Hadithi inaendelea kunoga, ahsante sana Mwanakijiji lakini chonde chonde isiishie hapo tafadhali.
Pia hadithi hii inatufundisha maisha halisi ya kwenye ndoa, usione watu wanacheka mitaani lakini wakiingia majumbani moto unawaka.
Ndio maana nyumba zinajengwa na mapaa, madirisha na milango kwa maana mambo ya ndani yabakie humohumo ndani msiwape watu wengine faida. Na wanaume (samahani kama nitawakwaza) huwa hawatosheki hata uwape nini, mwenye katabia kake kakupenda kufunua sketi haachi hata awe mwanamke mzuri kama malaika.
Na sie wanawake, wasichana wa kazi tuwe tunawapa uhuru angalau weekend wanatoka kwenda kusalimia jamaa na yeye aweze kupunguza haja zake ama sivyo mtakuta wote mnamuwindia mwanamme huyo aliyepo ndani. Lakini yakikuzidi mmmh kipoozeo muhimu au ndio uombe talaka la sivyo leo BP juu mara sukari mara oooh stroke na unamucha mwenzio anapeta.
Tujipe hongera sisi wanawake huwa tunavumilia sana kwa hawa viumbe na mungu ametupa moyo wa kusamehe lakini tunateseka kama binadamu kwa kutokuwa na uwezo wa kusahau. Inshallah