Ugaidi, Mashehe wa Uamsho na Uislamu ni dhana tu? Waislamu Wang'aka

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,042
20,404
Swali la kujiuliza, je ni kweli Uislamu ni ugaidi?
Je, wale mashehe wa uamsho wanaopanda kisutu ni magaidi, kwanini wana nia ovu na nchi yetu?
wangekamatwa nhi nyingine si wangesganyongwa? serikali inasubiri nini kuanyonga kwakuwa nia yao ilikuwa kuua watanzania wema?
Serikali inaogopa nini?
al shabab.jpg



Raia mmoja wa Tanzania ni miongoni mwa washukiwa watatu wa ugaidi nchini Kenya waliopatikana na hatia ya kutekeleza shambulio la mwaka 2015 katika chuo kikuu cha Garissa lililosababisha mauaji ya takriban wanafunzi 148.

Mtanzania huyo kwa jina Rashid Charles Mberesero pamoja na Hassan Edin na Mohammed Abdi jina jingine Mohamned Ali Abikar walipatikana na hatia ya kupanga shambulio hilo chini ya ushirikiano wa wanachama wa kundi la Al-Shabab.

Pia walipatikana na hatia ya kuwa wanachama wa kundi la al-shabab kutoka Somalia.


Mamlaka za usalama nchini Tanzania zimewatoa hofu wananchi juu ya tishio la ugaidi katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, zikisema zilikuwa na taarifa hizo na kwamba zimeshaanza kufanyiwa kazi.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amesema kuwa jeshi lake lilishapata fununu za shambulio hilo kabla Ubalozi wa Marekani kutoa tahadhari juu ya tukio hilo kupitia tovuti yake Juni 19,2019.
Kuhusu tahadhari iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Sirro alisema: "hiyo ni taarifa kama taarifa nyingine, inaweza kuwa ya kweli au uongo, lakini sisi kama vyombo vya ulinzi huwa hatupuuzi jambo''.

Aliongezea kuwa walipata taarifa kuhusiana na tishio hilo Tangu siku ya Jumanne Juni 17, 2019 tulipata na kwamba timu zao za operesheni na intelijensia na wengine wanaifanyia kazi.


Katika tangazo lake Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari kuwa kuna fununu za mipango ya mashambulizi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa tahadhari hiyo iliyochapishwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Ubalozi huo, eneo la Masaki ndilo linalolengwa.

Eneo hilo lililopo kwenye rasi ya Msasani ni moja ya maeneo ya makazi ya kigahari zaidi jijini humo.

Tahadhari hiyo inabainisha kuwa, maeneo yanayolengwa ni mahoteli na migahawa ambayo hutembelewa na watalii ikiwemo eneo maarufu la maduka ya Slipway.

"Ubalozi hauna ushahidi wa moja kwa moja wa tishio hilo ama taarifa za muda gani mashambulizi yatatokea, hata hivyo unawaonya wananchi kuchukua tahadhari."

Ubalozi huo aidha umewataka wakazi, kujiepusha na makundi na kufuatilia taarifa kupitia vyombo vya habari.


Kumbukumbu ya Mashambulizi ya mwaka 1998

Miaka zaidi ya 20 iliopita wapiganaji wa jihadi walishambulia kwa pamoja balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania, na kuanzia wakati huo Ugaidi umeendelea kukita mizizi Mashariki mwa Afrika.

Ilikuwa tarehe 7 mwezi Agosti mwaka 1998, saa nne na nusu asubuhi, wakati wauaji wawili walilipua lori moja lililokuwa limejaa mabomu mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, nchini Kenya.

Dakika tisa baadae bomu lengine likalipuka katika balozi nyengine ya Marekani mjini Dar es Salaam katika nchi jirani ya Tanzania.

Takriban watu 242 waliuawa katika mashambulizi hayo mawili yalioharibu kabisa balozi hizo za Marekani na kusababisha kuporomoka kwa nyumba zilizokuwa karibu.








Dola la Kiislamu Iraq na Syria (ISIS)

Wafuasi wengi wa kundi hili ni waumini wa madhehebu ya Sunni wenye msimamo mkali wa kidini. ISIS imepata nguvu kwa mda mfupi tu na kueneza ushawishi wake katika maeneo yote wanayoyadhibiti nchini Syria na Iraq. Muongozo na nadharia yao ni kifupisho cha jina lao - ISIS au Dola la Kiislam kuanzia Iraq, Syria na katika eneo la Sham.

Lengo lake ni kubuni dola kubwa la Kiislam litakaloziunganisha Syria, sehemu ya Iraq, Lebanon na sehemu kubwa ya Palestina na Jordan. Kundi hili linasemekana kuwa na msimamo mkali zaidi kuliko hata al-Qaida. Sehemu kubwa ya operesheni zake zinagharimiwa na wafadhili binafsi kutoka mataifa ya Ghuba, hasa Qatar na Saudi Arabia.

Vyenzo vyengine vinavyowapatia fedha ni visima vya mafuta kaskazini ya Syria na hongo. Wataalamu wanakadiria kundi hili la kigaidi lina wapiganaji wasiopungua 10, 000 na kwamba limejivunia umashuhuri mkubwa zaidi katika ugomvi kati ya jamii ya Sunni walio wachache na Shia wengi nchini Iraq. Zaidi ya hayo, ndani ya kundi hilo muna pia wanamgambo kadhaa wa kigeni waliojitolea kupigana jihadi, baadhi yao wakiwa ni wale waliosilimu.


Al-Nusra Front la Syria
Al-Nusra linaangaaliwa kuwa ni tawi la al-Qaida na jina lake linamaanisha "Waungaji mkono wa umma wa Syria". Linatajikana kuwa kundi muhimu kabisa la waasi nchini Syria. Malengo yao ni pamoja na kuundwa kwa dola la Kiislamu nchini Syria na katika eneo la Mashariki la Bahari ya Kati.

Al-Nusra linakadiriwa kuwa na wafuasi kati ya 5,000 na 7,000 wanaokutikana zaidi katika eneo la kaskazini mwa Syria, ingawa hivi karibuni lilitangaza utiifu wake kwa hasimu wake wa zamani, ISIS.



Boko Haram la Nigeria
Jina la kundi hili linamaanisha kwa ufupi kuwa "elimu ya Magharibi ni dhambi". Wanapigana kwa sehemu kubwa kaskazini ya Nigeria na wanapigania utawala wa Sharia ya Kiislamu kote nchini Nigeria. Wafuasi wake wanajulikana zaidi kutokana na utekaji nyara. Umaskini uliokithiri na ukosefu ajira kaskazini mwa Nigeria unawarahisishia kazi viongozi wa Boko Haram kuwasajili wanamgambo wapya.

Vikosi vya usalama vya Nigeria vina pata shida ya kukabiliana na magaidi hao wenye silaha za kila aina. Tangu mwaka 2003 ,mashambulizi yamekuwa yakifanyika dhidi ya vikosi vya usalama, idara za serikali, makanisa na shule na maelfu ya watu kuuliwa. Katika miezi minne ya mwanzo ya mwaka 2014 pekee,watu waiopungua 4,000 wameuwawa kutokana na mashambulizi ya Boko Haram.



Al-Shabab la Somalia
Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (HSM) au al-Shabaab (Vijana) kwa ufupi ni kundi la wanamgambo wa Kiislamu lililoundwa kati ya mwaka 2004 na 2006 nchini Somalia, wakati nchi hiyo ikiwa tayari imeshazama katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kundi hilo linapigania kuundwa kwa dola la Kiislamu katika Pembe ya Afrika. Nadharia yao ya itikadi kali ya dini ya Kiislamu haitambui mipaka. Wanafanya mashambulizi hivi sasa katika eneo lote la Afrika Mashariki -mfano katika mji mkuu wa Kenya ambako mashambulizi yake katika jengo la maduka makubwa la Westgate Septemba 2013 liliangamiza maisha ya zaidi ya watu 60.

Al-Shabaab wanadhibiti sehemu kubwa ya eneo la kati na kusini la Somalia. Wakuu wa kundi hilo, wengi wao wakiwa raia wa kigeni, wanashadidia kushirikiana na al-Qaida katika kuwapatia mafunzo wanamgambo. Zaidi ya hayo, kundi hilo lina mafungamano na Boko Haram



Ansar-al-Sharia la Libya na Tunisia
Wenyewe wanajiita "Wafuasi wa Sharia ya Kiislamu" na kundi hili lina makao yake nchini Libya na Tunisia. Makundi madogo madogo ya Ansar-al Sharia yanakutikana pia kwenye mataifa mengine ya Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini. Lengo lao ni kuanzisha sheria ya dini ya Kiislamu.

Ngome ya Ansar-al Sharia, tawi la Libya, ipo Benghazi, ambako ni kitovu cha uasi uliokuja kumuondoa madarakani Muammar Gaddafi.

Kundi hilo linabebeshwa jukumu la mashambulizi dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi, tarehe 11 Septemba 2012, ambayo yaliuwa watu wanne, ikiwa ni pamoja na balozi wa Marekani nchini Libya. Ansar-al Sharia linasemekana kuwa na mafungamano na al-Qaida, ingawa wenyewe wanakanusha dhana hizo.



Hizbullah la Lebanon
Kundi la wanamgambo wa Hizbullah nchini Libnan limeundwa mwaka 1982. Wanajipatia uungaji mkono kutoka mashirika na taasisi za madhehebu ya Shia nchini Iran na Syria. Tawi la kijeshi la kundi hilo linaangaliwa nchini Marekani na katika nchi za Umoja wa Ulaya kuwa ni kundi la kigaidi. Waamgambo wake wanapigana upande wa vikosi vya Rais Bashar al-Assad nchini Syria


Hamas la Palestine

Vuguvugu la Kiislamu la Hamas limeundwa mwaka 1987. Hilo ni tawi la Chama cha Udugu wa Kiislam katika Palestina. Baada ya Fatah, chama cha kiongozi wa utawala wa ndani wa Palestina Mahmoud Abbas, Hamas ni kundi la pili muhimu linalowawakilisha Wapalestina.

Kinyume na Fatah, Hamas hawaitambui Israel. Lengo lao ni kuiona dola la Israel linateketezwa. Na ili kulifikia lengo hilo, wanatumia mbinu za kigaidi. Katika miaka ya '90, walifanya mashambulizi kadhaa ya kuyatolea muhanga maisha nchini Israel.

Tangu mwaka 2007, Hamas ndio wanaotawala katika eneo la Gaza katika wakati ambapo Fatah wanatawala katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Hivi karibuni, Fatah na Hamas wamesikilizana na kuunda serikali ya umoja. Israel imeanza kuwaandama na kuwakamata wafuasi wa Hamas, tangu walipotekwa nyara vijana watau wa Kiisraeli.



Al-Qaida - gaidi wa ulimwengu

Al-Qaida wanajulikana kama mama wa makundi yote ya jihadi ulimwenguni. Jina lake linamaanisha "msingi" ama "chanzo kikuu." Ndilo kundi lililopanga mashambulizi ya Septemba 11 2001 dhidi ya Marekani. Lengo lake ni kusimamisha dola la Kiislamu ambalo litayajumuisha mataifa yote ya Waislamu na waumini wa dini hiyo.

Baada ya kifo ya kiongozi wake, Osama bin Laden, al-Qaida sasa inaendeshwa na Aiman al-Zawahiri, ambaye ni mzaliwa wa Misri. Hivi leo, mtandao huo una matawi mengine kadhaa yanayojitambulisha nao katika mataifa mbalimbali duniani, kama vile al-Qaida ya Magharibi na Kaskazini mwa Afrika (AQIM), ambayo inaendesha harakati zake kutokea Algeria hadi Mali, na pia tawi lake la Yemen, ambako ni kitovu cha wapiganaji wa jihadi.

Mwandishi: Sven Pöhle/DW Politik
 
Wawaache tu wale wazee hawana kitu na washatepeta,
Ni maalim tu ndo alowaponza na kuwashawishi kutaka zanzibar ijitawale wkt zanzibar ni sehemu halali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania
 
uamsho waliwaunganisha wazanzibar bila kujali vyama,wakajali dini yao na uzanzibar wao..hilo ni hatari kwa afya ya muungano
 
Nini faida ya muungano kwa dunia ya kizazi cha sasa?
kuna padri huko zanzibar alijibu hili nafikiri kama kumbukumbu zangu hazijatoboka,ilikua 2005 hivi nadhani,zamani palikua na imani kwamba jambo la zanzibar linaenea maziwa makuu pote
 
Wale masheikh kama magaidi kwanini wasihukumiwe mpaka leo? Mnajaribu kutaka kuupaka matope uislamu lakini mnashindwa, hivyo vikundi vyote mlivyovitaja havijafanya kama mauaji yaliyofanywa na US na wenzake dhidi ya waislamu. Na waasisi wa Taliban, Al Qaida na ISIS ni wamarekani wenyewe. Hakuna muislamu mwenye kushabikia uharibifu au mauaji kwa wanadamu wengine unless akiwa ameanza kutendewa ubaya yeye.
 
Ninatumai siku moja utakuja kuamini hawa wanaoitwa Magaidi ni Waislamu safi
Magaidi kwa ufupi ni Jeshi la Kiislamu.
Lengo lao wanataka dunia iendeshwe kwa mujibu wa Sharia na Taratibu za Dini ya Kiislamu.
Ndio maana wanaojiita Islamic State.
Uislamu sio dini tu, Uislamu ni Dola yenye mamlaka kamili.
Yenye kuihitaji maisha ya Kiislamu.
Ujue njia za kuueneza Uislamu katika dunia nzima kwa njia ya Amani imeonyesha kushindwa.
Hivyo hao wanaojiita Magaidi Sera yao ni kuueneza Uislamu kwa kwa njia ya nguvu au Vita.
Ndio maana wakivamia eneo la watu na kufanikiwa kuyashinda majeshi ya Serikali wanapandisha Bendera yao yenye maneno ya nguzo moja ya Dini ya Kiislamu, Shahada.
Hapo inamaana eneo lipo chini ya Sharia ya Kiislamu, hapo ukigundulika umeiba basi mkono ni lazima ukatwe.
Tunamshukuru Mungu aliyeumba Mbingu na nchi kawanyima nguvu hao mamjamaa. Na kamwe hawataweza kutimiza lengo lao hilo.
 
Back
Top Bottom