Kulea wazee katika familia zetu

Kulea wazee katika familia zetu

kwann mliamua kukaa na huyo bibi kwenye mji wenu yani nyumban kwenu?
hongera sana kwa kufanikiwa kumwona bibi yake mama yako

Alikua mbali nasi then alikua ameshakua mtu mzima hakuna mtu wa kumuangalia kwa umakini ndie mama akamchukua ili apate huduma nzuri akiwa nyumbani kwetu....
 
gfsonwin hujambo mdogo wangu? Nafurahi kukuona.

B2T, in general malezi ya wazee yanahitaji uvumilivu, umakini na upendo wa dhati wa kila anaemzunguka hasa kama ni familia.

Ni ngumu kidogo kueleza ama kuwa na namna moja ya malezi ya wazee, kwa misingi kuwa watu wazima wengi wametofautiana namna ambavyo wanazeeka tokana na hulka ama tabia zao wanapokuwa kabla ya hali ya uzee sana. Pia na afya yao ni kigezo kikubwa cha malezi na uangalizi atakaopaswa kupewa. Hivyo mwisho wa siku inategemea zaidi upendo dhidi ya mzee huyo toka kwa wale ambao yupo chini ya uangalizi wao. Upendo utafanya kuwajibika zaidi, kujali zaidi, kuwa karibu na pia kuhakikisha vile vilivyo msingi na mhimu vinatimizwa.
Mimi nadhani dada mkubwa gfsonwin anataka kupata uzoefu. Hebu tujaalie uzoefu wako wewe.
 
Last edited by a moderator:
nimekuelwa sana da mkubwa, nafkiri unajua vyema kwamba bibi yangu mzaa mama yupo na ni mzee sana na kwa bahati mbaya sana yeye ana osteoporosis kiasi kwamba hadi mgongo umepinda lkn hatak kuskia tunasema tumchukue tukae nae manake anaona ananyimwa uhuru wake na kubwa analodai ni kwamba yeye hawez kuondoka akaacha kaburi la mumewe peke yake wala akaacha ng'ombe na mbuzi wake ambao kwasasa sidhan kama hao ng'ombe na mbuzi wana msaada sana manake ni gharama tu kubwa za utunzaji. tulichoamua ni kumuhudumia huko huko nyumban kwake ingawa hili linaleta ugomv sana kati ya yeye na mama yangu, mama anaona mama yake ni mkaidi huku bibi anaona mwanae anataka kumuhamisha kwenye mji wake. hii ni scenario ya kwanza.

scenario ya pili......... unajua wazi kwamba babu mkwe na bibi mkwe wetu kwa Kaizer wapo hai. mama mkwe wetu akaamua kuwachukua akae nao nyumban kwake ili awasaidie, sisi sote tuliafiki. sasa ishu inakuja babu ni mzee kuliko bibi ikabidi tukubaliane kutafuta msaidizi wa babu manake miaka 101 sio midogo. sasa bibi (88) anaona babu ana raha sana manake anamsaidizi na kuanza kulalamika mara ooh..........babu yenu anaraha sana yeye ana hadi mtu wa kumwogesha na kumfulia, mimi sijui lini nitapata. yeye bibi anaumwa sukari na presha sasa kwenye menu ukimpa chakula ambacho hakina chumvi kimechemshwa tuu anaanza kulalamika ""mwenzangu mie ana raha sana yeye kila kitu anakula lkn mimi yaani hata mayai tu nanyimwa kula"" yaani hapa huwa nakosaga hata la kusema manake linakera sana

kumbuka babu kazeeka hadi nguvu zimemwishia hawez kutembea yaani tunamtoa nje kuota jua na kumwingiza ndani yeye bibi bado kigori manake anatembea kwa miguu yake. lakin kila kukicha analalamika tuuu kwamba anakula vibaya yeye, anateseka yeye, ana tabu yeye hebu niambie kwa hizi scenario mbili unapata picha gani??

Dada mkubwa ukikaa na wazee kama hao unapowasikiliza, hutakiwi kutilia maanani sana wanayosema (Kwa maana ya kuumizwa na maneno), vinginevyo unaweza kumsemea maneno mabaya sana mzee wako. Ndio maana kwa sisi waislamu, imesisitizwa sana kuishi vizuri na wazee na ni haramu hata kumgunia (mguno wa maudhi) mzee wako. Kinachotakiwa ni kumsikiliza halafu fanya vile ambavyo unaweza kuhakikisha anapata matunzo mazuri na pale unapoweza angalau aridhike (Ingawa kwa uzoefu wangu naona hili la kuridhika ni kama huwa halipo hivi).

In short just do your best and ignore what they say as much as you can (Without showing that you are ignoring them). Pia inabidi uweke mambo katika mizani kwa kujitahidi kuwasikiliza pale inapobidi. Uzuri wengine hata wao wenyewe huwa wanajua kuwa ni wasumbufu.

Huyo bibi mkwe ataendelea kusema na kulalamika hivyo hivyo. Of coz if she has nothing else to do, what do you think she is gonna do? (She is still a human being)
 
ni kuwalea kama umleavyo mtoto mdogo kwa upendo na kumjali lakini pia uvumilivu aiseeeeeeee
Mtoto mdogo ni rahisi. Akikuzingua unamuadabisha anatulia, mzee utamfanya nini? Acha kabisa kazi ya kukaa na mzee mkorofi ni ngumu asikwambie mtu.
 
Mama Mkwe ana umri wa miaka70 , Baba Mkwe ana 78 na Bibi mzaa mama ana 92. Wanaishi pekee yao na mdada wa kazi.

Mama anafanya kazi zake kama kupika na kufua. Tena kufua ndo usiseme kabisaaaa hafuliwi nguo zake na yeyote.

Tunachokifanya ni kumsaidia tu wadada wa kazi pamoja na ku provide mahitaji yao yote.

Am old fashioned in matters of taking care of the aged na when my Dad is old am gonna take care of him by myself.
Hawa wako poa shukuru Mungu. dada mkubwa gfsonwin anazungumzia wale ambao kwa namna moja au nyingine hawajiwezi, wale ambao msaada wa dada wa kazi peke yake hautoshi. Hawa bwana kuna kazi kubwa sana.

Mimi nadhani lile suala la kupoteza uhuru na kutegemea watu wengine pia linakera sana na linachangia kwa kiasi kikubwa kuanza kwa usumbufu. Kwa mfano ukiangalia kwa sehemu kubwa wale wazee ambao wamejaaliwa afya na bado wanaweza kufanya shughuli zao (wengine hata za kuwaingizia kipato) ni nadra kusikia wakilalamikiwa usumbufu.
 
Karucee mimi pia huwa sikomplecate maisha kwenye kuwalea wazee, but mimi napata shida moja tuu nayo ni sipendi mtu anayenung'unika nung'unika kila saa na ukweli hata wanangu wanajua hilo sasa unakuja kukutana na mzee ambaye ulalamish ni sehem ya maisha yake how do you handle??
You work on getting used to it. There is no any other way out sister.
 
Alikua mbali nasi then alikua ameshakua mtu mzima hakuna mtu wa kumuangalia kwa umakini ndie mama akamchukua ili apate huduma nzuri akiwa nyumbani kwetu....

je alikuwa mzee kiasi cha kushindwa kujihudumia?? yaani alifika miaka kama 80+ hivi??

je hakuwah kuona kama vile amenyeng'anywa uhuru wake?
 
Yeah napenda sana kuongea kwa watu niwapendao mazungumzo yangu 95% ya utani.....

swala la kaupenda kuongea na kutania watu uwapendao ni zuri sana na mie huwa najitahd sana kutania wazee wangu ila tu nina wazee wakorofi kiasi kwamba nataman kujua ujanani walikuwaje
 
Dada mkubwa ukikaa na wazee kama hao unapowasikiliza, hutakiwi kutilia maanani sana wanayosema (Kwa maana ya kuumizwa na maneno), vinginevyo unaweza kumsemea maneno mabaya sana mzee wako. Ndio maana kwa sisi waislamu, imesisitizwa sana kuishi vizuri na wazee na ni haramu hata kumgunia (mguno wa maudhi) mzee wako. Kinachotakiwa ni kumsikiliza halafu fanya vile ambavyo unaweza kuhakikisha anapata matunzo mazuri na pale unapoweza angalau aridhike (Ingawa kwa uzoefu wangu naona hili la kuridhika ni kama huwa halipo hivi).

In short just do your best and ignore what they say as much as you can (Without showing that you are ignoring them). Pia inabidi uweke mambo katika mizani kwa kujitahidi kuwasikiliza pale inapobidi. Uzuri wengine hata wao wenyewe huwa wanajua kuwa ni wasumbufu.

Huyo bibi mkwe ataendelea kusema na kulalamika hivyo hivyo. Of coz if she has nothing else to do, what do you think she is gonna do? (She is still a human being)

yaani my brodah hapo kwenye ku-ignore ndipo penye shida sana wewe uliwezaje hilo??

imagine jana babu mkwe was so weak na he had coughs na kwakua hawez kukohoa had kutema makohozi alipewa dawa ambayo itamsaidia makohozi yatoke hata kama naiaa akwa kutapika..... ukweli mida ya asbh akatapika and mimi kwa kuona hilo i had to wash him manake he puke all over the bed and things were mess, kilichotokea sasa grandy ma akaanza bora yake na mwenzangu ana mtu hata wa kumwogesha mimi sijui kwenye uzee wangu kama nitampata wa kuniogesha she is 80+ now lkn ana complain hana mtu wa kumsaidia.

ukweli nilikasirika manake niliona hivi haoni kama mumewe anaumia hata kwa kuogeshwa kwa mjukuu wa kike yeye anaona anapata raha tuu, bibi yuko stable kiasi kwamba she can manage taking care of herself babu yeye hawez jamani anahitaj hata mtu wa kumlisha.

the worse thing babu yuko kwenye stage ambayo hata mfanyakazi wa kumuhudumia unaona tabu manake who will be ready ku mwogesha, kumfulia, kumtawaza kumlisha kila siku hata kama analipwa hela?? inabidi sisi wajukuu ndo tufanye hivyo sasa na penyewe bado bibi analalamika hafanyiwi khaaa!!!
 
Hawa wako poa shukuru Mungu. dada mkubwa gfsonwin anazungumzia wale ambao kwa namna moja au nyingine hawajiwezi, wale ambao msaada wa dada wa kazi peke yake hautoshi. Hawa bwana kuna kazi kubwa sana.

Mimi nadhani lile suala la kupoteza uhuru na kutegemea watu wengine pia linakera sana na linachangia kwa kiasi kikubwa kuanza kwa usumbufu. Kwa mfano ukiangalia kwa sehemu kubwa wale wazee ambao wamejaaliwa afya na bado wanaweza kufanya shughuli zao (wengine hata za kuwaingizia kipato) ni nadra kusikia wakilalamikiwa usumbufu.
yeah nazungumzia mzee wa ambaye hajiwez yaanai yule ambaye anahiataj msaada hadi wa kulishwa napengine hadi nati zimeshakatika kwa kuzeeka
 
je alikuwa mzee kiasi cha kushindwa kujihudumia?? yaani alifika miaka kama 80+ hivi??

je hakuwah kuona kama vile amenyeng'anywa uhuru wake?

Yeah alikua anafika wala hakuwa akilalamika sana ila akimis kwake tunampeleka alafu tunamrudisha ila si unajua tena mtu mzima siku nyengine anakasirika bure bure chakula hataki hadi tumbeleze
 
swala la kaupenda kuongea na kutania watu uwapendao ni zuri sana na mie huwa najitahd sana kutania wazee wangu ila tu nina wazee wakorofi kiasi kwamba nataman kujua ujanani walikuwaje

Mie mzee yeyote nkimuona mtu poa basi anakua best friend....wazee wangu wote wapo cool sana
 
Eiyer naona kama vile unaongelea wazee wenye nguvu zao,

hebu niambie unawezaje kuepuka kumkwaza mzee ambaye yuko above 80??

Nadhani unajua kuwa ili uishi na mtoto vizuri wakati mwingine unatakiwa uwe kama yeye

And so hawa wazee ......!!
 
Nafurahi kila nikikuona hapa

Lakini tutashindwana hizi mambo zako za kupotea ....lol!

Nafurahi pia Eiyer, sana tu.

Usijali, saizi si ahidi ili unione kwa vitendo 🙂
 
my dearest.............nafikir kuna jambo silielewi katika hii dunia.labda leo waweza nifumbua macho, hivi inawezekana wewe kumwogesha babu yake Kaizer?? je ule mwiko wa mkwe unaufanyaje hapo??

nafkiri upendo ndio jambo la msingi sana katika kuwalea wazee lkn unadhan utawezaje kuchukulia poa manung'uniko ya mzee ambaye hata anacholalamika hakina mantiki?? hivi unatakiwa ku assume nini ili wewe uweze kuachilia moyo wako kwa huyu mzee??

Kuna nyakati katika masuala haya unalazimika kufanya vitu ambavyo katika hali ya kawaida haikubaliki na pengine ni taboo kabisa. Suala la kuogesha ni kheri hata ukatafuta kijana ambaye yeye kazi yake itakuwa kuongesha tu, maana kwa kulifikiria tu mtihani kidogo. Haifai kwa kweli mie kumwogosha babu yake baba watoto; ila sasa bora kumuogesha yeye kuliko kumuogesha baba wa baba watoto.

Hapo suala la namna ya kumhandle mzee... Ndiyo maana mara nyingi ni kheri tu kumhandle kama mtoto mdogo (lakini kwa adabu).
 
yaani my brodah hapo kwenye ku-ignore ndipo penye shida sana wewe uliwezaje hilo??

imagine jana babu mkwe was so weak na he had coughs na kwakua hawez kukohoa had kutema makohozi alipewa dawa ambayo itamsaidia makohozi yatoke hata kama naiaa akwa kutapika..... ukweli mida ya asbh akatapika and mimi kwa kuona hilo i had to wash him manake he puke all over the bed and things were mess, kilichotokea sasa grandy ma akaanza bora yake na mwenzangu ana mtu hata wa kumwogesha mimi sijui kwenye uzee wangu kama nitampata wa kuniogesha she is 80+ now lkn ana complain hana mtu wa kumsaidia.

ukweli nilikasirika manake niliona hivi haoni kama mumewe anaumia hata kwa kuogeshwa kwa mjukuu wa kike yeye anaona anapata raha tuu, bibi yuko stable kiasi kwamba she can manage taking care of herself babu yeye hawez jamani anahitaj hata mtu wa kumlisha.

the worse thing babu yuko kwenye stage ambayo hata mfanyakazi wa kumuhudumia unaona tabu manake who will be ready ku mwogesha, kumfulia, kumtawaza kumlisha kila siku hata kama analipwa hela?? inabidi sisi wajukuu ndo tufanye hivyo sasa na penyewe bado bibi analalamika hafanyiwi khaaa!!!

I feel your pain sister. Ila ndio kama nilivyokwambia, chukulia kwamba ni uzee tu unamsumbua. Ingawa pia naanza kupata picha kuwa huyo bibi yenu ni mtu aina hiyo, yaani ni mtu ambaye hawezi kuridhika hata ufanye kitu gani. Trust me kwa mtu wa aina ya bibi yenu atapata cha kusema hata kama wote wawili wangekuwa wanapata kila kitu sawa. Sasa sisy mtu wa hivyo ni kama hakuna unachoweza kufanya ukizingatia na umri. Mimi nadhani, akilalamika haogeshwi unaweza kumwambia bibi usijali, nitakuogesha mara moja moja na wewe na hapo tegemea atatoa lalamiko jingine.

Mzoee tu hakuna namna.
 
ni kweli ugonjwa unachangia lkn hivi kweli ina maana huwa hawaoni kwamba wanakera??

unajua my dear ili mtu akuihudumie kwa upendo unapaswa na wewe uwe sehem ya hiyo huduma like uwe na moyo safi wa shukran na upendo na kuridhika sasa wewe kama haya yote huna na anayejitahd kukuonyesha upendo na ukarimu anafanya tena zaid unafkiri atajiskiaje??

Maskini I think its something they cannot control.

Mie bwana ma mkwe kila siku ananipa kesi za bibi. Alie weeeee.

Bibi yuo freshi mno. She trylu appreciates kila anachofanyiwa but sielewi tatizo liko wapi.

Hamna alie bedridden. Hata bibi anaenda washroom mwenyewe, anapenda kuoga na sio demanding sema wiki ikipita bila kuku mtanuniwa ukoo mzima.

Mbona mtatuma hata kwa tigo pesa??

But mimi ni muoga kweli wa ku react. I try my best kuwachukulia walivyo na kumuomba Mungu awajaalie wepesi na mie anijaalie nguvu ya kuishi nao.
 
Ujue hata sisi tunaowalea ni binadamu, kwa hyo wakilalamika hata kidogo kiasi fulani tunaweza kukwazika. Na kwa sababu inawezekana ninyi hamjadili na wasumbufu kuliko huyo bibi yenu basi mnaona ni msumbufu. Ila kwa uzoefu nilionao mimi, huyo bibi yenu ni super cool yaani. Kuku na hela za kutumia hapa na pale sio ishu sana.
 
Back
Top Bottom