Kukunja kushoto kwenye Mataa

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,338
2,000
Mfano mzuri ni kona ya Barabara ya Bibi Titi Mohamed na Mtaa wa Maktaba ukiwa unatokea Mwenge. Mfano mwingine ni TAZARA kama unatoka mjini kukata kona ya kushoto kuingia Barabara ya Mandela. Utakuta madereva wanaogopa kukata kushoto kwa vile watakamatwa.

Pana sababu zipi wakamatwe?
 
Mmassy JM

JF-Expert Member
Jul 30, 2020
831
1,000
Hapo left turn iliruhusiwa ila imezuiliwa makusudi ili kuepuka jam. Kwamba wakiruhusu left turn jam inaongezeka. Kwa hiyo inamlazimu dereva apitilize halafu aende kugeuzia mbele halafu arudi then akate kulia.

Sheria Kama hii ipo Mataa ya Magomeni ambapo gari zikitoka mjin kwenda Morocco haziruhusiwi kukata kulia. Wanapitiliza na kugeuzia mbele.

Kwingine ni mbezi mwisho kwenda goba Kama unatoka kimara unakata kushoto then unaingia round about then unaenda goba.

Nyingine ni mataa ya fire
 
GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
1,572
2,000
Inaelekea wengi hawajapita kozi ya udereva au ni kutokujua, kunakopelekea kuogopa kukamatwa!.

Kwa maelezo uliyoyatoa kwenye maeneo hayo, ni ruksa kukata kona ya kushoto kwenye makutano hayo hata kama hakuna taa ya kuongozea.

Mahali hapo uamuzi uko kwa dereva kuendelea na safari huku akitoa kipaumbele kwa watembea kwa miguu tu. Kama hakuna anayevuka, ni ruksa kuendelea na safari na pale ufikapo barabara kuu baada ya kuvuka pundamilia, kama hakuna gari inayokuja upande wa kulia unajiunga na msafara.
 
Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,338
2,000
Hakuna sababu ni vile tu traffic police wanajifanya hawaelewi wanatumia hiyo ishu Kama fimbo ya kuwachapia wenye magari.

Left turn sio lazima ungoje taa as long as umejiridhisha ni salama kwenda

Wapi left turn imezuiliwa?

Hapo left turn iliruhusiwa ila imezuiliwa makusudi ili kuepuka jam. Kwamba wakiruhusu left turn jam inaongezeka. Kwa hiyo inamlazimu dereva apitilize halafu aende kugeuzia mbele halafu arudi then akate kulia.

Sheria Kama hii ipo Mataa ya Magomeni ambapo gari zikitoka mjin kwenda Morocco haziruhusiwi kukata kulia. Wanapitiliza na kugeuzia mbele.

Kwingine ni mbezi mwisho kwenda goba Kama unatoka kimara unakata kushoto then unaingia round about then unaenda goba.

Nyingine ni mataa ya fire

Kukata kona kwenda kulia ni sawa kukizuiliwa, kwa vile pana magari yanayokuja opposite direction. Lakini kwa upande wa kushoto, hakuna ulazima kwa vile TZ magari hupita kushoto mwa barabara.

Inaelekea wengi hawajapita kozi ya udereva au ni kutokujua, kunakopelekea kuogopa kukamatwa!.

Kwa maelezo uliyoyatoa kwenye maeneo hayo, ni ruksa kukata kona ya kushoto kwenye makutano hayo hata kama hakuna taa ya kuongozea.

Mahali hapo uamuzi uko kwa dereva kuendelea na safari huku akitoa kipaumbele kwa watembea kwa miguu tu. Kama hakuna anayevuka, ni ruksa kuendelea na safari na pale ufikapo barabara kuu baada ya kuvuka pundamilia, kama hakuna gari inayokuja upande wa kulia unajiunga na msafara.

Hata kama sheria unaijua, kitendo cha Trafiki kusumbua magari yanayokunja kushoto, kunasababisha upotevu wa muda usio na ulazima. Kwa mfano TAZARA, kama unatokea mjini, imewekwa kabisa nafasi ya kupita kwa anayekunja kushoto, na halafu akasubiri mpaka iwe salama kuingia kwenye njia kuu, bila kujali taa. Hali kadhalika ukitokea uwanja wa taifa kwenda uwanja wa ndege.
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,648
2,000
Hapo left turn iliruhusiwa ila imezuiliwa makusudi ili kuepuka jam. Kwamba wakiruhusu left turn jam inaongezeka. Kwa hiyo inamlazimu dereva apitilize halafu aende kugeuzia mbele halafu arudi then akate kulia.

Sheria Kama hii ipo Mataa ya Magomeni ambapo gari zikitoka mjin kwenda Morocco haziruhusiwi kukata kulia. Wanapitiliza na kugeuzia mbele.

Kwingine ni mbezi mwisho kwenda goba Kama unatoka kimara unakata kushoto then unaingia round about then unaenda goba.

Nyingine ni mataa ya fire
Maelezo yako ni mazuri na sahihi kabisa. Lakini ukifanya hivyo unakamatwa na unaandikiwa faini au utoe rushwa! Siri iliyowazi ni kwamba askari wa usalama barabarani wanalazimisha makosa kwa madereva ili wawatoe pesa za rushwa
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
40,646
2,000
Hao ni Aina ya Askari wanaolazimisha makosa. Kama hamna taa hapo kwenye kona unaweza kupita kwasababu ukisema usimame hamna Pia taa ya kukuruhusu upite hapo kwenye kona.

Mfano ukitokea Selander bridge kwenda Obama avenue kuna taa ya kukuruhusu au kukusimamisha kwenye kona(zamani haikuwepo ilikuwa ruksa kupita)

Bibi titi kuingia Ohio street inakubidi ufuate taa, Bibi titi kuingia Azikiwe unaruhusiwa kupita hamna taa pale.
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,648
2,000
....kosa lake ni TZS 60,00.... nilitakiwa nisubiri hadi taa ya kijani iwake upande wetu ndipo niende kushoto
Huo ni uonevu na kama vyombo vya kupambana na rushwa vingekua makini na serious katika majukumu yao wangelishughulikia na hilo pia
 
Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
1,356
2,000
Sijaelewa hapa...Mfano mwingine ni TAZARA kama unatoka mjini kukata kona ya kushoto kuingia Barabara ya Mandela.
 
skfull

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
2,588
2,000
Wapi left turn imezuiliwa?Kukata kona kwenda kulia ni sawa kukizuiliwa, kwa vile pana magari yanayokuja opposite direction. Lakini kwa upande wa kushoto, hakuna ulazima kwa vile TZ magari hupita kushoto mwa barabara.

Hata kama sheria unaijua, kitendo cha Trafiki kusumbua magari yanayokunja kushoto, kunasababisha upotevu wa muda usio na ulazima. Kwa mfano TAZARA, kama unatokea mjini, imewekwa kabisa nafasi ya kupita kwa anayekunja kushoto, na halafu akasubiri mpaka iwe salama kuingia kwenye njia kuu, bila kujali taa. Hali kadhalika ukitokea uwanja wa taifa kwenda uwanja wa ndege.
Kuna sehemu zimezui mkuu kwa mfano ukitokea kamata hapa mataa ya kuingia manazi makutano ya lumumba kwa kumsaidia asiejua kama sehemu unataka kuingia upande wa kushoto kwenye makutana angalia upande wako wa kushoto ukiona taa ifuate ila kama iko upande wa kulia pekee hiyo haikuhusu kuna sehemu zinakuepo taa upande wa kushoto na kulia kwenye mchepuko wa kushoto kusho inakuhusu wewe na ya kulia kwako inamhusu aaliepo upande wako wa kulia,, tunaelekezana na kukumbushana,, Ni sawa na kibao kimechorwa mshale wa kwenda kulia halafu kikakatwa halafu hapo kilipo nyuma yake kabla hujakikuta kuna mchepuko wa kwenda upande wako wa kulia utafanyaje? Jibu Ni hivi kile kibao hakikuhusu kama kingekuhusu kingeka nyuma kidogo kabla ya kufikia mchepuko wako,, mfano mzuri kwa wale waliopita Barabara ya vingunguti mataa kuelekea viwandani,, ukiwa unatokea viwandani ili uingi njia kuu ya kwenda airport kuna hicho kibao,, Sasa Askari wa usalama Barabarani walikuwa wanatumia udhaifu wa uelelwa wa madereva kila anafuata uelekeo wa kulia pale kabla ya main road anakula cheti,,, nikaja huko sijui hili wala lile nikaambiwa weka pembeni halafu kwa ukali mpaka nikapata hofu kuwa kuna nini au nimeumiza mtu huko bila kujua ila nikakumbuka nipo sawa,, nikaweka gari pembeni akaja mmoja akaanza naomba leseni yako nikamuonyesha akataka kuichukua nikarudisha nyuma nikaamwambia kwanza niambie kuna nini maana hiyo simamisha sio ya kwaida tuloizoea akaniambia nipe leseni nikuandikie usinipotezee muda huoni wenzako wanaandikiwa hawana ubishi niwaelewa wanajitambua, kidogo nakapata donge la hasira nikamwambia kwa hiyo mimi sio muelewa okay nipe sababu za kuhitaji kuniandikia wakati hujanikagua akasema hujaona kibao pale kinakuzuia kuingia kulia nika mwamba sasa nimeellewa kuwa wewe ndiyo sio muelewa na wanaondikiwa ni wapumbavu Mimi si miongoni mwao,, na ili uendelee kufanya hivi niache niende,, akawa mbogo nikaangalia kwa upande wa pili nikamuona boss wake wa nyota mbili nikashuka nikamfuata nikamuomba tumsogelee yule askari hakuwa mbishi kufika nikamwambia nimeambiwa natakiwa kukuandikiwa faini ila kosa langu bado halijadhirika kuwa linastahili faini akaniuliza kosa gani nikamwambia silijui akacheka kidogo akamgeukia yule bwana akamuuliza kuna nini akamwelezea akaniambia umeelewa nikamwambia hapana naomba tusogee pale tukasogea pale nikaanza kumwelezea na mwisho nikamwambia hiki kibao kina mkataza mtu anaeingia main road kufuata muelekeo wa kulia akaniambia na huu mchepuko vipi nikamwambia kama ingehusika ingelazimu kuwa na vibao viwili cha nyuma na cha mbele au kimoja cha nyuma chenye amri wakilishi mbili niliachwa nikaondoka sikuwahi kuwaona tena pale na wakiwepo wana fanya mambo mengine au kama wanafanya hivyo ni kosa ila madereva wengi uoga hawajikubali hata kidogo yaani shule usome wewe halafu unapelekwa tu kama mzigo ni hatari madereva tujitahini kusoma alama na kuzielewa na tafsiri zake vema bila kusahau kufuata kanuni na sheria za usalama Barabarani Askari asikutoe ufahamu wako kwa mikwala yake tuendesheni magari kwa umakini turudishe heshima ya Dereva
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,768
2,000
Mimi huwa na solution moja napita huku nimewasha hazard tick tock tick tock pyuuui moto napita.Wakinisimamisha nawaambiaga afande ujaona taadhari niliokuwekea. Wanacheka mama pita .Nawewe Tumia techniques za kwenye gari za kuwasha taa ya dharura.Mimi hata nikiona nimepita mataa ghafla taa zikawaka red .Hazard nawasha na moto wangu.
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
49,809

Unajitafutia ajali tu kwanini hupite kwenye red

Ova
 
Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
18,719
2,000
Mimi huwa na solution moja napita huku nimewasha hazard tick tock tick tock pyuuui moto napita.Wakinisimamisha nawaambiaga afande ujaona taadhari niliokuwekea. Wanacheka mama pita .Nawewe Tumia techniques za kwenye gari za kuwasha taa ya dharura.Mimi hata nikiona nimepita mataa ghafla taa zikawaka red .Hazard nawasha na moto wangu.
Hakuna Camera ?La sivyo nchi zingine utakuta tu fine imetumwa kwenye box lako la barua. Ukifanya hivyo unakuwa flashed.Maana taa za Hazard nazo haziwashwi hovyo hovyo.
 
Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
27,102
2,000
Inategemea na barabara, kuna barabara ukikunja kushoto zipo taa ni lazima uzifuate, au kama njia unayotaka kuingia ina lane moja hapo lazima uchukue tahadhari.

Junction ya Uhuru-Lumumba kuna taa, lazima uifuate ikiruhusu ndio upite, junction ya morogoro-fire kuelekea muhimbili kuna taa, lazima uifuate, zipo nyingi tu so kama huna uhakika ni heri kusubiri kuliko kusumbuana na hawa ndezi.
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,768
2,000
Hakuna Camera ?La sivyo nchi zingine utakuta tu fine imetumwa kwenye box lako la barua. Ukifanya hivyo unakuwa flashed.Maana taa za Hazard nazo haziwashwi hovyo hovyo.
Haaaa kwa kweli sasa unakuta traffic yeye anajua hazard ni inashida au gari lina shida kwahiyo akikwambia kwa nini umewasha nilishamwambia gari imeanza kutetemeka nimeogopa nikisimama tu litazima katikati ya barabara.Naniliposimama nilizima jumla.so akaona kweli ungetupa shida na nyie akina mama mgetupa kazi ya kuliondoa haaaa
 
me1

JF-Expert Member
Jan 24, 2015
310
500
Ni muhimu kuwafikiria watembea kwa miguu pia, wakati mwingine taa nyekundu inapowaka kwa left turn, taa ya watembea kwa miguu inawaruhusu wavuke mahali hapo hapo
 
Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,338
2,000
Sijaelewa hapa...Mfano mwingine ni TAZARA kama unatoka mjini kukata kona ya kushoto kuingia Barabara ya Mandela.

Pale utakuta baadhi ya madereva wanaogopa kukunja kushoto, wakati taa zimewaka nyekundu, ambazo kwa maoni yangu, haziwahusu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom