Kumbe baadhi ya viduka vya iPhone vilivojaa mjini ni center za ku-push madawa na bangi

Joyboy

JF-Expert Member
Sep 16, 2023
1,361
3,404
Heri ya mwaka mpya.

Hii kitu nilishawahi kuambiwa na mtu flani nikapinga, nikasema maybe huyu jamaa ana chuki na wivu na jitihada za vijana wajasirimali.

But baada ya kufikiria zaidi, it made so much sense, but sikuwa na uhakika 100%

Sasa kuna siku nilikuwa nimekaa na washkaji tunapiga story tunabadilishana mawazo, sasa hawa wanangu nawajua ni watumiaji wa bangi, sasa wakataka niwape lift wakachukue mzigo, fresh tukaingia kwenye gari tukaanza safari, sasa tulivofika (sinza) wakanielekeza nipaki mbele ya duka flani ivi la iPhone, washkaji wakatoka wakaingia kwenye hilo duka, mimi nilibaki kwenye gari.

Baada ya dakika 20 wakarudi bhana, nikawauliza "vipi mmepata" jamaa wakanijibu "uhakika kaka" nikajisemea kimoyomoyo "kumbe jamaa alienambia hivi viduka vya iPhone vina push hakukosea".

My take;
Vijana wenzangu tuweni makini, kupendapenda shortcut utaishia kujisaidia kwenye ndoo.
 
Mkuu inategemea walengwa, unajua fika watumiaji wengi wa Iphone ni aina gani.
Pili, Iphone shops inaweza kiwa no code zao za mawasiliano au.

Mmiliki wa viduka hivyo ndio mtandao wake
Miaka ya nyuma kabla maduka ya nguo hayajasambaa kila mahali kulikuwa na maduka yenye nguo kali sana. Kila ukiingia watu unaokuta wamekaa kwenye hayo maduka ni masista duu wakali na vijana watanashati. Nadhani ilikuwa ni njia ya kutakatisha fedha tu na huenda walikuwa na biashara nyingine kwenye hayo maduka.
 
Miaka ya nyuma kabla maduka ya nguo hayajasambaa kila mahali kulikuwa na maduka yenye nguo kali sana. Kila ukiingia watu unaokuta wamekaa kwenye hayo maduka ni masista duu wakali na vijana watanashati. Nadhani ilikuwa ni njia ya kutakatisha fedha tu na huenda walikuwa na biashara nyingine kwenye hayo maduka.
Hivi kwa hali ya Watanzania...haya maduka ya nguo za gharama yalivyo mengi wateja wao ni akina nani?

Nguo Sinza inauzwa laki 3 lkni Kariakoo 80k tu, lkn mule ndani kuna mabinti wakali balaa, huoni kuna kitu kimejificha?
 
Back
Top Bottom