Kumbe baadhi ya viduka vya iPhone vilivojaa mjini ni center za ku-push madawa na bangi

Heri ya mwaka mpya.

Hii kitu nilishawahi kuambiwa na mtu flani nikapinga, nikasema maybe huyu jamaa ana chuki na wivu na jitihada za vijana wajasirimali.

But baada ya kufikiria zaidi, it made so much sense, but sikuwa na uhakika 100%

Sasa kuna siku nilikuwa nimekaa na washkaji tunapiga story tunabadilishana mawazo, sasa hawa wanangu nawajua ni watumiaji wa bangi, sasa wakataka niwape lift wakachukue mzigo, fresh tukaingia kwenye gari tukaanza safari, sasa tulivofika (sinza) wakanielekeza nipaki mbele ya duka flani ivi la iPhone, washkaji wakatoka wakaingia kwenye hilo duka, mimi nilibaki kwenye gari.

Baada ya dakika 20 wakarudi bhana, nikawauliza "vipi mmepata" jamaa wakanijibu "uhakika kaka" nikajisemea kimoyomoyo "kumbe jamaa alienambia hivi viduka vya iPhone vina push hakukosea".

My take;
Vijana wenzangu tuweni makini, kupendapenda shortcut utaishia kujisaidia kwenye ndoo.
Maxence namuomba huyu jamaa kituoni aje kutoa ushahidi... over.


Punguza mdomo utafia jela.
 
Hivi kwa hali ya Watanzania...haya maduka ya nguo za gharama yalivyo mengi wateja wao ni akina nani?

Nguo Sinza inauzwa laki 3 lkni Kariakoo 80k tu, lkn mule ndani kuna mabinti wakali balaa, huoni kuna kitu kimejificha?
Kuna ya mademu wakali wakali wa jijini wamefunguliwa na mahawara zao, hasa wanaume wenye wake. Yanakuwa kama ni mapambo tu kwani wanatumia ile njia ya asili kujipatia kipato.
 
Biashara sio rahisi kama watu wanavyofirikia haswa hizi za ubishoo ka kuuza nguo , iphone ,watu wanaopiga pesa ni watu wa spares ,nafaka hawa ni rahisi kutoboa.

Hawa wengine unakuta frame kibao wanauza nguo hizo hizo ,nyuma wanapush biashara zao.

Mtu siku akidandiwa mtakuja kuona kaonewa.
 
VI biashara vingi vidogo mjini, huwa, ni front, za, biashara haramu, unakuta mtu kapanga flemu, ya 500K kwa mwezi, kaweka vinguo, vigauni viwili vitatu,ndsni kuna kadada kamelala tu, unajiuliza, hapa faida ipo kweli! Kumbe daaa
Unakuta duka lina visimu viwili vitatu, wameegesha makava ya simu kadhaa alaf nje kapaki BMW!! SIO KWELI!!
 
Back
Top Bottom