Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Kuna kasumba mbaya sana imejengeka ndani ya wafuasi na Wanachama wa Vyama vya Upinzani kuwa na akili mbovu ya kuwa wanalitakia mabaya taifa letu, kisa tu wao wamepoteza mvuto wa kisiasa hapa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa kama Upinzani ungekuwa unakubalika hapa Tanzania na upo ndani ya mioyo ya Watanzania, wananchi wangeikataa serikali ya CCM kwa udi na uvumba maana hakuna mtu ambaye yupo tayari kutawaliwa kwa mabavu na chama asichokitaka.
Kueneza uzushi kuwa kuna maambukizi ya COVID-19, huku mkifurahi utadhani kama huu mlipuko ukitokea hautawagusa ni uzembe wa kufikiri na kufirisika kisiasa. Mmesahau kuwa kete ya kususia bunge kwa minajiri ya kukwepa COVID-19 imesababisha mkakosa wabunge na kuporomoka kisiasa? Mbona hamjifunzi?
Mambo mengi mabaya mnaliombea taifa letu, kisa tu mmeshindwa uchaguzi. Huu ni upumbavu wa kisiasa.
Kwanini msiwe na subira mamlaka husika zikatoa taarifa kuhusu COVID-19? Kuliko kuwa mnazua uongo usio na kichwa wala miguu! Kwa nini msishinikize Serikali kutoa taarifa kamili kama kweli mnania njema na Watanzania.