Kuliombea mabaya Taifa letu haisaidii Upinzani kukubalika hapa Tanzania

Wale wanaoamini corona ipo waendelee kuchukuwa tahadhari dhidi ya maambukizi. Wale wasioamini waendelee kujichanganya.

Kila mmoja ana maamuzi yake binafsi na kama mnaamini mlishinda uchaguzi kihalali basi endeleeni kuchapa kazi achaneni na Wapinzani. Fimbo ya Mungu ipo milangoni mwa Watesi wa Wapinzani.
 
Boss kwani huu uzushi juu ya Covid 19 unaletwa na akina nani?
Wewe tembea ukiwaaminisha ndugu zako kwamba Tanzania hakuna Covid19, waache wanaoamini ipo waendelee kuhamasishana wachukue tahadhari, ipo siku mwenye akili atajulikana kati yenu.

Hata Ukimwi kuna wanaoamini siyo halisi na wanakwenda kavu kavu wanaliwa, wapo wanaoamini kondomu ndo zinazoeneza Ukimwi wanaweka pembeni wanaliwa. Unapowazuia watu kupeana tahadhari juu ya maisha yao toa na mbadala wakiyapoteza watayapata wapi!!?
 
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya Watanzania hawana furaha na mwenendo serikali awamu ya 5 hususani kwa umoja na ustawi wa taifa letu. Hata H, M.... walitawala uzuri utawala dhalimu haudumu milele.

Bora walau busara na Hussein Mwinyi Zbar inaleta nuru.
 
Uzuri wa maradhi hayachagui; uwe raisi ama waziri,uwe CCM ama CUF, uwe masikini ama tajiri.Hizi sifa zakijinga kutokuwaambia wananchi ukweli kwamba corona ipo ili wachukue tahadhari sio sawa. Tunafahamu tatizo n pesa za watilii hivyo ni bora tufe kwa corona lakini pesa ya kigeni ipatikane.

Mnachotakiwa mjue madaktari hawakuzaliwa na chama,ma dk wanawazazi na ndugu zao ambao huwaambia ukweli kwamba CORONA ipo na ndio chanzo cha taarifa nyingi hapa mtandaoni.

Pigeni kelele kama kasuku ila siku inakuja ugonjwa huu utachukua wa karibu yako,utachukua mama ama baba,kaka ama dada ndipo utaelewa kwakua ninyi ndio wale kama kenge hamsikii mpaka muone damu masikioni.

Wazo lakutokuwa na lockdown ni zuri lakini hili lakutowaambia wananchi ukweli ili wachukue tahadhari ni ukatili mkubwa kwa wananchi.

Ila twendeni muda ni mwalimu mzuri.
 
Njia nzuri ya kuwashinda Waomba mabaya ni kuongeza idadi ya Waomba mazuri....kwa vipi?, sasa ndio tutafakari.
 
We kilaza Uingereza imepiga marufuku Watanzania kuingia nchini kwao sababu ya corona,undhani walishauriwa na Lissu au Mbowe? 😫
Hapo ndipo mnapotosha na kulisha sumu mbaya wanosoma hili badiko lako.

Si watanzania pekee ambao (hata hivyo ni lazima wawe na makazi ya kudumu huko UK) ndio wanaozuiwa kuingia UK bali ni abiria wote wanotokea Tanzania na ndege zinazotokea au kupitia Tanzania.

Hivyo ukisema UK imepiga marufuku kwa watanzania kuingia UK unakuwa wakosea.
 
Naona wiki hii unawawaza wapinzani tu....una mimba ya Bananga nini?

Chapa kazi wapinzani hawapo wamekuacha uchape kazi acha kulia lia.
Labda anajua wapinzani wameleta Corona .Nchi haina upinzani acha kulia lia we kilaza.
 
Tanzania awamu hii tumepatwa na laana. Wajinga na wanafiki wamepewa mamlaka ofisi mbalimbali. Halafu wananchi wanashauriwa na baadhi ya wapumbavu kuwa wawasubirie hao wajinga watoe kauli kuhusiana na uhai wao.

Corona ipo. Chukua tahadhari. Usiku huu imemchukua RC.
Watu wengine mna akili za kuku. unapoongozwa na mjinga na mpumbavu maana Yake wewe ni punguani kuliko kiongozi wako.
Pole nyumbu kwa kuongozwa na mjinga na mpumbavu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom