Kuliombea mabaya Taifa letu haisaidii Upinzani kukubalika hapa Tanzania

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kuna kasumba mbaya sana imejengeka ndani ya wafuasi na Wanachama wa Vyama vya Upinzani kuwa na akili mbovu ya kuwa wanalitakia mabaya taifa letu, kisa tu wao wamepoteza mvuto wa kisiasa hapa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa kama Upinzani ungekuwa unakubalika hapa Tanzania na upo ndani ya mioyo ya Watanzania, wananchi wangeikataa serikali ya CCM kwa udi na uvumba maana hakuna mtu ambaye yupo tayari kutawaliwa kwa mabavu na chama asichokitaka.

Kueneza uzushi kuwa kuna maambukizi ya COVID-19, huku mkifurahi utadhani kama huu mlipuko ukitokea hautawagusa ni uzembe wa kufikiri na kufirisika kisiasa. Mmesahau kuwa kete ya kususia bunge kwa minajiri ya kukwepa COVID-19 imesababisha mkakosa wabunge na kuporomoka kisiasa? Mbona hamjifunzi?

Mambo mengi mabaya mnaliombea taifa letu, kisa tu mmeshindwa uchaguzi. Huu ni upumbavu wa kisiasa.

Kwanini msiwe na subira mamlaka husika zikatoa taarifa kuhusu COVID-19? Kuliko kuwa mnazua uongo usio na kichwa wala miguu! Kwa nini msishinikize Serikali kutoa taarifa kamili kama kweli mnania njema na Watanzania.
 
Tanzania awamu hii tumepatwa na laana. Wajinga na wanafiki wamepewa mamlaka ofisi mbalimbali. Halafu wananchi wanashauriwa na baadhi ya wapumbavu kuwa wawasubirie hao wajinga watoe kauli kuhusiana na uhai wao.

Corona ipo. Chukua tahadhari. Usiku huu imemchukua RC.
 
Hapa umeongea kinyume kwa Hali zote.

1. CCM haipendwi kabisa na Watanzania.

2. CCM inalijua Hilo wazi ndio maana wanatumia dola.

3. Watanzania waliowengi wamekata tamaa ya maisha chini ya ccm.

4. Mnajua watanzania hawawapendi ndio maana mmetunga sheria mbaya zinazowakandamiza na kuzuia Uhuru wa kutoa maoni.

5. Mnajua ubaya mliolifanyia taifa hili ndio maana mmeongeza wigo wa watu ambao hawatashtakiwa pindi wakitoka madarakani.

6. Kwataarifa yako kitu pekee CCM ilichowini ni kuwajengea hofu watanzania kwamba wakireact watauwawa au watatekwa.

7. Mlichomfanyia Ben Saanane na Tundu Lissu ndio kitu pekee watanzania walio wengi wanaogopa kufanyiwa Sasa mnapofanya makosa na hawareact sio kwamba wanawapenda wanahofia maisha Yao.

Muda ni mwalimu mzuri Sana siku mkiondoka madarakani ndipo mtakapowaelewa watanzania usiombe siku hiyo ikukute. Wanaojua ukweli wanajiwekea kinga za kisheria ili wakiondoka madarakani wasishtakiwe wewe endelea kusema upinzani hauna mvuto.
 
Mtoa mada wewe ndiyo mwenye akili mbovu! Sisi Watanzania Wazalendo hatuiombei mabaya Nchi yetu!

Kama ulikua hutambui, basi tambua kuanzia sasa!! Sisi tunaiombea mabaya Serikali ya Ccm na ccm yenyewe kwa kujimilikisha Nchi yetu kimabavu.

Na kama ulikua hujui, na Mabeberu wa Marekani nao asubuhi hii wamewawekea vikwazo hivyo hivyo vya kutoingia Nchini mwao kwa kuwahofia kumiliki hicho Kirusi kipya cha hiyo Corona! Walianza na Makonda, wakaja kwa akina Mahera, na sasa ni kwa Waenda Marekani wote!

Mpaka 2025, tutaelewana tu.
 
Sema sacco wana maumivu Makali sana, baada ya kunyimwa ulaji na sasa kazi yao ni kuliombea mabaya taifa,
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom