Jukwaa la siasa lahitaji uvumilivu kama ilivyo siasa yenyewe!
Kuna majukwaa mengine pia hayaingiliki kama la international, dini na celebreties.
International limevamiwa na watu wa dini kila utachoandika kinapindishwa na kuwa na mlengo wa dini mwisho wake kashfa na matusi ya kidini huanzia hapo.
Celebrities bana kumekaa kiumbea umbea kiasi mtu anasemwa hovyo then unakuta huyo mtu ni nduguyo au rafikiyo unamjua vizuri lakini yanyozungumzwa ni uongo uliopitiliza na watu wanashadadia kwelikweli na unakuta yanayozungumzwa ni tetesi! Waambie walete evidence uone unavyovamiwa na michambo ya haja!! Ban nje nje
Jukwaa la dini si jukwaa la kujifunza tena, ukiingia kule ukitoka kichwa kinauma!! Ukitaka ban ingia jukwaa la dini haipiti hata sekunde unakula kama tano hivi...!! Tatizo ni kukashfiana na kutukanana, multiple ID zimejaa kule! Mtu anapigwa ban anaingia na ingine anasongesha mashambulizi hahaaaa!
Ukipita majukwaa hayo kama una hasira za karibu soma na ujondokee kimyakimya