Mwongozo: Madini ya Ruby na soko lake nchini Msumbiji

Felix

JF-Expert Member
Mar 9, 2014
876
762
Wakuu, poleni na Majukumu

Wiki kama mbili hivi nilichangia hoja ya mtu aliyeomba ushauri kuusu kwenda msumbiji kufanya biashara ya madini. Baada ya apo nilipata PM nyingi za watu wakiomba niwape ramani ya kwenda huko. Kwanza niwaombe msamahaa wote ambao sikuweza kuwajibu kwa wakati na wengine niliwajibu kwa maelezo mafupi. Hii ni kwasabubu mimi ni mmachinga tu hivyo muda wangu mdogo wakati mwingine na kuwa sina muda wa kukaa nakutoa maelezo kama mlivyo tarajia. Nisameheni tu.

Kiujumala mimi siijui sana msumbiji ila kwa kile ninacho jua nitakieleza ili asiye kijua apate kupata msaada kwa kiasi flani. Kwa walio niuliza ramani ya kwenda msumbiji tu, swali hilo kidogo ni gumu kwasbb msumbiji ni kubwa hivyo ni vyema mge sema nnaenda jimbo gani. Msumbiji mpaka sasa ina majimbo 11 na kwa kuwa wengi
mmetaka kujua ramani ya kufika kwenye madini ya ruby, masoko yake n.k. Hivyo nitaelezea kuusu Jimbo la kabdrigado wilaya ya mutopwezi ambako ndiko kuna machimbo makubwa ya rubi kuliko majimbo mengine.Hata hivyo yapo majimbo mengine yenye madini aina ya dhahabu, mawe mengine ila kwa leo wacha tuongelee kuhusu ruby uko mutopwezi.


Katka makala hii, nitaongela Jinsi ya kufika kwa njia ya ndege,basi, na gari binafsi. Usafiri wa meli hauopo na
kwa njia ya ungo sijui. Lakini pia nitaongelea, namna ya kutoa madini msumbiji kupeleka nje na masoko ya ruby kwa ujumla. Pia nitaongelea changamoto unazo weza kukutana nazo uwapo safarini kuelekea msumbiji. Hivyo basi ikiwa wewe ni mmoja wapo ulio nitumia PM au pia na wewe unaitaji kufanya biashara hii na ulikuwa haujui pa kuanzia unaweza kusoma hapo. Kumbuka pamoja na hayo yote utakayo yasoma, anayetoa riziki ni Mungu, na anatoa kwa wakati wake,biashara hii inaitaji uvumilivu, ushapu wa khali ya juu na pia inaitaji kumuomba Mungu sana kwa sababu mambo ya kishirikina ndo kama sehemu yake.Usipokuwa makini unaweza ukaimaliza familia au ukamkosea Mungu kwa kiasi kikubwa.Karibuni.


1.Ukiwa unaenda kwa ndege
Panda ndege kutokea dar mpaka Pemba na-mahanisha pemba ya msumbiji.Ndege ya selikari ya msumbiji inayo kuja dar ni LAM sijajua kama ziko nyingine mimi nimeitumia hiyo tu.
Ukifika pemba ulizia kituo cha mabasi yaendayo mutopwezi, ukisha kuwa ndani ya gari mwambie konda akushushe nanyupu hapo ndipo yalipo machimbo ya madini aina ya rubi na watanzania utawakuta wengi sana, wengine niwachimbaji, mabloka, au wanunuzi wakubwa wapo wote. Kumbuka msumbiji wanaongea kireno. Ukitumia usafiri wa ndege unaweza usikutane na Kiswahili wala kingeleze labda kwa kidogo tu uwapo kwenye ndege au labda kama utakuwa umesafiri na wabongo. Maneno haya ya kireno unaweza kuyatumia kuomba msaada punde ufikapo pemba airport.

1.Msalimie mtu kwanza, kama ni asubui sema –Boa ndia, kama nimchana sema-Boa tarite, kama ni jioni sema Boa noite. Salam za namna hii, na yeye atakujibu kama ulivyo tamka.

2*.Mwambie ninaomba (stoapildir) ----
*unionyeshe (miamoshitra)
*niwapi (e aonde)
*kituo cha dalada chamutopwezi (naparaji di shapa dimutopwezi).
Ukiwa ndani ya gari muombe konda akushushe nanyumpu. apo ndipo machimbo yalipo. Konda unaweza kumwambia hivi

*Kondakta-Kobra dori *shusha nanyupu –Nanyupu paraji au ukasema Saida nanyupu. Kumbuka maneno haya nimeyaandika kwa Kiswahili ili uweze kuyasoma vizuri. Ukitaka kujifunza yana andikwaje kwa kireno , hilo litakuwa somo lingine. Ila yanatamkwa hivyo.

2.Kama unaenda mutopwezi kwa bus
Panda mabasi ya kwenda mtwara, kama utafika mapema unaweza kuchukua daladala mpaka mpakani boda, nauli yake ni shs 5000tshs, kama utafika jioni lala mtwara ulizia guest inayo itwa chilindima kuna watu wengi wanao enda kwenye madini upenda kulala pale na hivyoni rahisi ukapata kampani.

Kesho yake asubuh
daladala zitakuja apo gest panda mpaka mtoni Ruvuma, kumbuka kupitia emigration. Ukishafika mtoni panda mtumbwi au boti nauli yake ni Tshs 5000-1000. kabla ya kupanda boti ulizia kama pantoni,iko kazini na kama inafanya kazi panda pantone nauli yake ni ndogo na ni salama sana nauli yake ni shs 500 .Pantone hii wakati mwingine haifanyi kazi kwa sababu ya maji kupungua

Ukisha vuka utakuwa tayari umefika msumbiji ila bado kufika unako enda. Ukiwa ng'ambo , panda gari za kwenda msimbwa nauli yake ni 350-400 mitikash sawa na shilling helf 16,000-20,000 kulinga na exchange rate. kumbuka kupitia emigration kwa ajili ya passport. Ukifika msibwa kama utakuta gari inaenda mutopwezi panda kama hakuna lala gest, Ulizia kulala guesti ya marehem Yahaya. Guest hii watanzania ulala sana pale na hivyo unaweza kupata kampani lakini pia ni wasafi kiasi, tofauti na zingine. Bei yake ni kati ya 200-250 mitkash sawa na tshs 10,000-15,000 inategemea exchange rate.Mpaka kesho asubuh, panda gari za maning nice zakwenda mutopwezi, ila majuzi serikali ya msumbiji ilikuwa imemfungia leseni kwasbb gari zake ziliongoza kwa ajali. Sijajua kama wamemruhusu. Kama hazipo panda gari za kwenda Nampula shukia mitoro.Ukishuka mitoro utazikuta gari nyingi zinaita mutopwezi ukisha ingia mwambie konda kushukia nanyupu machimboni.



3.Kama unaenda msumbiji kwa gari yako binafsi .
Kama ni kipindi cha nvua pitia mtwara na ukifika mtwara usiku lala,kesho yake nenda mpaka boda nimesema kama ni nvua pita mtwara kwasababu maji yatakuwa mengi na pantone itakuwa inafanya kazi na hivyo itapakia gari yako.

Kama si kipindi cha nvua usipitie mtwara nenda mpaka masasi ukifika masasi nenda mpaka daraja la mtaa mbaa swala lilo jengwa kwaushirikiano wa Tanzania na watu wa msubiji. Ukifika mpakani kumbuka emigration.Kabla hujavuka, kama gari yako ina tinted sana nyeusi toa kwasbb ma-askari wa kule traffic police wanasumbua sana kwa ajili kukulia hela. mimi walinipiga faini ya mitikashi ya 6,000 sawa na laki tatu na zaidi ya Tanzania. hivyo kuwa makini usiweke matinted meusi sana kama tuwekavyo wabongo.

Ukiwa mta mbaa swala unaweza kukuta abiria haswa wabongo ,
wakati mwingine watakuomba kupanda gari yako kwa kulipia nauli au lift.kuwa makini usiwapakie na ukiwapakia jitahidi wale wanye magari ya abiria landkruza,wasikuone kwasbb wanakula pamoja na police na hivyo hautafika mbali utapigwa faini kubwa ya kubeba abiria wakati wewe labda uliwapa lift. Wale jamaa uwapigia police na kusema gari no flan limeiba abiria wetu.kama gari yako ina beba watu wa tano weka hao watano.lakini wale wenye landkruza za abiria wasikuone wana roho mbaya. ile faini utakayo lipa na wao wanapewa kidogo na police.


Ukisha vuka, utatembea kilo meta 5 tu barabara ya lami baadaya hapo utatembea kilometa zaidi 180 pori tupu na njia si lami.
ukiona gari yako inaonyesha kilometa 180 jua utakuwa umefika kwenye centere ya wilaya ya mueda mjini na utakuwa umefika mueda mjini. Mueda ni wilaya iliyoko katika jimbo la kabdrigado ambalo makao makuu yake ni Pemba.

Ukiwa mweda kama utaitaji kula, kuwa makini sana na maeneo ya pale kwa sababu pale kuna kabila la wamakonde sana na wamakua sana, hawa watu hasa wamakonde wa pale ula kono kono na panya na kama utakuwa una nafasi unaweza kwenda sokoni utakutana na kono kono au panya zinauzwa .ila kama wewe ni mlaji pia utakaribishwa sana. Na unaweza kupewa rost ya konokono bila kujua ukafikri pweza!!!
Uki anza safari kutokea pale Muedatembea kilometa 50 tu utafika njia panda panaitwa AWASI. Ukiwa awasi nenda kulia kwako na anza kuhesabu km za gari yako zikikifa 160 na utakuwa umefika kwenye barabara kuu na nzuri iendayo makao makuu ya jimbo la kabdrigo pemba.Ukiwa pale njia panda panaitwa silva makua nenda kushoto kwako.Ukianza safari pale, tembea kilometa 10 tu,utakuwa umefika njia panda nyingine, panaitwa mitoro, njiapanda hii ndo itakuwa ya mwisho kwako, kushoto barabara inaenda nampula mpaka Maputo. Ukiwa mitoro wewe usiende kushoto wala kulia wewe nyosha tu,ukianzia apo mitoro tembea kilometa 60 na gari yako ikikuonyesha zimefika 60 utakuwa umefika nanyumpu kwenye machimbo. Na ukitaka kwenda mutopwezi mjini utaongeza mwendo wa kilometa arobaini kamili.


Usumbufu unao weza kuupata ukiwa safarini
1.Kama utakuwa kwenye ndege, mala nyingi wahudumu uongea kireno na kutafisiri kwakingereza, Kiswahili usitegemee. Pamoja na hayo kuwa makini wanapo ongea kiingereza chao, usipo kuwa makini unaweza kupata huduma usiyo penda mfano ukaletewa chakula usichokiitaji na ukijifanya unaongea kiingeleza wahudum wengine waweza kukusaidia au wengine wakakwambia one moment please, akiondoka kusimama sehemu ndo basi mpaka mnafika harudi . Ndege yao- Lam ni nzuri ila mimi siku moja nikiwa natokea Pemba kwenda thailandi kupitia Kenya. Nakumbuka walitupa chakula kimechacha sijajua ilikuwaje ila na nafikiri wameisha jirekebisha.


2.Ukiwa kwenye basi jitahidi kuwa mvumilivu, kwa abiria atakae kuwa kalibu yako. Wananchi wa msumbiji hasa wa jimbo la kabdrigado,wanapenda sana kula hovyo hovyo, na gari likisimama upenda kula vitu kama miwa,mayai, kuku wa kukaangwa, machungwa, mandazi
n.k hivyo mpaka gari inafika wengine uachia harufu nzito aidha kutoka kinywani au wakati mwingine kwasbb ya mayai utoa harufu kwa kutokea kwingine. Nafikiri umenielewa apa.


Kama utakuwa hauna haraka sana usipande gari yoyote zaidi ya gari iliyo andikwa MICULA. Basi hizi
ni za mkuu mmoja wa zamani ndani ya selikari ya msumbiji. Hivyo mapolice na trafic uziogopa sana na huwa hazisimamishwi. Na ikitokea ikasimamishwa basi trafik p, atakagua kadi ya gari tu ila police wa kaida hawa tawakagua mabegi. Wakati mwingine kwenye mabasi mengine mbali na hiyo, police usumbua sana, wana weza kukukagua mpaka sehemu za siri. Wana vibanda vyao wakikwambia shuka mara moja,ujue una hati hati. Ila lengo lao ua ni kutaka hela tu. Na hii ni kwasbb watanzania wamewazoesha, watanzania hawapendagi zogo sana hivyo police akianza kumkagua wabongo utoa 50-100mitikashi na police uacha. Kama na wewe utaweza, chenji hela zako uwe na 50,50,50, kwa ajili ya kuepuka usumbufu kama huo.

Police wakisimamisha gari mala nyingi uingia ndani kuangalia kama kuna mtu mgeni asiye jua kireno na hivyo utumia mwanya huo kumchukulia hela. Kumbuka police wa msumbiji hata kama anajua Kiswahili au kingeleza,atajificha na kujiongelesha kireno kusudi akuchukue hela. Yafutayo yana weza kuwa maneno ya kukusaidia pale police akiingia kwenye gari na kuwasalimia,akisamilia ua anakuwa makini kuangalia ni nani hajajibu na akikupata anakuomba id au passport ili ajue ni wa wapi. Hivyo akiingia kwenye gari, kama ni hasubui ,mchana au jioni atasalimia hivi,
(a)Boa ndia-Asubuhi, na wewe mjibu Boandia sheefu (Yaani habari za asubuhi, wewe jibu nzuri mkuu)
(b) Boatarite-mchana, na wewe jibu Boatarite sheefu (Yaani habari za mchana, wewe jibu nzuri mkuu)
(c) Boanoite-usiku, wewe jibu Boanoite sheef(……………………………………………………………………………………..)

Ukinyamaza kimia akaona mdomo wako hauja itikia atajua wewe ni mgeni na hivyo atakuomba ID. Ikitokea akakwambia shuka. Atakuuliza unaendawapi? (Vai para aonde? Kama bado uko nyuma nyuma uko msimbwa, usimwambie naenda mutopwezi mwambie naenda pemba au Nampula. Akisema vai para aonde wewe jibu kwa ufupi NAMPULA. Akisema unaenda kufanya nini? (fazero ke? Mwambie kutembelea ndugu yangu, usimwambie naenda kuchimba madini. Akisema vai para fazero ke?Mjibu vizitari meo limao, kama ndugu yako ni mwana ume, kama ni mwana mke jibu tu kwa ufupi , vizitari minya ihirimaa. Mananeo hayo yanatamkwa hivyo kwa kireno ila nimeyaandikwa kwa Kiswahili yakusaidie kuelewa , mjibu askari
kwa kujiamini. Mwishoe atakwambia nipe basi hela ya sonda. (Dala refureshiko) kama utakuwa na 50 wee mpe, nadhani unafahamu msafiri kafiri.

3.Ukiwa unaenda nunua kanda mbili za kuvaa chooni, watu wa msumbiji kwenye gest hawaweki kanda mbili labda zile hotel kubwa. Mimi sijui ua wanaogaje, lakini kwa usalama zaidi nunua kanda mbili zako na taulo.


4.Ukichukua guest, nyingi hazina vyoo vya self,
badala yake mnakua mnachangiana choo chumba moja. Mfano, room yako unaweza kuona ina choo lakini kumbe na mwezio jirani anatumia choo hicho, kwa maana choo chenu kina milango miwili. Atakaye wai kuingia chooni atalock mlango wa mwenzie. Si guest zote ziko hivyo ila nyingi ziko hivyo.


5.Jambo la mwisho katika kero, geust za msumbiji zina bei sana, guest ambayo unaweza kukuta ina choo cha kujitegemea, tv na maji. Gharama yake ita anzia mitikash 1,000 sawa na 50,000 ya Tanzania au zaidi.



BAADA YA KUFIKA MONTOPWEZI.
Kama unataka kununua mawe tafadhari hata kama unayajua , kwanza kuwa mjinga kwanza uone wenzio wanafanyaje, jinsi wanavyo tathimini jiwe, wanavyofanya selection ya caption n.k, pia usipende kuwaonyesha wewe una hela sana.Unaweza kuwaambia una dola 1,000 tu ya kuzungushia. Kuwa makini ukimwi ni mwingi sana pale, matumizi ya hela yako hovyo ovyo, mtu wa mawe kumuonga Malaya dola 200 kwa one night ni kitu cha kawaida, kule dola 100 ni hela ya kawaida tu. Kuwa makini sana ila kama ndo fani yako mmmmmmmm, utakuja kutuomba ushauri hapa jamvini tena.

SOKO LA KUUZIA MAWE AINA YA RUBY

Masoko ni mengi sana hata apa Tanzania ni mengi lakini pia na pale msumbiji kuna watailandi wananunua vizuri pale mutopwezi. Ila soko kuu ambalo ni zuri la ruby duniani niThailand.

JINSI YA KUPELEKA RUBI THAILAND,UKIWA MSUMBIJI
.

Ziko njia nyingi ila mimi nitaongelea ile ambayo naifahamu kwa sabb nimeitumia sana. Ukipata rubi caption ambazo hazina quality sana ila nyingi unaweza kuziuza palepale au kama una order nzuri uko Thailand , unaweza kwenda kwenye makampuni yanayo tuma madini nje, yako Jimbo la nampula mjini. Ukifika utalipia hayo mawe yako caption au mengine mfano tamalin na hivyo wao watayapokea na kuyatuma wewe utapanda ndege na kuyakuta Thailand. Mpaka majuzi walikuwa wanacharg dola 20 kwa kila kilo.. tunaita cheap stone. Kumbuka kwenye ruby inaweza kuuzwa kwa njia ya kilo kama ni makaption yasiyo kuwa na quality sana, ila rubi inauzwa kwa gram, au karet.
Kama hatakuwa na caption bali una jiwe lako zuri na la uhakika na unasoko lake vizuri, tafuta watu uko msumbiji wenye Leseni ya kuexport, watakuandikia vibali kutoka wizara ya madini, mtakubaliana kulipana % flani kabla au baada ya mauzo kutokana na mapatano yenu. Mtu mwenye leseni atakusindikiza mpaka airport na wewe utapanda ndege ukiwa na copy za leseni yake nabarua iliyotoka wizara ya madini inayo onyesha madini yale ni ya aina gani,uzito wake, thamani yake, na final destination yake kuuzwa ni thailand.

Kumbuka ukiwa msumbiji kama wewe hauna kibali cha kuishi uko muda mrefu, Residence permit. Ukienda Maputo kuomba visa ya Thailand hautapewa.Badala yake utatakiwa kwenda ubalozi wa thailandi Kenya kuomba visa. Mimi natumia sana ubalozi wa thailandi nchini Kenya, hivyo sijui kama apa Tanzania upo. Jambo hilo unaweza kuulizia kama upo, lakini pia hata kama upo Tanzania ukiingia na madini na kuwaonyesha yanaenda nchi nyingine, Watu wa TRA wakati mwingine baadhi yao, uleta usumbufu sana. Hivyo mimi hilo ua nalikwepa.

Utapanda ngege kutoka pemba airport-kwenda Kenya airport kwaajili ya kuunganisha ndege nyingine nakuomba visa. Msumbiji hawana ndege inayoenda Thailand kutoka pemba. Nauli ya pemba –kenya haizidi $600 return ticket. Ukifika Kenya airport peleka madiniyako na vibali vyako custom. Watayapokea, na kukupa lisiti. Hivyo wewe utaingia Kenya kuomba visa, bila kuzunguka na mzigo. mara nyingi haizidi siku mbili kupata visa. Baada ya apo utanunua ticketi yakwenda Thailand na ukifika airport tayari kwa kuondoka utapewa madini yako na watu wa custom bila charges yoyote. Ziko ndege nyingi Kenya zinazo endaThailand ila kama wewe mtu wa budget, ni vyema ukatumia Kenya airways, kidogo wana nafuu kuliko ndege zingine.

UFIKAPO THAILAND
Baada ya kufika airport na kumaliza procedures za emigration,peleka jiwe lako custom kwa ajili ya kulilipia ushuru. Ushuru wa Thailand si mkubwa sana. Kumbuka rushwa iko nchi zote duniani, ufikapo custom wape vile vibali hasa ile barua inayo onyesha mzigo wako na thaman yake, then wao watakwanbia ni bhati ngapi unatakiwa kulipia. Katika kukamilisha rushwa zao hao watu, wanaweza kukwambia unatakiwa kulipia bhat 6,000 sawa na Tshs lak 3 au zaidi kidogo kutegemea na exchange rate .Lakini hapo apo wanaweza kukupa option kwamba lipia bhati 2,000 ila watakupa lisiti ya bhati 1,000.Ukikubali watafanya hivyo na ukikataa bado pia watacharge bhat 6,000 na lisiti watakupa. Wakati mwingine kama utakubali watafanya urafiki na wewe na kukupanamba zao na kukwambia kabla hauja panda ndege kutoka Africa nipigie ujue kama niko counta au la!! Sasa mimi hapa siwezi kukushauri ufanye hivyo au la, akili kichwani ila ninakupa mwanga tu.

Faida ya kulipia ushuru custome, ukiwa nchini kwao, utauza jiwe lako bila woga, kwa muda wowote, na wakati wowote.

UFIKAPO MJI MKUU WA THAILAND.

Ukiwa Thailand banckok, utakuwa bado hujafika sokoni.Utatakiwa kuchukua basi 3hrs au demostic flight mpaka kwenda kwenye sehemu moja inayoitwa chantaburi. Sijajua ua ni mkoa au ni wilaya sijui. Unaweza kugoogle uka angalia, Apo chantaburi ndipo lilipo soko la rubi haswaaaa, siku ya ijumaa na jumamosi, ni siku kama ya soko mahalum kama gulio vile la rub. Ni siku za mauzo, matajiri utoka nchi za ulaya,za scandnavia, austrelia na kwingineko kununua ruby pale Chantaburi. Usishangae kuona mtu anauza kajiwe kadogo kama gram 30 hivi anakauza $1,000,000 milioni.Mimi mwenyewe mpaka leo sijawai kupata jibu hawa watu wanao nunuaga mawe hayo kwa bei kubwa uyafanyia nini, sijui.

Kumbuka mawe ya kuuza kwa bei hiyo a sikama jiwe lako ulilotoka nalo msumbiji, mawe hayo uwa tayari yamefanyiwa cutting,na yana
shap. Hivyo waafrica wengi uwauzia matajiri wa Thailand then matajiri hao,uyaongezea thamani kwa kupitishwa kwenye machine zao.


JINSI YA KUUZA JIWE LAKO
.

Uwapo chantaburi kwa mala ya kwanza inaweza ikakuwia vigumu kumjua nani mnunuzi mzuri ila utawaona wathai wengi na maduka yako wakitaka uwauzie vyovyote wakiona muafrica wanajua ana mali. Unaweza kuingia kwenye duka, ofisi yoyote na hii inategemea na jinsi roho yako itakavyo kutuma. Kumbuka pia pale thailandi kuna madalali wengi na wao ni matajiri na wanatambulika kisheria. Ukipenda kuwatumia unaweza kuwatumia ila usimpe mtu jiwe. kama hupendi unaweza kuachana nao. Nakushauri kama utapenda kutumaia dalali kuwamakini sana. Ila kuna faida kubwa sana ya kuwatumia hasa kwa mala ya kwanza mfano.mpaka unafika chantaburi jiwe lako linaweza kuwa na thamani ya $20,000 na wewe malengo yako ukauze angalau 27,000 au mwisho 25,000 dola,

Lakini ukimtumia dalali mzuri usishangae kuona jiwe ulilo fikiria kuliuza dola 27,000 dalali analiuza dola 50,000!! hayo ni mambo ya kawaida kwenye mawe. Ukisha fanyabiashara, bosi atakupa cheque
au unaweza kuongozana nae benk, ikiafanyika transfer kwenda kwenye account yako unaona. Au kama una ka ulimbukeni unaeza kuomba upewe dola zako upande nazo ndege. Akili kichwani. Jitahidi sana yule bosi atakae nunua jiwe lako uchukue contact zake na hivyo kwa mara nyingine na root zingine utakuwa tayari mzoefu.


Ukiwa chantaburi, kuna hotel nyingi sana za kifahari lakini kama hautajari, nakushauri ulale hotel moja inaitwa-ALEX APARTMENTS. Gharama zake ni ndogo chumba kizuri self, air condition, TV, wife cha bei ya chini ni bhati 300 sawa na shs 15,000-17,000 kutegemea na rate. Inamilikiwa na muafrica hotel hiyo. Hotel hii mimi naipenda sana kwasbab michangudoa haizoei sana pale.Na bei ni rahisi sana. Utawakuta sana waafrica haswa kutoka west Africa wengi wana maofisi yao na wao wananunua mawe ya kila aina hasa haya macheap stone.Jitahidi kuwa social sana na watu
ii itakufanya kupata marafiki wengi. Usipende kuwa ambia sana kwamba wewe unajiwe, kwanza nyamaza uku ukisoma mazingira.


Mpaka hapo nahisi ninacho jua nimekupa
kwa upande wa Msumbiji mutopwezi. kila lakheri.

MUNGU AKUBARIKI .
 
Mwenyewe nimevua kofia kwa jinsi somo lilivyokuwa zuri na kuelewka kirahisi sana,hili somo nitalitumia kumsomesha mmoja wa brothers wangu ambaye kajikita ktk biashara za mawe,nitajaribu kufuata maelezo hapo juu ili nione kama ataweza kufanya kama ilivyoelezwa hapo juu na mtaalamu,hapa napenda kuingia na kusoma mtu unaweza ukakutana na kitu kitakochokuletea faida kubwa sana katika maisha yako,hii ni sehemu moja ya maana sana ukiachilia mbali na siasa zetu za vyama vingi.Mwisho napenda kumshukuru sana mkuu kwa hii information isiyokuwa na uchoyo wowote ule.Mbarikiwe wote.M/Mpamba.
 
Felix...maelekezo murua!ila hapo kwenye boatarite...umerudia mara nyingi sahihi ni "Boa Tarde" tamka kwa kukaza R...ama sio?Kiasi nina experience na dhahabu Mozambique,Ruby sijawai kujaribu...ila pia nawashauri wanajamvi....huku pia wapigaji wapo...kwa hiyo umakini kidoogoo...
 
Last edited by a moderator:
Felix...maelekezo murua!ila hapo kwenye boatarite...umerudia mara nyingi sahihi ni "Boa Tarde" tamka kwa kukaza R...ama sio?Kiasi nina experience na dhahabu Mozambique,Ruby sijawai kujaribu...ila pia nawashauri wanajamvi....huku pia wapigaji wapo...kwa hiyo umakini kidoogoo...

upigaji unanzia huko maana kuna watu wana synthetik ruby wanawapa wachimbaji huko hiwe hilo hilo linakwenda hadi kwa mnunuzi wa thailand wenyewe washapigwa sana huko mozambiq na winza.dodoma,nakumbuka hapo mtopwez kuna jamaa alikuwa anaitwa maspana jamaa kwa kupiga watu mazandu(synthetik) hafai kabisa mshen....z sana
 
Last edited by a moderator:
Felix...maelekezo murua!ila hapo kwenye boatarite...umerudia mara nyingi sahihi ni "Boa Tarde" tamka kwa kukaza R...ama sio?Kiasi nina experience na dhahabu Mozambique,Ruby sijawai kujaribu...ila pia nawashauri wanajamvi....huku pia wapigaji wapo...kwa hiyo umakini kidoogoo...

Ahasante kwa kunikosoa, ni lugha za watu hizi, na isitoshe nilikuwa nafuta jinsi ya kuindika kwa Kiswahili ili ujembe umfikie mlengwa. kwa kireno hainip shida kabisa
 
upigaji unanza huko,hapo mtopwez kuna jamaa alikuwa anaitwa maspana jamaa kwa kupiga watu mazandu(synthetik) hafai kabisa mshen....z sana

Na yote tumeleta sisi wenyewe wa TZ,maana kila biashara lazima tuitie ibilisi....wa-Mozambique bado walikuwa hawajafunguka vichwa kiasi hicho...
 
Na yote tumeleta sisi wenyewe wa TZ,maana kila biashara lazima tuitie ibilisi....wa-Mozambique bado walikuwa hawajafunguka vichwa kiasi hicho...
kweli tanzania sisi tunapenda sana kuharibu biashara kuanzia upigaji kingine wengine wanauzia mawe njaa hawana msimamo..tunabakia kulalaliwa tu
 
kweli tanzania sisi tunapenda sana kuharibu biashara kuanzia upigaji kingine wengine wanauzia mawe njaa hawana msimamo..tunabakia kulalaliwa tu

mkuu felix umesema hapo awali kwamba katika biashara hii usipokuwa makini unaweza kuteketeza familia yako, kivipi? Halafu naomba kujua ni kiasi gani cha pesa angalau unatakiwa kuwa nacho kama mtaji, hii ina maana pesa ya kununua mzigo na nauli zote mpaka thailand?
 
Back
Top Bottom