Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Tumemezeshwa kuwa sababu ya kuwa hakuna chanjo ya kirusi cha UKIMWI ni kwa sababu kinabadilikabadilika sana. Lakini tumeona jinsi kirusi cha Korona kinavyobadilika badilika lakini bado wanasayansi wanakaza kuendana nacho, kwa kutengeneza chanjo mpya kila siku. natumaini tutakishinda hiki kirusi cha Korona.
Sasa kumbe hata kirusi cha UKIMWI tungeweza pambana nacho namna hiyo, bahati mbaya ugonjwa huo unaathiri sana maskini na wajinga, hivyo huwezi kuta makampuni tajiri kama Pfizer yanashughulika nao.
Hebu Afrika ambao tunaathiriwa sana na Ngoma tupambane tupate chanjo. Tukiwa na kampeni ya kutengeneza chanjo na kuchanja kila aina ya kirusi cha UKIMWI tunaweza utokomeza ndani ya 20 years.