mwanakijiji nakuja na critism ya hii hadithi ......i hope utaichukulia in a good way
ni hadithi nzuri ya mapenzi na nimevutiwa na style ya uandishi ya kumalizia kila sura kwa beti za nyimbo.
hata hivyo kwa vile umekaribisha kukoselewa pia mie nimeona mapungufu haya:-
1) kuna makosa ya kimaandishi mengi mno..........ama neno linajirudia mara mbili, au neno halimalizi, au neno la nyuma na la mbele limeunganika n.k. Inaondosha raha ya usomaji kwa kiasi flani.
2) Uandishi wako kuna baadhi ya wakati unaandika kama kwa kutumia kiswahili cha pwani ( kama watu wa pwani wanapoeleza kitu) , na baadhi ya wakati kinakuwa kiswahili cha bara. Kwa upande wangu huu mchanganyiko wa 'aina' ya kiswahili sounds a bit off na nafikiri ingependeza zaidi ungetupa mtiririko wa hadithi kwa kutumia 'aina' moja ya kiswahili.
3) kwa vile hii kazi yako ina lengo la kuendeleza na kuhifadhi kiswahili, basi unge achana na kutumia maneno ambayo yanatumika kimakosa mtaani lakini hayabebi maana halisi ilokusudiwa au maneno ambayo maana yake halisi ni moja na watu kwa kushindwa kuelewa wanatumia maana nyengine
tunasubiri kwa hamu maendeleo ya hadithi hii