sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,029
- 5,259
Kufuatia kuibuliwa mahakamani kwa barua ambayo inadaiwa iliandikwa na Job Ndugai aliyekuwa spika wa bunge kwenda kwa Katibu wa Bunge ikimtaarifu kuwa anajiuzulu uspika kuanzia tarehe 06.01.2022, bunge la JMT limefuta taarifa kwa umma iliyozitoa tarehe 07.01.2022 kukiri kupokea nakala ya Barua ya kujiuzulu iliyoawasilishwa na Job Ndugai kwenda kwa Katibu Mkuu wa CCM.
Pia taarifa nyingine kwa umma ilikuwa ikiwataarifu wabunge kuwa shughuli zote za bunge zinasimama mpaka pale atakapochaguliwa Spika wa Bunge. Taarifa zotehizo ziliwekwa katika tovuti ya bunge yaani parliament.go.tz na pia katika ukurasa wa twitter wa bunge la JMT utumiao jina la bunge_tz .
Barua hiyo ya Ndugai kwenda kwa Katibu wa Bunge iliibuliwa katika Lesi ya kikatiba Na. 02 ya 2022 iliyokuwa Mahakama kuu ya Tanzania - Dar es Salaam ambayo nayo imetupiliwa mbali leo tarehe 28.01.2022 kwa kuonekana haina mashiko.
Taarifa walizofuta ni kama zinavyoonekana hapa chini kabla hawajazifuta kwenye twitter account. Unaweza kuthibitisha kwa kubonyeza hapa