Kumbe hata Ulaya hakuna Uhuru wa kutoa Maoni, Wanaounga mkono Hamas na kuikosoa Israel wanapigwa rungu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,903
Bila shaka mkoa Pouwa Kabisa.

Nilidhani ni hukuhuku kwetu Mambo ya kupigana rungu la mdomo, kuzibana na kukabana makoo ili Watu wasizungumze labda kuhusu jambo fulani.

Wanaharakati na wapiga domo husemaga nchi yetu na nchi za Afrika hakuna Demokrasia ikiwemo uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.

Lakini kumbe hata Ulaya mambo ya kupigana rungu la mdomo yapo. Vita inayoendelea huko Mashariki ya Kati baina ya Israel na Palestina (Hamas) imezifanya nchi za Ulaya kuichana Demokrasia kwa wale ambao wanaiunga Mkono Palestina (Hamas).

Wanahubiri kile wasichokifanya. Na hiyo ni dalili ya Unafiki. Habari za Karim Benzema na wachezaji wengine walioiunga mkono Hamas (maana yake kuipinga Israel) wamejikuta katika kunyimwa haki zao za kujieleza kama nchi hivyo zinavyojiita nchi za kidemokrasia.

Je, hiyo ndio demokrasia?
Kama wanaruhusu mtu kushabikia au kufanya ushoga kwa nini iwe shida mtu kuwa upande wa Hamas? Kama wao wanashabikia Israel kwa nini wawazuie wanaoshabikia Hamas? Je hiyo ndio demokrasia?

Jioni njema
 
Lakini hizo hadithi sio kila mtu anaziamini.

Fikiria hapa Tanzania waje Watu waseme ati ni nchi yao sijui mungu wao aliwapa, hivi unafikiri tutawachukuliaje?
Wapalestina Wenyewe hilo wanalielewa vizuri ila wanadai Wana sehemu ya Urithi wa Esau

Ikumbukwe Esau alimuoa mtoto wa Ishmael Baada ya kuingizwa mjini na Israel ( Yakobo)
 
Back
Top Bottom