Marekani walipoenda Iraq kwa Saddam Hussein hawakuweza kufikia hata kwa theluthi walichokiweza Iran, yani Iran wameigeuza kama sebule yao, wanajipigia tu.
Osama alikuwa mwiba sana, hadi Marekani wanamkamata ilikuwa shughuli nzito.
Iran alitegemea zaidi kufanya mashambulizi kwa Proxies kama Hamas, Hezbolah, Houthi, Vikundi vya Iraq na Syria.
Iran kupigana Direct ni mchovu sana, Israel na Marekani zinaingia Iran kama vile sebuleni. walitumia SEKUNDE 60 tu kuwafyeka Ayatollah na viongozi wengine wakubwa wa jeshi. SEKUNDE 60.
Yani Israel na Marekani watautumia sana huu mfano kila muda wakielezea uwezo wa majeshi yao.
Hadi sasa wiki bado haijaisha ila mifumo ya ulinzi wa Iran ipo nyanga nyanga si rada wala meli, leo hii ndege ya kivita ya Iran iliyotaka kujaribu kupigana na F 35 za Israel imepigwa angani punde tu ilipopaa.
Na vita inazidi kuwa nyepesi kwasababu wananchi wengi wapo upande wa Marekani na Israel, wanaona wanakombolewa sio vita hii.