Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
2,199
6,890
B6301FD5-524C-4F9A-AE5D-CF0DA822F660.jpeg
Wale walioko Arusha na viunga vyake leo tumeshuhudia/kuona Mh. Raisi mama Samia Suluhu Hassan kaongezewa ulinzi mara dufu, tofouti na tulivyozoea na msafara wake umekuwa na ulinzi mkali na idadi kubwa ya askari na usalama wa taifa kitengo cha ulinzi.

Pia msafara wake una magari zaidi ya 70 kutoka 20 ya awali kama tulivyokwisha zoea, msafara huu umeambatana na helikopta mbili kama tulivyokuwa tukiona enzi za Hayati John Pombe Magufuli.

Cha kushangaza amekuwa akisisitiza kauli kama ile ya Hayati John Pombe Magufuli ya kwamba “aombewe”, kulikoni?

Je, hii misafara mikubwa sio janja janja ya baadhi ya watumishi wakubwa kujilipa posho kubwa kubwa ilihali, wananchi wanalia maisha magumu katika awamu hii ya sita?

Tujadili.
 
Hili swali linawahusu TISS, na kwa bahati mbaya hawawezi kukujobu
Pia kuna wale wenye mabunduki ya kivita warefu pua zao zimechongoka kama wanyarwanda, kuishi kwangu Tanzania sijawahi kuona watu warefu kama wale, je ni wa vitego pia ama ni kutoka nchi za jirani? Maana hata huku mtaani hawaonekani kabisa wale watu warefu wenye mabunduki ya kivita
 
Mimi ile kauli ya kwamba Watanzia mniombee imenishtua sana, pia sioni haja ya msafara kuwa na walinzi wengi kiasi kile wakati Tanzania haina historia ya ulipuzi wa viongozi
Kwani maadui hawawezi kutoka nje ya nchi? Unasubiri itokee hatari kwanza ndio ulinzi uimarishwe? Hizo ni fani za watu jomba sio kila jambo atalijua kila mtu.
 
Kwani maadui hawawezi kutoka nje ya nchi? Unasubiri itokee hatari kwanza ndio ulinzi uimarishwe? Hizo ni fani za watu jomba sio kila jambo atalijua kila mtu.
Kama ni fani yao mbona kipindi kaenda Marekani hao hao unaowaita wabobezi walisahau majukumu yao hadi kushika simu ya raia na kusaidia kupiga picha, je kile kitendo ni sawa ama si sawa?
 
Ameshajua kuna kundi flani lina mind sana! Kumbuka siku ana waapisha wale majaji na wateule wengine,alisema anapotengua watu,sio anawatengua sababu ya kabila lao, anatengua sababu ya kushindwa kwao kazi! Sasa hii kauli ni nzito sana kutolewa na head of the State! Ukute Pamba FC, wame mind sana watu wao kuliwa vichwa!
Huwenda maana sio kwa ulinzi ule nilioona kwa siku ya leo, na hizi kauli za kuombeana huwa zina beba maana nzito sana
 
Japo siukubali utawala wa kihafidhina wa ccm, lakini ninavyoelewa ni kwamba msafara wa rais unaongezeka kutokana na sababu kadha wa kadha.mfano inategemea ziara yake inahusu nini , pia kuna mdau amegusia swala la ulinzi wa rais. Rais lazima apewe ulinzi maana yule ni kiongozi wa nchi tayari hivyo basi ulinzi wake unaimarishwa mara dufu

MÊmENtO HoMO
 
View attachment 1977510Wale walioko Arusha na viunga vyake leo tumeshuhudia/kuona Mh. Raisi mama Samia Suluhu Hassan kaongezewa ulinzi mara dufu, tofouti na tulivyozoea na msafara wake umekuwa na ulinzi mkali na idadi kubwa ya askari na usalama wa taifa kitengo cha ulinzi.

Pia msafara wake una magari zaidi ya 70 kutoka 20 ya awali kama tulivyokwisha zoea, msafara huu umeambatana na helikopta mbili kama tulivyokuwa tukiona enzi za Hayati John Pombe Magufuli.

Cha kushangaza amekuwa akisisitiza kauli kama ile ya Hayati John Pombe Magufuli ya kwamba “aombewe”, kulikoni?

Je, hii misafara mikubwa sio janja janja ya baadhi ya watumishi wakubwa kujilipa posho kubwa kubwa ilihali, wananchi wanalia maisha magumu katika awamu hii ya sita?

Tujadili.
Hivi, tozo zilisitishwa kwani?
 
Back
Top Bottom