Ijue sayansi ya chanjo hizi na chimbuko la wasiwasi wake. Hata Ulaya ni 5% tu ndiyo wamechanja katika miezi 3. Je, wanatusubiri sisi?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,942
4,316
Nitajaribu kuieleza sayansi hii kwa njia na lugha nyepesi ili jamii ipate mwanga suala hili ambalo kisayansi ni complex. Lengo ni kuelimishana ili kupunguza mihemuko na mivurugano tunayoishuhudia kwa sasa hasa kwa baadhi ya wanasiasa na viongozi mbali mbali wa kijamii na wenye taaluma ya habari.

Atakayeweza kusoma nakala hii ndefu anakaribishwa.

1. Nitaanza na vinasaba (genes):
Miili ya viumbe hai ina undwa na chembe chembe ndogo sana zinazoitwa seli (cells). Binadamu ana matrillion ya seli. Seli hizi zinafanya kazi mbali mbali za kuwesha kuishi (metabolism). Kila seli ina nukleasi iliyozungukwa na saitoplasm. Kwenye nukleas kuna molecules za Deoxyriboncleic acid - kifupi chake DNA. Kila seli ya binadamu ina DNA zipatazo billion 3 zilizobebwa kwenye mikufu (chromosomes) 46 ndani ya nukleas.

Taarifa zote za jinsi miili yetu inavyojengeka na kufanya kazi inabebwa kwenye hizo DNA. Kazi zote za miili yetu inafanyika kwenye saitoplasm ya seli zetu. Yaani kwenye saitoplasm ndiko kwenye viwanda mbali mbali vya kuiwezesha miili yetu iishi na kufanya kazi zote vizuri.

Kazi zote zinazofanyika kwenye kwenye saitoplasm zinafanyika kwa maelekezo na usimamizi wa DNA. Ili DNA iweze kusimamia kazi inayofanyika kwenye saitoplasm huwa inatengeneza molecule ya Ribonucleic acid - kwa kifupi RNA na kuituma huko kwenye saitoplasm kwenda kusimamia kazi husika. Hivyo inaitwa messenger RNA - kwa ufupi mRNA.

DNA ilivyumbuliwa mwaka 1953. Huu ulikuwa ni uvumbuzi wa siri ya maisha kwani siri zote za uhai na jinsi kila seli ya mwili inavyofanya kazi zimebebwa kwenye DNA. Baada ya sayansi mpya ya uhandisi wa vinasaba (genetical engineering) kuendelea (advance), kwa kipindi cha miaka 13 kuanzia mwaka 1990 hadi 2003 wanasayansi toka sehemu mbali mbali duniani walifanikiwa kuzing'amua (decode) siri zote za DNA zote billion tatu zilizoko kwenye seli za mwili wa binadamu. The entire human genetic code was decoded/ revealed. Ziko kwenye ving'amuzi vya maabara mbali mbali za uhandisi wa vinasaba.

Kuanzia hapo wanasayansi wameendelea kucheza na hizo vinasaba vya DNA ili kuweza kuangamiza baadhi ya magonjwa kwenye seli za binadamu hususani ya saratani kama ya kongosho (pancreas cancer) na ya baadhi ya virusi kama virusi vya Zika vilivyogundulika huko Uganda mwaka 1947 kwenye msitu wa Zita vikienezwa na mbu Aedes.

Pamoja na kuonesha matokeo mazuri sana katika tiba za maradhi haya, hadi sasa kwa kipindi cha mwongo mmoja mamlaka za FDAs zilishindwa kuzipa kibali tafiti hizi kuendelea na phase 2 ya clinical trials za watu wengi zaidi. Wasi wasi ukiwa ni athari ya muda mrefu ambayo inaweza kutokea kwenye vinasaba (DNA) ya seli ya binadamu.

2. Virusi ni vitu gani:
Virusi ni vimifuko ya vipande vidogo sana ya vinasaba (genes). Kuna virusi ambavyo genetic material yake ni DNA tupu na zingine ambazo ni za RNA tupu. Kirusi cha ukimwi ni cha RNA chenye genetic code 9 tu. Kirusi cha coronavirus nacho ni cha RNA na kina genetic codes 56.

Seli ya kirusi haina saitoplasm. Yaani hizo RNA au DNA zake zimehifadhiwa kwenye gamba (envelope) la protein. Kwa coronavirus gamba hili la protein ni la duara lenye miiba midogo midogo mingi (spike protein). Maji ya sabuni (soapy water) huweza kulisambaratisha (denature) gamba hili kwa urahisi na kukiua kirusi hiki. Ndiyo sababu ya kuwashauri watu kunawa mikono yao kwa sabuni mara kwa mara. Pia joto la nyuzi 45 hadi 56 C kwenye mazingira ya unyevunyevu huweza kulisarambaratisha gamba hili. Hii nayo ndiyo sababu ya tafiti mbali mbali duniani ambazo zimeweza kuonesha faida ya steam inhalation therapy ambao kwetu tunaita kujifukuzia.

Kwa kuwa virusi havina saitoplasm ili viweze kuzaliana zinahitaji kuingia kwenye seli za kiumbe kingine chenye saitoplasm. Hivyo zinaingia kwenye seli ya binadamu kwa lengo la kwenda kuzaliana. Kikishaingia kwenye seli ya binadamu genes ya virusi hivi huchukua kamandi ya maelekezo na usimamizi wa viwanda vya saitoplasm. Vinaamurishwa kufanya kazi ya kuzalisha virusi tu. Kazi zingine zinasitishwa. Hivyo seli zizovamiwa na virusi hivi zinageuzwa kuwa viwanda vya kufyatua virusi tu na vikishafyatuliwa vinavyamia seli zingine. Seli za askari wa mwili (immune cells - B lymhocytes, T lymphocytes, macrophages, Killer cells, cd4 cells etc) zinaingia vitani ambayo matokeo yake ni kifo au kupona.

3. Chimbuko la chanjo za SARS-CoV-2
Baada ya mlipuko mkubwa wa SARS (kiswahili chake Changamoto la Upumuaji) wa kirusi cha CoV-2 au coronavirus wa pili huko Wuhen, China mwezi Nov 2019 wahandisi mahiri wa vinasaba waliingia kazini kumchakata huyu kirusi. Hadi March 2020 wakawa wameweza ku decode the entire genetic code ya kiumbe hiki kidogo ambacho hadi wakati huo hakuna aliyekuwa anazijua hapa duniani. Mchina angeweza kukaa na king'amuzi hicho kwa siri peke yake maana ilikuwa ni uvumbuzi mkubwa wa siri ya maisha ya kirusi hiki. Lakini kwa upendo wa kipekee aliamua kuwasambazia bure maabara zote kubwa za genetic engineering ulimwenguni. Maabara hizi zilipokea kwa furaha ving'amuzi hivi na mara moja kuanza kucheza na vinasaba za kirusi hiki ili kupata dawa au chanjo ya kumwangamiza.

Bahati mbaya au nzuri zilijielekeza zaidi kwenye genetic code ya gamba la mdudu huyu - the spike protein genome. Ziliona hapo ndipo rahisi kummaliza mdudu huyu. Clinical trials zikafanyika haraka haraka. Ilikuwa ni fursa kwa tafiti zao za tiba kwa njia ya vinasaba zilizokuwa zimekwamishwa na FDAs zao kwa miaka mingi sasa kupewa ruhusa angalao ya dharura. Hadi kufikia December 2020 zikawa zimepata hiyo emergency approval na kuanza mass vaccination ya watu wote duniani kama phase IV clinical trial.

Cha kushangaza Mchina ambaye ugunduzi wake wa vinasaba ndiyo ulipelekea utengenezaji wa hizo chanjo, yeye chanjo yake haikutumia teknolojia hiyo. Yeye chanjo yake inatumia kirusi chote (the whole virus with its entire structure including the entire genome intact) kilichopunguzwa makali kama ambavyo zilivyo chanjo za magonjwa mengine tulizozizoea.

Chanjo hizi za wengine ni kama ifuatavyo:

- Pfizer na Modern: Hizi saitoplasma ya seli za binadamu inaingiziwa mRNA kuiamuru izalishe magamba (spike proteins) ya virus vya corona. Unapata kinga dhidi ya magamba yake na hivyo hataweza kuingia tena mwilini mwako kama ataendelea kubaki na gamba lile lile. Ndani ya muda mfupi imeonekana kwamba gamba la kirusi hiki ni kama la kinyonga. Hujibadilisha mara kwa mara kutegemea na mazingira. Kwa muda mfupi zaidi ya aina 7 ya magamba haya yamegundulika - kuna South Africa variant, UK variant, Brazil variant, na majuzi Kenya variant na kadhalika.

Chanjo hizi za mRNA ni ngumu kuzitunza kwani zinahitaji ubaridi wa -20 C kwa Moderna na -70 C kwa Pfizer.

- Johnson & Johson, AstraZeneca na Gamaleya (Spunik V from Russia):
Ili kutatua tatizo la uhifadhi, chanjo hizi zinatumia DNA adenoviruses zilizofanyiwa engineering kubeba ndani yake gene ya spike protein ya CoV-2. Tofauti kati yake ni aina za hizo adenovirus zilizotumika kama kibebeo. Ile ya Astra Zeneca inatumia kirusi cha mafua ya sokwe (chimpanzee flue virus). Ile ya Urusi ina viral vector mbili (Ad26 na Ad5). Ile ya J & J ina viral vector Ad26.

- Efficacy ya chanjo hizi kwa matokeo ya phase III clinical trials: Moderna 94%, Pfizer 95%, Gamaleya 91.4%, AstraZeneca 62%, Johnson & Johnson 62%.

4. Coverage ya chanjo huko ughaibuni:
Zoezi la chanjo huko ughaibuni na america lilianza mwanzoni mwa mwezi December 2020. Lilienga kuanza kwa wale waliokwenye hatari zaidi ya kupoteza maisha kwa gonjwa hili ambao ni wanaohudumia wagonjwa hawa mahospitalini, wazee wenye umri zaidi ya miaka 70 na wenye magonjwa hatarishi km kisukari, magonjwa ya moyo au figo au maini, saratani na ukimwi.

Hadi kufikia tarehe 4 March ni wastani wa asilimia 5 tu ndiyo walioweza kuchanjwa ndani ya muda huo wote wa miezi mitatu pamoja na hamasa kubwa iliyofanyika na inayoendelea kufanyika. Sababu kubwa ni wasi wasi walionao wananchi pamoja na baadhi ya wanasayansi wao kuhusu chanjo hizo zinazocheza na vinasaba za genes zao. Bado kuna vitu vingi havijajulikana kisayansi. Kwa mfano unaambiwa hata ukichanja lockdown, kuvaa barakoa na mambo mengine unaendelea nayo kama awali. Yaani hata hiyo efficacy yake hawaiamini.

Halafu wanaona kabisa licha ya kuchanja gonjwa hili badala ya kupungua huko kwao limekuwa likiongezeka. Kwa nini?
Vaccination coverage kwa baadhi ya nchi zao ni kama ifuatavyo:

USA 7.7%, Belgium 7.2%, Italy 7.8%, France 7.1%, Netherland 5.9%, Russia 3.7%, Bulgaria 3.5%, Sweden 8.1%, Germany 8.1%, Spain 8.6%, Portugal 8.8%, Greece 9.5%,

5. Huu upendo kwa nchi za Afrika umetokea wapi?:
Wakati kasi ya coverage ya chanjo kwenye nchi zao zimekuwa za kusuasua, sisi wametuandama tuchanjane haraka. Wametupa au kutuahidi kutupa chanjo bure zinazotosheleza kuchanja watu laki 5 kila nchi ya Afrika. Masharti ya chanjo hizi za bure ni kwamba zichanje watu wenye afya nzuri walio na umri wa miaka 18 hadi 45. Wasiwe na magonjwa mengine ye yote including morbid obesity. Wamediliki hata kutuamuru kuwa watu hawa wawe ni walimu na polisi wetu.

Kwa nini wanataka watu wa aina hii ndiyo tuwachanje wakati watu wa aina hii miili yao iko imara kukabili virusi vya corona kwa asilimia 99.9%?
Kwa mjanja atagundua kuwa wanataka kuwafanyia a phase IV clinical trial watu hawa ambayo matokeo yake yanaweza kuondoa wasi wasi walionao watu wao huko ughaibuni kuhusu hizi chanjo.

Wanatusubiri sisi tuchanjane. Hadi sasa nchi 10 za Afrika zimekubali 'msaada' huu na faster faster zimepelekewa hizo chanjo na wameanza kuchanjana.

Nchi inayokataa au kusuasua kupokea 'msaada' huu inaandamwa kinoma na inachukuliwa kama adui. Sisi hatujaukataa bali tumewaambia watupe muda wa wanasayansi wetu kufanya uchambuzi na utafiti. Loo ona mashinikizo tunayoyapata hadi kutoka kwa watu tunaowaheshimu sana. Tupeni muda kidogo. Uamuzi tutatoa bila kushinikizwa tuzitoe wapi na tumchanje nani.

6. Ushauri wangu: Tuangalie zaidi chanjo ya Sinopharm ambayo imeiwezesha China kuudhibiti vizuri sana ugonjwa huu.
 
- Efficacy ya chanjo hizi kwa matokeo ya phase III clinical trials: Moderna 94%, Pfizer 95%, Gamaleya 91.4%, AstraZeneca 62%, Johnson & Johnson 62%.

6. Ushauri wangu: Tuangalie zaidi chanjo ya Sinopharm ambayo imeiwezesha China kuudhibiti viziri sana ugonjwa huu.
Ugonjwa umetengenezwa na wachina ili wawe super power halafu wewe unasema tukachukue chanjo kwao?
 
Kama uliouandika ndio ukweli basi makenya na manyarwanda yaliyikimbilia kuchanjana yatakua hayana tofauti na manguruwe;halafu mbona hujaweka idadi ya watu waliochanjwa huko Israel maana nasikia Israel iliamua kuwatoa kafara watu wake kwenye hii chanjo
 
Ndugu mleta mada mimi binafsi nimekulewa sana.

kwangu hili ni bandiko bora sana karibu yote yanayo husu hili janga, kwa sababu maelezo yake ni kitaalam sana na hayana usiasa ndani yake.

Ni kama bahati mbaya sana hapa kwetu tumekua na mihemuko ya kisiasa karibu kila jambo na hii imepelekea kujengeka kwa taswira ndani yetu ya kutazama kila kitu kisiasa, hii pia ipo kwa viongozi wetu wakijamii kidini na kisiasa.matokeo yake kila mwanachi tumekua tukitoa maoni na kunzisha mijadala kwa mtazamo wa ki CCM na ki Chadema.

Mimi sidhani mtu kama rais anazungumza kitu asichokua na taarifa nacho kiasi tushindwe kumuamini na kuwa na subira kwanza wakiti wakitafuta nini cha kufanya kilicho sahihi.
 
Umezungumza kiutaalam Sana, shida ni hawa watu wa bavicha. Subiri uone
IMG_20210218_174254_207.jpg


Hiiiiii bagosha!
 
Yote 10, maisha / uhai wako uko mikononi mwako. Tusitafute wa kulaumu au kuhamisha goli.

Huyu wa kwenye red hata kwenye hali hii tuendelee kumpongeza? Labda kama itakuwa unafanya utani jombi.

IMG_20210304_213802_073.jpg


Kwa maisha yanayopotea kutokana na kutokuwajibika kwake mbona ana case ya kujibu?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Huu utopolo wote ni kutaka kuhalalisha sisi kuendelea kufa kwa uzembe wa kutopokea chanjo zilizopo?

IMG_20210218_173848_589.jpg


Chanjo zilizopo zipo vizuri na habari thabiti kukuhusu iliyopo ni hii;



Mtajishaua sana na vi websites mnavyovinukuu nje ya mada. Utakuwa chanjo uko ndani ya wiki za mwanzo mlitegemea 100% ya watu kuwa vaccinated tayari?

Kwamba zingine za hivi pelekeeni wajinga.
 
Huyu wa kwenye red hata kwenye hali hii tuendelee kumpongeza? Labda kama itakuwa unafanya utani jombi.
Nadhani siyo kosa lake. Ni kosa la wanasayansi wetu kuwapatia uelewa wa kisayansi kwa lugha rahisi kuhusiana na kinachoendelea kwenye kupambana na janga kama hili la coronavirus kisayansi. Ninadhani kama atasoma thread hii ataachana na mhemuko huo wa kisiasa.
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom