Kumbe ilikuwa jeuri ya madawa!!

Kumbe ilikuwa jeuri ya madawa!!

Ilifikia mahali watoto hawapendi tena shule kisa kuna dili fulani eti mbona fulani hajasoma ila katoka?kumbe ni huu ujinga tu,sasa walau shule itaanza kudefine maisha ukisoma ukafanya kazi poa tuone matunda ya mshahara siyo mtu hana lolote lakini mara mademu mara vipira vikari duh!!.. tena wafe kabisa.
 
Uza na wewe free country

Siwezi nikafanya biashara itakayoniumiza mimi mwenyewe. Utakapouza madawa utafurahia utajiri kwa wakati huuu lakini vipi kuhusu kizazi unachokiharibu? wanao watatumia madawa hayo unayoyauza na utaangamiza maisha yao, utakuwa umejiumiza mwenyewe kwa uroho wa pesa. Hata hizo pesa unazokusanya hazitawasaidia chochote.

Walaaniwe wauza madawa wote maana wanaua kizazi chao wenyewe wakifikiri wanawakomoa wengine.
 
Nilikuwa anauliza hawa wahudhuriaji wa show za bongo fleva ni kula kulala iweje leo msanii aliyepafomu awe bilionea?
 
Ni nai kati yenu ambayo atamwonea wivu ndama aliye nona atakapokuwa anapelekwa machinjioni? Hasha acha watese kwa mimi ni kama ngombe aliyenona anayepelekwa machinjioni
 
Hapa ni kweli i wish and we wish things could be that way BUT huu ni upepo unapita. Wataendelea kuuza na wataendelea kutesa mpaka utawala ubadilike. JK hana historia ya kushughulikia masuala nyeti kama haya na ndio maana wakati mwingine huwa tunasema na yeye ni mshiriki. Hayawahi kumwajibisha mtu yeyote kina Jairo wapo wanapeta regardless ushahidi ulioonekana yaani ni balaaaaaaaa.


Ndio shida ya inji hii! tunaishi kwa upepo.... ukishapita kila kitu kinarudi kama kilivyokuwa. Lakini naamini na ninamuomba Mungu hili lisipite na upepo. Kwa kweli hali ya nchi ni mbaya sana. Hima watanzania tuamke sasa angalau tupipe kelele hadi JK aamke katika hili
 
Kinachoniuma mimi zaidi ni jinsi Watanzania tunavyopekuliwa kama majambazi sugu pale tunapojulikana kwamba sisi ni Watanzania. Image ya nchi na raia wake kwa kweli imekuwa chafu kupita kiasi. Mtu mpaka unafika mahali unaogopa kujitaja kwamba wewe ni Mtanzania. Laiti JK angekuwa proactive na kuchukua hatua mapema pale alipopewa majina inawezekana hali isingekuwa hivi kwa sasa.

Hope hii vita itafanikiwa ili kuisadia kurudisha heshima ya nchi na watu wake.

Tiba

Kweli kabisa! Tunapekuliwa hadi kero! Juzi nimepiya pale FUIMICINO Roma jamaaa wanauliza, A Tanzanian from Dubai? Wakakamata begi langu walimwaga nguo zote wakafungua mpaka zip ya nyuma

Baada ya hapo maswali mpaka mwenyeji wangu kidogo aondoke
 
Na kama hali ikiwa taiti ndani ya miaka 2, hutaona ghorofa zinaota kama uyoga na magari ya kifahali yanapungua barabarani! Maduka makubwa ya kuzuguia yatafungwa na watu waliokuwa wanajiita mapededjee wanafilisika. Naomba Mungu hali iwe taiti zaidi ili rangi halisi za watu zijulikane.

Ha haa haaaaa! kwa hiyo Magufuli hata asiongeze barabara, foleni itaisha automatically.......
 
Siku nyingi nilikuwa najiuliza hawa Watanzania wenzangu wanapata wapi pesa za kutesa namna hii? Nilikuwa nashangaa nikitoka out usiku nikiwa nimejidundulizia vipesa vya mtoko kwa zaidi ya miezi sita tena kwa kujibana ajabu, cha kushangaza naenda kujionea jinsi watu wanavyojirusha kwa ufahari wa hali ya juu. Matumizi yao ni kufuru, magari waliyopaki nje ya kumbi za starehe ni ya gharama nisiyoweza kuifikiria! Bei ya mavazi waliyovaa ndio usiseme.

Nikifikiria elimu ya watoto wangu, uwiii nachanganyikiwa! mbona wa TZ wenzangu wanapeleka watoto wao kwenye mashule ya gharama ambazo mimi niliziona kama kufuru! mmmh kwani hawa wenzangu wanapata wapi hayo manoti yote? mbona mie siyapati? kama ni mshahara huu huu tena kuna wengine nawazidi mshahara, kama ni bajeti; sidhani kuna anayenifikia kwa kujua kubana matumizi. Kama ni biashara ... mmmh sijaona ya kuwafanya watu wawe hivi... sana sana naona mabutiki yanafunguliwa tuuuuuu na hayana wateja... mashoo room yamesambaaa kila kona sioni wanunuzi, labda biashara ya mabar na glossary naweza sema yanalipa. sasa inakuwaje? Loooh nimeanza kufunguka sasa kumbe wengi wao walikuwa wanashiriki kwa namna moja au nyingine kwenye hii biashara ya DAWA!

Biashara iliyopandisha maisha ya Watz kuwa ya juu na kutengeneza matabaka maana imetufanya wengine tuonekane kama hatujui kutafuta pesa na hatujui mipango... Looo umefika wakati wao wa kuumbuka sasa.... naanza kuona dalili za kukosekana kwa wateja kwenye mabaa na maclub, magari ya kifahari kupungua barabarani, makanisani, masherehe na sehemu mbalimbali za starehe! mmmmmm naendelea kusikilizia majina yanayotajwa huko kwenye ushiriki wa madawa! mboni mambo!! masikio yanaanza kuwasha maana tutasikia hata tusiyoyatarajia.....

WaTz kiboko! hadi mnakodi meli??? du kumbe nchi hii imeshaoza eeeeeeeh! Ona hospitali zinavyojaa waathirika wa madawa, cheki vituoni ujionee mateja yanavyonesa ..... balaa hili.

EEE MUNGU WAUMBUE WOTE NA BIASHARA HII IFE KIFO CHA MENDE, WATOTO WETU WAPONE; AMENI.
lakini hapa ni transit tu,ingekua mzigo wote unauziwa hapa ingekua noumer.
 
Lakini sio madawa tu, sekta zingine zote bongo zimeoza kuna rushwa na 'madili' kila mahala, mpaka tutakapoondoa serikali ya kishkaji ndio hali itakuwa sawa, madawa ni sehemu moja tu. Watu wanaiba twiga kwa ndege!
 
Mi natabiri,baada ya muda tutawaona waliokuwa wauza unga wanaanza kuokota chupa za plastiki mitaani.hihihihi...

Waokota makopo watoke wapi wakati baba lao anawakumbatia na hataki kuwaanika!!na wao wanajipanga huko waliko kwa kujianzishia miradi ya kufa m2..yaani mi nachukia miji2 inajulikana af haitajwi!
 
mawazo ya kichawi haya, kwahiyo mtu asijenge gorofa tayari anauza unga?? jenga na wewe lako tukuite muuza unga
 
Nina kanga wangu hapa home anapiga makelele kweli usiku...hivi ni kweli anakaribia kutaga? Mwenye akili ndio atanielewa hapa, kwamba ngoma ikilia sana.....!!!! Basi show inakaribia kwisha!!
 
Kinachoniuma mimi zaidi ni jinsi Watanzania tunavyopekuliwa kama majambazi sugu pale tunapojulikana kwamba sisi ni Watanzania. Image ya nchi na raia wake kwa kweli imekuwa chafu kupita kiasi. Mtu mpaka unafika mahali unaogopa kujitaja kwamba wewe ni Mtanzania. Laiti JK angekuwa proactive na kuchukua hatua mapema pale alipopewa majina inawezekana hali isingekuwa hivi kwa sasa.

Hope hii vita itafanikiwa ili kuisadia kurudisha heshima ya nchi na watu wake.

Tiba

Wapi, hakuna kinachoendelea mbona majina hayatajwi? Wauza unga wanatamba tu. Waliokamatwa ni wapagazi tu. Wenye mali wanapeta!
 
TRA wanafatilia hawa? au wanafatilia watu wanaojitahidi kufanya kazi zao kihalali tu? Hili ni jambo TRA na vyombo vya usalama vinahusika sana
 
Siku nyingi nilikuwa najiuliza hawa Watanzania wenzangu wanapata wapi pesa za kutesa namna hii? Nilikuwa nashangaa nikitoka out usiku nikiwa nimejidundulizia vipesa vya mtoko kwa zaidi ya miezi sita tena kwa kujibana ajabu, cha kushangaza naenda kujionea jinsi watu wanavyojirusha kwa ufahari wa hali ya juu. Matumizi yao ni kufuru, magari waliyopaki nje ya kumbi za starehe ni ya gharama nisiyoweza kuifikiria! Bei ya mavazi waliyovaa ndio usiseme.

Nikifikiria elimu ya watoto wangu, uwiii nachanganyikiwa! mbona wa TZ wenzangu wanapeleka watoto wao kwenye mashule ya gharama ambazo mimi niliziona kama kufuru! mmmh kwani hawa wenzangu wanapata wapi hayo manoti yote? mbona mie siyapati? kama ni mshahara huu huu tena kuna wengine nawazidi mshahara, kama ni bajeti; sidhani kuna anayenifikia kwa kujua kubana matumizi. Kama ni biashara ... mmmh sijaona ya kuwafanya watu wawe hivi... sana sana naona mabutiki yanafunguliwa tuuuuuu na hayana wateja... mashoo room yamesambaaa kila kona sioni wanunuzi, labda biashara ya mabar na glossary naweza sema yanalipa. sasa inakuwaje? Loooh nimeanza kufunguka sasa kumbe wengi wao walikuwa wanashiriki kwa namna moja au nyingine kwenye hii biashara ya DAWA!

Biashara iliyopandisha maisha ya Watz kuwa ya juu na kutengeneza matabaka maana imetufanya wengine tuonekane kama hatujui kutafuta pesa na hatujui mipango... Looo umefika wakati wao wa kuumbuka sasa.... naanza kuona dalili za kukosekana kwa wateja kwenye mabaa na maclub, magari ya kifahari kupungua barabarani, makanisani, masherehe na sehemu mbalimbali za starehe! mmmmmm naendelea kusikilizia majina yanayotajwa huko kwenye ushiriki wa madawa! mboni mambo!! masikio yanaanza kuwasha maana tutasikia hata tusiyoyatarajia.....

WaTz kiboko! hadi mnakodi meli??? du kumbe nchi hii imeshaoza eeeeeeeh! Ona hospitali zinavyojaa waathirika wa madawa, cheki vituoni ujionee mateja yanavyonesa ..... balaa hili.

EEE MUNGU WAUMBUE WOTE NA BIASHARA HII IFE KIFO CHA MENDE, WATOTO WETU WAPONE; AMENI.

kwahio kwako wewe mtu anaepeleka watoto shule nzuri za gharama ni muuza unga,mtu anaeendesha magari ya kifahari ni muuza unga,mtu anaejenga ghorofa ni muuza unga....acha ku-generalize watu wanaishi vizuri kwa shughuli halali wengi tu....sio lazima wewe ujue mtu anafanya nini kila mtu na maisha yake
 
Na kinachoniuma zaidi ni kwamba hatuwezi kuwadhibiti,si unajua tena ukoo wa panya!
 
mawazo ya kichawi haya, kwahiyo mtu asijenge gorofa tayari anauza unga?? jenga na wewe lako tukuite muuza unga

Kweli mzee, kila Gorofa source yake sio unga. Vile vile nchi yenyewe imejaa propaganda, hakuna ajira, viongozi wengi porojo porojo tu. Bungeni ndio usiseme. Acha wauze unga at least wanajenga na kuleta maendeleo nchi mwetu. Kwanza watumiaji wengi wako nchi ya TZ. Italy, china, UK etc. Wanaopata madhara wazungu who cares. Mnaouza uzeni na jengeni magorofa makubwa makubwa at least yanapendezesha nchi yetu.
 
Wote tulipumbazika kabisa na kuanza kuamini story za freemason. Sijui kwa nini watz ni wazito sana kugundua jambo; wauza madawa walijificha chini ya mwavuli wa freemason magazeti ya udaku yakisaidia.

usinikumbushe blog ya masanjamkandamizaji na sign zake za ki-freemason
 
Kweli mzee, kila Gorofa source yake sio unga. Vile vile nchi yenyewe imejaa propaganda, hakuna ajira, viongozi wengi porojo porojo tu. Bungeni ndio usiseme. Acha wauze unga at least wanajenga na kuleta maendeleo nchi mwetu. Kwanza watumiaji wengi wako nchi ya TZ. Italy, china, UK etc. Wanaopata madhara wazungu who cares. Mnaouza uzeni na jengeni magorofa makubwa makubwa at least yanapendezesha nchi yetu.


Mighorofa yenyewe si ndiyo inaporomoka yenyewe na mingine inalaliana,sijui wameshalibomoa au usanii tu unaendelea!kweli hii nchi ni majanga tu kila kona .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom