#COVID19 Elimu kuhusu chanjo... Part 2 – uviko 19 (muendelezo wa uzi wa elimu kuhusu chanjo)

msugupendigwite

Senior Member
Dec 20, 2012
137
26
Kabla ya kuendelea tafadhali piti andika linalohusu chanjo kwa ujumla Elimu ya jumla kuhusu chanjo (yoyote inayotolewa hapa nchini)
UVIKO 19 NI NINI?

Kwa Kiswahili tunaita UVIKO 19, yaani “Ugonjwa wa Virusi vya Korona wa mwaka 2019” ikiwa ni tafsiri sisisi ya maneno “Corona Virus Disease 2019” yaani COVID 19, kwa jina maarufu Korona kama ilivyozoeleka mtaani na kwenye mazungumzo ya kila siku. Ugonjwa huu ulipewa jina hili baada ya mlipuko wa kwanza kutokea mwishoni mwa mwaka 2019 katika jimbo la Wuhan nchini China.

CHANZO

Kama nilivosema mwanzo ugonjwa huu unasababishwa na kirusi cha korona aina ya ‘SARS-CoV-2’ ( SEVERE ACUTE RESPIRATORY SYNDROME CORONA VIRUS TYPE 2). Kirusi huyu anafanana kabisa na yule aliesababisha mlipuko wa Homa ya mapafu huko huko China mwaka 2003 na kuenea miongoni mwa nchi zisizopungua 4. Shirika la afya duniani WHO na mamlaka za Afya na utafiti ulimwenguni kama GOARN walishirikiana na walifanikiwa kudhibiti mlipuko na tafiti ziliendelea kuhusiana na kirusi cha SARS-CoV-2. Tafiti zinaonesha kwamba SARS-CoV-2 anaishi kwa wanyama hasa Popo na wengine wa jamii hiyo. Kitabibu anaitwa “ZOONOTIC”

Mlipuko huu wa UVIKO 19 umepita kwenye hatua/ ‘phase’ nyingi 1, 2, 3 zikiwa na majina tofauti kama Delta n.k…. kwa sasa tuko kwenye wimbi la tatu, na/au Delta la UVIKO 19.

MAAMBUKIZI ‘TRANSMISSION’

Kama nilivoainisha hapo juu kuwa kirusi huyu ni ZOONOTIC na akishafika kwa mwanadamu maambukizi toka kwa mtu mmoja hadi mwingine hupitia majimaji yanayotoka kwenye njia ya Hewa kwa njia ya kuongea, kukohoa, kupiga mwayo,kupiga chafya, kuimba na hata kupumua kwa ukaribu.

DALILI


Hapo mwanzo au hatua za mwanzo za mlipuko wa UVIKO 19 dalili zake zilikua ni homa ( mwili kupata joto ) lya wastani hadi kali zaidi, Dalili za mafua na koo kukereketa, Maumivu ya viungo, Mwili kuchoka na kuishiwa nguvu, Kubanwa kifua na kushindwa kupumua (Dalili ya Mwisho Kabisa), ijapokua baada ya phases mbalimbali dalili zimekua zikibadilikabadilika na kufanana na za magonjwa mengine “non Specific”. Ieleweke kwamba ugonjwa huu unaweza kuumkuta yoyote na asiwe na dalili au awe nazo na ukapona wenyew bila matibabu yoyote, lakin ni hatar zaidi unapowapata watu wenye umri wamiaka 50 na kuendelea, na wenye magonjwa ya muda mrefu kama kisukari, magonjwa ya moyo, na wenye upungufu wa kinga mwili.

KUJIKINGA


Mamlaka za afya za kimataifa na kitaifa zilitoa na zimeendelea kutoa tahadhari na jinsi ya kujikinga na UVIKO 19 ili kukata mnyororo wa maambukizi, njia hizi ni zile zile ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono “sanitizer”, kupunguza msongamano kwa kukaa umbali wa mita 1 kati ya mtu mmoja na mwingine, kuvaa barakoa, kuepuka kujishika midomo, pua na macho, kuvaa barakoa unapokua kwenye msongamano, kujiziba mdomo kwa ‘kiwiko’ unapopiga chafya au kukohoa na KUCHANJWA. (Maandiko mengine yameainisha namna nyingi za kujikinga).

MATIBABU

Magonjwa yanayosababishwa na virusi mengi hayana tiba kamili (si yote, yapo mengine yana tiba), hivyo hata kwa UVIKO 19, Mgonjwa anatibiwa mambo yaliyosababishwa na UVIKO 19 kitaalumu tusema unatibu “complications” kwa mfano mgonjwa amekuja ana shida ya kupumua atapewa huduma ya kwanza atapewa tiba Oksijeni kama iko chini ya kiwango cha 90, ana homa kali atapewa dawa za kushusha homa, atapewa Antibayotiki kuzuia na kutibu “Secondary Bacteria Infections” hadi anapokaa sawa na kuweza kuendelea na matibabu nyumbani. Tangu mlipuko wa mwanzo wa ‘SARS’ wa mwaka 2003 mamlaka za utafiti ziliingia maabara kwa ajili ya tafiti mbalimbali za matibabu na chanjo ya kirusi hiki.

CHANJO MBALIMBALI ZA COVID 19.


Hpa nitazungumzia chanjo kwa makundi yake kama nilivyoziainisha kwenye uzi wa Elimu kuhusu chanjo. Elimu ya jumla kuhusu chanjo (yoyote inayotolewa hapa nchini) lakini nitaanza na chanjo ya Johnson and Johnson iliyoletwa na inaendelea kutolewa nchini kwetu.

JOHNSON & JOHNSON COVID 19 VACCINE
Hii ni chanjo aina ya “Recombinant/Conjugate Vaccines” ( rejea makundi au aina za chanjo kwenye uzi uliopita). Imetengenezwa kwa kutokana na vinasaba ‘genes’ vya kirusi cha korona yaani SARS- CoV-2. Vinasaba vya chanjo hii “Protein Spikes” vikiingia mwilini huchochea mwili kuzalisha kinga ya kupambana na SARS- CoV -2. Kitaalamu wanasema inachochea uzalishaji wa ANTIBODIES. Chanjo hii Inazalishwa na muunganiko wa makampuni 3 yaani JANSSEN VACCINES ya Uholanzi, JANSSEN PHARMACEUTICALS ya ubelgiji na JOHSON & JOHNSON ya Marekani. Chanjo hii inatolewa kwa njia ya Sindano kwenye misuli ya juu ya bega “deltoid muscles”. Ina ufanisi wa 63% na inafanana kimakundi utendaji kazi na chanjo za Oxford- Astra Zeneca ya Uingereza, na Sputnik Covid 19 Vaccine ya Nchini Urusi.

MAUDHI MADOGOMADOGO YATOKANAYO NA CHANJO YA JOHNSON AND JOHNSON

Wataalamu wa chanjo wameainisha maudhi madogo madogo yanayoweza kutokea baada ya kuchanjwa kuwa ni pamoja na maumivu eneo ulilochomwa, uvimbe, wekundu, Mwili kuchoka, Jotoridi la mwili kuongezeka, Maumivu ya misuli n.k (haya sio lazima yatokee)

Ukiona hali tofauti unatakiwa kurudi kituo cha chanjo au kituo cha afya cha karibu……. Hizi ni pamoja na Mzio au allergy baada ya kuchanja, kushndwa kupumua au kubanwa na pumzi.
Pia chanjo hii imeainisha baadhi ya makundi ambayo hayapaswi kupata chanjo hii ni pamoja na wenye mzio au allergy, wagonjwa sana (Hili ni takwa la chanjo yoyote ile) na Wajawazito (*rejea nyingine hazijaainisha hili)

CHANJO NYINGINE ZA UVIKO 19 KWA UFUPI

Pfizer BioNtech Covid 19 vaccine
- hii nayo ni “Recombinant/Conjugate Vaccines” ambayo imetengenezwa na muunganiko wa kampuni 2 Pfizer ya nchini marekani na BioNtech ya nchini ujerumani, Hii ndiyo ilikua chanjo ya kwanza kukubalika na kuanza kutumika nchini Uingereza, Ina ufanisi wa 50% kulingana na tafiti mbalimbali zilizofanywa katika muendelezo wake wa kutolewa.

Moderna Covid 19 Vaccine --- hii nayo ni “Recombinant/Conjugate Vaccines” ambayo imetengenezwa na Kampuni ya Moderna kutoka Marekani pia ina Ufanisi wa 50% kwa mujibu wa CDC na tafiti mbalimbali.
Kiujumla tafiti zinasema zipo chanjo nyingi zimezalishwa na mataifa mbalimbali kwa ajili ya kupambana na UVIKO 19, kulingana na maandiko zipo chanjo 17 ambazo zimezalishwa.... Katika andiko hili nimejaribu kuainisha zile zilizotumika kwa wingi Ulimwenguni na ile ambayo imeletwa nchini kwetu Tanzania.

FAIDA ZA KUCHANJWA UVIKO 19

Kitabibu zipo faida nyingi za kuchanjwa UVIKO 19 kuliko madhara kama inavyoenezwa na kusambazwa vijiweni, Chanjo zimepitia tafiti na majaribio mengi ya kisayansi hivyo zina usalama. Faida iwayo kubwa ya Kuchanjwa ni kwamba.......; Chanjo inakukinga na maambukizi ya UVIKO 19, na endapo utapata maambukizi madhara yanakuwa sio makubwa ya kupata ugonjwa serious hadi kupelekea kifo.

Dhumuni la andiko ni kutoa Elimu kuhusu chanjo na kumfanya msomaji awe na maamuzi ya kuchanjwa au kutochanjwa.


AFYA NI MTAJI............ Karibuni kwa mjadala, Maoni, Marekebisho na pia mlipigie kura andiko hili.
Ahsante kwa muda wako.


REJEA

 
Back
Top Bottom