Ripoti Maalum: Kutajwa kwa Vyombo vya Usalama na Wengine kwenye Madawa ya Kulevya ni Mtego kwa JK

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,483
40,002
shehena-ya-dawa-za-kulevya-baada-ya-kukamatwa-na-polisi.jpg


Jeshi la Wananchi, Polisi, Uhamiaji na vyombo vingine vya usalama pamoja na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara maarufu nchini wametajwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa kulevya ambayo imeharibu maisha ya maelfu ya vijana na kuvunja vunja familia. Taarifa za kuhusika huku kwa maafisa wa vyombo hivi vya usalama na watu hawa mashuhuri zimekuja baada ya mmoja wa vijana wa Kitanzania aliyekamatwa huko Hong Kong kuandika barua ya kukiri kuhusika kwake na bishara hiyo pamoja na kuwataja watu waliomuingiza na kumwezesha kufanya biashara hiyo.


Barua hiyo ilipostiwa katika mojawapo ya tovuti zinazofuatilia mambo ya madawa ya kulevya na kubandikwa chini ya kichwa cha habari cha "Punda wa Madawa" kwenye mtandao wa waumini wa Kanisa Katoliki ambao umeundwa ili kuunga mkono mabadiliko na mafundisho ya Mtaguso wa Pili wa Vatikano.


"Punda wa Madawa" ni jina linaloelezea watu wale wanaotumiwa na kutumika kusafirisha madawa ya kulevya kutoka kwa wafanyabiashara wa jumla kwenda kwa wafanyabiashara wa reja reja. Watu hawa wanaweza kuwa ndani ya nchi au kati ya nchi na nchi. Mara nyingi – kama jina linavyoashiria – watu hawa ni vyombo tu vya vinara wa madawa wa kulevya na lolote litakalowakuta huwa ni juu yao wenyewe. Hata hivyo, endapo wanafanikiwa kusafirisha ‘mzigo' kutoka pointi moja kwenda nyingine basi huweza kulipwa vizuri na wengine huishi maisha ya kifahari kabisa kutokana na biashara hii.


Kabla ya kwenda kuwataja watu ambao mwandishi anawatuhumu kujihusisha na biashara hii mtunzi wa barua hii anaelezea kwa kirefu jinsi alivyoingia katika mtego wa kujihusisha na biashara hiyo na hatimaye kujikuta akiangukia kwenye mikono mikali ya sheria ya polisi wa Hong Kong, China. Mwandishi anaelezea kwa kirefu kuwa aliingia katika biashara hiyo baada ya shida za maisha kumzidia na kujikuta hana njia ya kupata kipato kingine halali ili kuisaidia familia yake na hivyo kuamua kutumia njia za mkato.


"Pamoja na misukosuko yote hiyo nilivumilia, lakini mtihani mkubwa ni pale kodi ya nyumba ilipoisha na mwenye nyumba akanipa notice ya mwezi mmoja (nihame), au nimpe kodi ya miezi ya 360,000tsh" ameelezea mwandishi huyo ambaye hakuweka jina lake. Mwandishi huyo wa barua anadai kuwa baada ya kujitahidi kutafuta fedha hiyo na kushindwa alijikuta ameomba msaada kwa marafiki zake ambao anawaita ‘wabaya' kwani ni wao ndio walimchukua na kumpeleka kwa bosi wao ambaye alimlipia kodi ya miezi sita na kumpa fedha za ziada za shilingi laki mbili. Tajiri huyo ni mtu anayeishi Magomeni Mwembechai.


Ni hapo ndipo alipoanza kupewa mazoezi ya kumeza vidonge vya heroin. Siku chache baadaye alijikuwa amepewa vidonge 93 vya madawa hayo ambavyo kila kimoja kina gram 15 kwa jumla ya gram 1395 (sawa na paundi tatu hivi-MM). Kutokana na kuanza kupata matatizo na kutoka vidonda kijana huyo alijaribu kutaka kuacha biashara lakini akakumbushwa kuwa ana deni la 560,000Tsh na upande mwingine aliahidiwa kuwa endapo angefikisha mzigo ule salama basi angelipwa dola 5000. Akapewa mpango wa safari kwenda Hong Kong akiwa katika hali ya udhaifu mkubwa wa mwili.


Mwandishi alitarajia kuwa kutokana na hali mbaya basi wangekamatwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar. Hiyo haikuwa hivyo kwani kwa maelezo yake "Ajabu pale airport kulikuwa na mtu ambaye aliandaliwa kunipitisha mimi mpaka boarding room" anasema kijana huyo. Ilikuwa ni hali aliyokuwa nayo ndiyo iliwafanya maafisa wa Hong Kong kumtilia shaka na kumweka kizuizini.


Kitu ambacho mwandishi inaonekana hakuwa anakijua ni kuwa Hong Kong hawana huruma na watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya kwani wana vifungo vikali kabisa na kwa maelezo yake kuwa hadi hivi sasa kuna vijana wa Kitanzania karibu 150 ambao wameshafungwa na wengine wakiendelea kusubiri kesi zao ziendelee. Alichoshukuru Mwandishi ni kuwa angalau yeye na wenzake wamekamatwa Hong Kong kwani kama wangekamatwa China yenyewe basi wangenyongwa kwani tayari – kwa maelezo yake – wapo vijana wa Kitanzania walionyongwa huko.


Kwa maelezo yake ambayo yanashabihiana kwa kiasi kikubwa na taarifa za vyombo vya usalama vya kimataifa vinavyofuatilia biashara hii haramu mizigo ya madawa ya kulevya yanaingia nchini Tanzania yakitokea Pakistani na Afghanistan kupitia maeneo ya Tanga, Dar, Mtwara na Bagamoyo ambayo huja kwa boti na kupokelewa na wahusika wakubwa nchini.


Ikumbukwe kuwa mwaja jana Januari mtoto wa aliyekuwa afisa wa Benki Kuu Amatus Liyumba aitwaye Morine alikamatwa na wenzake huko Lindi akiwa na mzigo wa madawa ya kulevya wenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 9!
"Mizigo hiyo huwa inasindikizwa na magari ya jeshi na polisi na hii siyo siri kwani hata wahusika wanajua" amesema kijana huyo katika barua hiyo ambayo imewashtua Watanzania wengi baada ya kupostiwa katika mtandao maarufu wa JamiiForums siku ya Jumamosi.


Kuhusishwa kwa vyombo vya usalama na biashara hii haramu si jambo la kushangaza kwa watu ambao wamekuwa wakifuatilia kuenea kwa vitendo vya uhalifu nchini. Ipo mifano kadha wa kadha ambayo inaonesha kuwa baadhi ya watumishi wa vyombo hivi vya usalama wako ‘compromised' na haijulikani ni nani anaweza kuaminika. Baadhi ya mifano ni hii ifuatayo:



  • · Mwaka 2011 – Mwanajeshi wa JWTZ alikamatwa mjini Morogoro akijaribu kusafirisha magunia 12 ya bangi kutoka Iringa kuja Dar. Hii ilikuwa ni mwezi Disemba mwaka huo. Kijana huyo wa miaka 26 alikamatwa na askari wa polisi waliokuwa doria akiwa amevaa sare za jeshi hilo. Ni afisa wa Kambi ya Lugalo mwenye namba MT86879.
  • · Januari 2013 – Afisa wa JWTZ mwenye namba MT 59503 Sajenti Aziz Athumani alikamatwa huko Arusha akiwa na pembe mbili za ndovu.
  • Aprili 2013 - Askari wa Magereza Brighton Octavian alikamatwa katika gereza la keko akiwa na kete 732 ambazo inadaiwa alikuwa anazipitisha kwenda kwa wafungwa. Kuna ushahidi mkubwa wa uwepo wa mtandao wa kihalifu wa maafisa wa magereza ambao wamekuwa wakitumiwa na wafungwa kupeleka habari nje au kuleta habari ndani kutoka kwa mabosi wa madawa ya kulevya nchini.
  • · Julai 2013 – Hivi majuzi tu mwanajeshi mwingine Seleman Chasama (50) –katika hali ya kushangaza akili kabisa – amefikishwa mahakamani akishtakiwa makosa ya uhujumu uchumi na yale ya Uhifadhi wa Wanyama Pori baada ya kukutwa na pembe 357 za ndovu zenye thamani ya dola milioni 2.6.
  • · Julai 2013 – kabla hilo la mapema Julai halijatulia wiki iliyopita taarifa za maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza kukamatwa na nyara za serikali nalo zimeonesha kuwa hata Magereza nako si salama. Maafisa hao akiwemo Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP) Joseph Sauli, Warden Richard Barick na Koplo Silvester Bukha walikutwa wakitumia gari la Magereza kubeba Twiga 2, Pundamilia 2, Swalapalapala 2 na Mbuni 2 wote wakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 55!
Hiyo ni mifano michache tu ya kuhusishwa kwa maafisa wa usalama na mambo ya ujangili, madawa ya kulevya na hapo hatujaangalia uhalifu mwingine. Na hapa izingatiwe hawa ni wale ambao walikamatwa tu na hatujaangalia wale wa polisi ambao kama watu wanakumbuka waliwahi kutuhumiwa kujaribu kumtegeshea mtoto wa Mzee Mengi madawa ya kulevya pale Uwanja wa Ndege na barua hii inatupa mawazo tu jinsi gani hilo linaweza kutokea kweli.


Ikumbukwe barua hii imekuja tayari kukiwa na habari za mabinti wawili wa Kitanzania wamekamatwa Afrika ya Kusini baada ya kutua nchini humo na mzigo wa madawa ya kulevya wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6; na hawa waliondokea uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar-es-Salaam. Bila ya shaka kuna kuhusika kwa maafisa wa kikosi cha uhamiaji ambao wanawajibu wa kusimamia watu wanaoingia na kutoka nchini.


Vilevile, barua hii imekuja siku chache tu toka Mbunge wa Musoma Mjini Vicent Nyerere (CHADEMA) kuzungumza na waandishi wa habari kutaka serikali ijisafishe kwani inaonekana kuwaogopa vinara wa madawa ya kulevya. Katika tamko lake la Julai 19 Bw. Nyerere ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani alisema kwa ukali kuwa "Kupuuzia na kutochukua hatua kwa wahusika wa dawa za kulevya ni kuangamiza nguvu kazi ya taifa. Nguvu kazi ya taifa ikishaharibiwa na dawa za kulevya hatuna taifa tena. Hivyo Serikali ifahamu kwamba kuendelea kulifumbia macho jambo hili kwa manufaa ya mafisadi wachache ni kulihujumu taifa na huo ni usaliti dhidi ya kiapo ilichokula cha kulitumikia taifa na kusimamia usitawi wa wananchi wa Tanzania. Aidha, Serikali itambue pia kwamba kuendelea kukaa kimya bila kuchukua hatua yoyote juu ya jambo hili kunatoa dalili kwamba yamkini ya yenyewe inahusika na biashara hiyo."


Katika kuhitimisha barua yake, mwandishi wa barua hiyo alienda na kuwataja baadhi ya watu ambao wanahusika na mtandao wa madawa ya kulevya na namna ya ushiriki wao huku akisema kuwa wapo wengine ambao majina yao yakitajwa nchi itashtuka kwani ni watendaji wa ngazi za juu serikalini. Kwa mujibu wa kijana huyo wanaodaiwa kuhusika na biashara hiyo nchini ni hawa wafuatao (kama alivyoandika):



  1. 1. Beka Rangers – Yupo Magomeni Mapima na ana Bureau De Change, Magomeni.
  2. 2. Yasin – Yupo Sinza Madukani na amepanga floor nzima ya gofoa lililopo hapo madukani. Ana semitrailer za kusafirishia mizigo. Anajulikana sana.
  3. 3. Chonji – Yupo Magomeni Mwembechai na ana ghorofa analijenga hapo Mwembechai la ghorofa tano. Naye ni maarufu sana.
  4. 4. Ahmed Horohoro – Maarufu hapo Magomeoni Mapipa
  5. 5. Gatuso – Maarufu Magomeni Mapipa – Chipolopolo
  6. 6. Manganja – Sinza Uzuri Darajani. Ukitokea Magomeni kwenda Sinza –Uzuri baada tu ya kumaliza daraja, nyumba ya pili kushoto ndipo kuna ofisi yake.
  7. 7. Gasper – Vijana Kinondoni; ana ofisi ya stationery hapo vijana ni maarufu sana.
  8. 8. David Kanyau – Anajulikana hata na maaskari wengi.
  9. 9. Kogoko – Yupo Dar-es-Salaam, mizigo mingi inayoenda China ni ya kwake; maaskari wanamjua sana.
  10. 10. Mhe. Iddi Azzan – Magomeni – Huyu ni mbunge na asichanganywe na Musa Azzan "Zungu".
  11. 11. Tanaruza – Mwembechai
  12. 12. Shikuba – tajiri mkubwa, serikali inamtambua.
  13. 13. Wanaopokea mizigo huko China ni watu aliowataja kwa majina ya Omary na Shakur.
Barua yake hiyo ilitumwa kwa vyombo mbalimbali vya habari vya Tanzania. Kitu kimoja ambako kiko wazi ni kuwa kijana huyo amefanya kile ambacho watu wengi wameshindwa kukifanya japo wakiwa na uwezo wa kukifanya.


Kukithiri kwa biashara ya madawa ya kulevya nchini kunafichua tu ya kile kinachoendelea na kusukuma ‘gurudumu la maendeleo' nchini ambapo wakati watu wengine wanahenyeka kila siku kufanya kazi halali na kwa jasho lao lipo kundi ambalo limejikita hadi kwenye madaraka ambalo licha ya kufanya vitendo vya ufisadi serikalini lipo pia kwenye mtandao wa uhalifu (organized crime) na limejipenyeza hadi kwenye vyombo vya dola. Barua ya kijana huyu kuhusisha vyombo vya usalama yaweza kuwa ni andiko la mwisho kwa serikali ya Kikwete kuangalia utendaji wa vyombo vyake ambavyo anaonesha kuwa anaviamini sana.


Jambo la kutisha ni kuwa kutokana na watu wa makundi mbalimbali kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya tusije kushangaa hakuna mtu yeyote ambaye tunaweza kumwamini tena. Je, serikali itapokeaje taarifa hii? Je, kuna mtu mwenye ujasiri wa kupambana na kuufumua mtandao huu? Je, kama kijana huyu kawafanyia kazi yote na kuwatajia majina na mahali je serikali ya Tanzania ina maana kuwa miaka yote hii haijui watu hawa na kama haiwajui vyombo vya usalama kwanini vinatumia "intelijigensia" nyingi kwenye mikutano ya CDM badala ya wahalifu hawa wakubwa? Na kama watu hawa waliotajwa hawajulikani na vyombo vya usalama au wanajulikana lakini hawakamatwi je Kikwete anahalalisha vipi kuendelea kuwatumia watu wale wale walioshindwa kusimamia usalama wan chi? Si ni yeye aliyesema jusi kwenye sikukuu ya mashujaa kuwa nchi iko "salama". Kama yaliyomo kwenye barua hiyo ni kweli je tunaweza kusema kweli nchi iko "salama"? Salama kwa nani?


Maswali 2 ya kujiuliza na kufikirisha:
1. Kwa kila madawa yanayokamatwa na kwa kila watuhumiwa wanaokamatwa ni wangapi wanafanikiwa kupita na kuishia mitaani au nchi jirani?

2. Je, majina ya hawa waliotajwa yamo kwenye ile orodha aliyopewa Rais Kikwete, au ile ya viongozi wa makanisa au ile ya Kikosi cha Kuzuia Madawa ya Kulevya?



Niandikie:
mwanakijiji@jamiiforums.com
 
CCM has failed in many ways this is the time kuing'oa nchi kiuhalisia haiko salama,drug dealers,mafisadi ,wauaji nk ndo ambao wamebaki kuipa nguvu serikali ya sisiemu tena kwa manufaa yao binafsi na kukwepa mkono wa sheria,kwa taarifa hiyo tu inatakiwa ijitathmini na ikiendelea kuishikirilia without feedback(reaction) makes me to believe ccm ni kichaka cha maovu yote yanayojulikana duniani-wauaji,mafisadi,drug dealers,wakandamizaji,wanyonyaji,wahujumu uchumi n.k n.k
Imefika hatua nchi hii aliyoiacha Nyerere iko salama Mbunge ni drug dealer,Waziri fisadi,polisi wa kawaida jambazi,inspector muuaji,luteni ni Jangiri !!Nani hapo atamnyooshea mkono mwenzie..huu mtandao unatakiwa kung'olewa na watu safi,walio nje ya mfumo wao si wengine ni CDM

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Building penetentories, they build no school brainwash education to make us too full!
That could be poverty of our love!!!!!!!!!
So we gonna chase those crazy, chase those crazy bold-headed x2 Out of the town!!!!

Bob Marley, 1980, Dortmund,German.
 
Umenena MM. sasa nani atamfunga paka kengele. ndani ya serikali haijulikani na Raisi na polisi.
 
Muandishi pia amesema kuna baadhi ya vigogo wanauza poda kuwajata ni aibu inaweza ikaatarisha usalama wa nchi,frankly speakin' mkuu wa kaya na wanae wanauza sembe,idd azan tumetaja sana rejea uzi wa tuwatambue wauza unga wa may 30 lakini mod sijui wameuweka wapi? Idd Azan ni muuza unga mkubwa BONGOLALA kaja kumtetea humu kwamba hanaish nhc,kama anaish nhc basi ni zuga tu,muulize ile kesi yake ya kupigwa mil150 aliyönunua kiwanja hewa imeishia wapi?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kipindi nakaa Sinza huyo jamaa #2 anayeitwa Yassin namfahamu ni maarufu sana kitongoji hicho kwani ni kijana ambaye ana ukwasi wa kutisha gari anazotembelea tu si mchezo Audi Q7, BMW X6 na Benz McLaren pia ana Cargo ambazo ni Semi Trailler si chini ya 150 na hii Transportation ndo anapofichia uharamia wake.

Kifupi jamaa yuko fit kwenye mkwanja pia kuna tetesi hiyo ghorofa hapo ambapo kuna chuo cha Biashara amaeshainunua.
 
Building penetentories, they build no school brainwash education to make us too full!
That could be poverty of our love!!!!!!!!!
So we gonna chase those crazy, chase those crazy bold-headed x2 Out of the town!!!!

umechapia sana mzee ni to make us the fools
Hatred is your reward for our love
chase them crazy baldhead
 
Mkuu kipindi nakaa Sinza huyo jamaa #2 anayeitwa Yassin namfahamu ni maarufu sana kitongoji hicho kwani ni kijana ambaye ana ukwasi wa kutisha gari anazotembelea tu si mchezo Audi Q7, BMW X6 na Benz McLaren pia ana Cargo ambazo ni Semi Trailler si chini ya 150 na hii Transportation ndo anapofichia uharamia wake.

Kifupi jamaa yuko fit kwenye mkwanja pia kuna tetesi hiyo ghorofa hapo ambapo kuna chuo cha Biashara amaeshainunua.

Hawa wauza poda ndio wanaotudharaulisha mitaani wanapata fedha za kimagumashi na wana zi blow kweli kweli poda imewatoa wengi believe dat waanhe brrrr.
 
Hawa wauza poda ndio wanaotudharaulisha mitaani wanapata fedha za kimagumashi na wana zi blow kweli kweli poda imewatoa wengi believe dat waanhe brrrr.

We acha kaka amefanya vijana wengine wenye tamaa wamfuate,,ni kijana tu lakini huo utajiri si mchezo ni wa muda mfupi.
 
Kwangu mimi naona haya;
Uhusika wa vyombo vya usalama kwenye biashara haramu ya dawa za kulevya una baraka za wakubwa, kuanzia JK mwenyewe, mawaziri, viongozi wa taasisi mbalimbali na usalama wa taifa.

JK ameshindwa kukemea wala kutoa agizo kuhusu kukamatwa kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wanaofahamika. Na sasa, Tanzania ni nchi inayoongozwa na kundi la wahalifu, JK yuko pale kama figure/mwakilishi kuhakikisha kuwa hakuna kikwazo kwenye biashara zao
Kiongozi dhaifu, kwa taifa dhaifu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Swali la kujiuliza, kama dege la kijeshi liliingia anga ya nchi yetu na kutua ili kuwachukua wanyama wakubwa kama Twiga, tupo salama kweli? Kumbuka ni dege la kijeshi la nchi nyingine tena ya mbali.

Pili, dege hilo lililokuja kuchukua wanyama tuna uhakika gani kama halikupakua mzigo wa madawa ya kulevya kama sehemu ya biashara? Na ilishindikanje endapo halikujulikana limeingieaje nchini.

Tatu, gunia na nusu la madawa lipitaje uwanja wa ndege ili hali kuingiza laptop tu inakuwa nongwa?
Kilo 160 kupitia uwanja wa ndege! je nchi ipo salama.

Ricin ni sumu ya mbegu inayoweza kuua(lethal dose is 20-30 mg) kumbuka 1 Kg is 1000g.
Gunia moja na nusu linaweza kupita uwanja wa ndege, nini kinashindikana kupitisha robo kilo ya ricin yenye lethal dose kupita uwanja huo huo ulioweza kupitisha Kg 160.
Nchi ipo salama kweli?
 
Umeichambua vizuri hiyo barua lakini ulipoingiza mambo ya Chadema na CCM uchambuzi wako umekosa nguvu, kama suala la polisi kuwasumbua vyama vya siasa hawajaanza leo mbona haujawasema CUF wewe na Chadema tu.

Mwanakijiji ni mwanaharakati wa chadema.
 
Nchi hii inaongozwa na genge la wahalifu ambao kwa kiasi kikubwa wanatumia madaraka yao kama shield protection.
Nadiriki kusema Mr. Dhaifu ni kama kivuli tu kaz yake ni kuongea porojo tu bila kuchukua hatua yeyote
Kwa style hii unategemea nini hakuna wa kuwatetea vijana maisha yao yamekuwa magumu, ajira ni kilio so akitokea kupata dili ya aina hiyo ataifanya tu...
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji endapo wenye mamlaka hawakuelewa mwandishi wa barua ile, andiko lako hili lazima watalielewa. Ninachojiuliza ni je, ile orodha ya majina ya wanaofanya biashara hii ya madawa ya kulevya ambayo Mh Raisi aliwahi kusema kuwa anayo, alichukua hatua gani? Ama ndio ilikuwa mtaji wa Mabilioni ya Kikwete? na je, ipo haja kureview mpango ule wa mabilioni ya Kikwete ili kuona mafanikio yake?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom