaka tunadhalilishwa mbele ya kadamnasi, mabegi yetu yanafunguliwa na yanabinuliwa upside down mpaka nguo za ndani zote zinamwaga chini katika check up points za airports.Kwakweli serikali iseme sasa basi.

Cha ajabu sijasikia kama Serikali imesema chochote, na watu wanaendelea kudhalilishwa!
 
Mmeamini kuwa hata wasanii waliokufa kiajabu hawakuwa freemason.Ni masembe tu wanayotumwa kubeba wakishindwana kwenye mapato na wakuu wanawamaliza ili wactoe siri. Kwa nini ufreemason uwaibue tu wasanii wa TZ na kuwaua hao hao tu.sembe tu
 
Watanzania wenzangu rudini na kutulia muone jinsi mafisadi wote wanateketea. No stone will be left un turned! Ni garika hakuna hata mmoja atasalia in all aspects za ufisidi!

Vita si vyetu ni vya Bw! Tanzania njema kuzaliwa ni a must is not a choice.

It was over since 2007! Haya ni manifestation tu.
 
Siku nyingi nilikuwa najiuliza hawa Watanzania wenzangu wanapata wapi pesa za kutesa namna hii? Nilikuwa nashangaa nikitoka out usiku nikiwa nimejidundulizia vipesa vya mtoko kwa zaidi ya miezi sita tena kwa kujibana ajabu, cha kushangaza naenda kujionea jinsi watu wanavyojirusha kwa ufahari wa hali ya juu. Matumizi yao ni kufuru, magari waliyopaki nje ya kumbi za starehe ni ya gharama nisiyoweza kuifikiria! Bei ya mavazi waliyovaa ndio usiseme.

Nikifikiria elimu ya watoto wangu, uwiii nachanganyikiwa! mbona wa TZ wenzangu wanapeleka watoto wao kwenye mashule ya gharama ambazo mimi niliziona kama kufuru! mmmh kwani hawa wenzangu wanapata wapi hayo manoti yote? mbona mie siyapati? kama ni mshahara huu huu tena kuna wengine nawazidi mshahara, kama ni bajeti; sidhani kuna anayenifikia kwa kujua kubana matumizi. Kama ni biashara ... mmmh sijaona ya kuwafanya watu wawe hivi... sana sana naona mabutiki yanafunguliwa tuuuuuu na hayana wateja... mashoo room yamesambaaa kila kona sioni wanunuzi, labda biashara ya mabar na glossary naweza sema yanalipa. sasa inakuwaje? Loooh nimeanza kufunguka sasa kumbe wengi wao walikuwa wanashiriki kwa namna moja au nyingine kwenye hii biashara ya DAWA!

Biashara iliyopandisha maisha ya Watz kuwa ya juu na kutengeneza matabaka maana imetufanya wengine tuonekane kama hatujui kutafuta pesa na hatujui mipango... Looo umefika wakati wao wa kuumbuka sasa.... naanza kuona dalili za kukosekana kwa wateja kwenye mabaa na maclub, magari ya kifahari kupungua barabarani, makanisani, masherehe na sehemu mbalimbali za starehe! mmmmmm naendelea kusikilizia majina yanayotajwa huko kwenye ushiriki wa madawa! mboni mambo!! masikio yanaanza kuwasha maana tutasikia hata tusiyoyatarajia.....

WaTz kiboko! hadi mnakodi meli??? du kumbe nchi hii imeshaoza eeeeeeeh! Ona hospitali zinavyojaa waathirika wa madawa, cheki vituoni ujionee mateja yanavyonesa ..... balaa hili.

EEE MUNGU WAUMBUE WOTE NA BIASHARA HII IFE KIFO CHA MENDE, WATOTO WETU WAPONE; AMENI.

hao watanzania wenzako.....
 
pole sana kwa kuchelewa kung'amua
 
Usipaparuke twende taratibu, unaonekana hujauelewa huu uzi. Sijasema wote wanaoishi maisha mazuri na wenye magorofa au utajiri wowote ni wauza unga. Maisha ya utajiri yalikuwepo tangu enzi za Suleiman ambapo hata hao wauza unga hakuna aliyeufikia utajiri wa Suleiman. Soma uelewe. Sihitaji kujua maisha ya mtu.

kwenye uzi wako umesema watanzania wenzako hio tayari ishaweka hata mimi ambae ni mtanzania mwenzako,mishahara yao unaijua,wengine umewazidi[unaonyesha uko concerned hadi kufuatilia mishahara ya watu] na hii unaonyesha wazi unapenda kujua maisha ya watu huwezi kukwepa hilo,kama biashara unasema hujaona za kuwafanya wawe hivyo[unajua wewe vipi] sasa unataka kutuambia unajua biashara za wote wanaoendesha magari,wenye magorofa ya kifahari???usiowajua ndio unawaita wauza unga??
 
Tushukuru mwakyembe kasaidia kuwaumbua watu hawa. Tukipata wengne wa mfano wake I hope wengi wataumbuka.
 
Kwakweli serikali iliangalie hili kwa umakini, image ya watanzania imeharibika sana kwenye sura ya kimataifa. Tunasumbuliwa sana wabongo kwenye viwanja vya ndege jamani tena mpaka tunadhalilishwa mbele ya kadamnasi, mabegi yetu yanafunguliwa na yanabinuliwa upside down mpaka nguo za ndani zote zinamwaga chini katika check up points za airports.Kwakweli serikali iseme sasa basi.

utasubiri sana kiongozi, adui wa serikali ni CHADEMA hayo mengine hayawahusu
 
Hapa ni kweli i wish and we wish things could be that way BUT huu ni upepo unapita. Wataendelea kuuza na wataendelea kutesa mpaka utawala ubadilike. JK hana historia ya kushughulikia masuala nyeti kama haya na ndio maana wakati mwingine huwa tunasema na yeye ni mshiriki. Hayawahi kumwajibisha mtu yeyote kina Jairo wapo wanapeta regardless ushahidi ulioonekana yaani ni balaaaaaaaa.

Tafakari, chukua hatua. Tuache maneno tuamke tutende. Pesa za madawa ya kulevya ni mbaya kuliko chochote unachokijua weyee. Hawa ndo wanaamua nani atawale, kwa muda gani na kumwachia nani. Sii kura tena. JK wa watu mnamwonea bure, akisema kweli hatachukua siku 2 na atawekwa mwingine.
Dawa ni 2015. Kukiondoa tu hiki chama kilichokwisha tangaza kuwa kimechoka. JK hawezi kuwaondoa maboss wake.
 
Nafurahi kuona mmewagundua kuwa ni wauza unga na sio FREEMASON kama muwaitavyo kitaani. maana ilijengeka dhana kwamba kila aliyepata utajiri kwa muda mfupi, basi jibu rahisi ni FREEMASON.

HAKUNA FREEMASON bongo wote ni WAFANYA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA.

Unajua mkuu hata mm nilikuwa naudhika sana watu walipokuwa wanashindwa kutambua uhalisia wa utajiri wa hawa mafisadi wa madawa. Na kuwaita freemasons. Muda wao umefika. Mungu endelea kuonyesha ukuu wako.
 
Sasa nauona mwisho wa wale wanaoishi kwa nguvu ya upambe kwa Mapedeshee wa Sembe hapa mjini, kwa kuanzia natarajia kuona bendi nyingi za muziki wa dansi kufa vifo vya ghafla kama vya Ebola, Wakongoman wengi waliojaza kuimba na kusifia watu ili waishi kukimbia mji, shule nyingi kukosa wanafunzi hasa zile zilizokuwa zinatoza ada ya kufuru kwa kisingizio cha kuitwa ST. Academia....
 
...haya maunga yametuharibia nchi kweli, maana watu hata ada za nursary schools mamilioni, watu wanalipa tu kama mchezo looh...

wanafanya tupandishiwe miada na michango kila mwaka maana mchango tu mtu anatoa milioni 2 mkuu wa shule anaona wazazi wa pesa inauma sana jamani ikifika jan na june hujui mtoto atakuja na barua inayohitaji mchango wa ziada shilingi ngapi mbali na ada ni balaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom