Kujiuzulu kwa Ndugai: Bunge ladaiwa kufuta taarifa kwa umma ilizochapisha katika tovuti yake na ukurasa wake wa Twitter

Noma sana !
Mimi sijui mfumo wa hizi machine za kisasa yaani computer! Je wamefuta kwa maana ya kufuta kwenye kioo au wamefuta kwa maana ya kuondoa ndani ya computer zao? NA KAMA ilinakiliwa na kuhifadhiwa na mtu mwingine, hapo mwongo ni nani?
 
Mimi sijui mfumo wa hizi machine za kisasa yaani computer! Je wamefuta kwa maana ya kufuta kwenye kioo au wamefuta kwa maana ya kuondoa ndani ya computer zao? NA KAMA ilinakiliwa na kuhifadhiwa na mtu mwingine, hapo mwongo ni nani?
Kamanda usituletee ujuaji hapa, kufuta kwenye kioo unamaana gani hasa?
 
Unamkumbuka Leo Lwekamwa?
Alikuwa Chairman wa TLP kabla ya Lyatonga

Kwny Mkutano wa hadhara pale Jangwani wakati wa Mkapa alisema hivyo akaichukua katiba akaikanyaga kanyaga pale Jukwaani

Aligombaniwa kama mpira wa kona na dola
Katiba ya nchi hii ni kama gazeti la kufungia maandazi!
 

Kufuatia kuibuliwa mahakamani kwa barua ambayo inadaiwa iliandikwa na Job Ndugai aliyekuwa spika wa bunge kwenda kwa Katibu wa Bunge ikimtaarifu kuwa anajiuzulu uspika kuanzia tarehe 06.01.2022, bunge la JMT limefuta taarifa kwa umma iliyozitoa tarehe 07.01.2022 kukiri kupokea nakala ya Barua ya kujiuzulu iliyoawasilishwa na Job Ndugai kwenda kwa Katibu Mkuu wa CCM.

Pia taarifa nyingine kwa umma ilikuwa ikiwataarifu wabunge kuwa shughuli zote za bunge zinasimama mpaka pale atakapochaguliwa Spika wa Bunge. Taarifa zotehizo ziliwekwa katika tovuti ya bunge yaani parliament.go.tz na pia katika ukurasa wa twitter wa bunge la JMT utumiao jina la bunge_tz .

Barua hiyo ya Ndugai kwenda kwa Katibu wa Bunge iliibuliwa katika Lesi ya kikatiba Na. 02 ya 2022 iliyokuwa Mahakama kuu ya Tanzania - Dar es Salaam ambayo nayo imetupiliwa mbali leo tarehe 28.01.2022 kwa kuonekana haina mashiko.

Taarifa walizofuta ni kama zinavyoonekana hapa chini kabla hawajazifuta kwenye twitter account. Unaweza kuthibitisha kwa kubonyeza hapa


View attachment 2098310

View attachment 2098311
 
Kiukweli hii nchi tumekaa kishamba sana.

Inaakuwaje mtu anajiuzuru bila kufata utaratibu?

Hata hivyo basi, Inakuwaje mtu anajiuzuru bila kuandika sababu ya kujiuzuru?

Vizazi vijavyo vitakuta historia gani?

Naomba Barua iandikwe upya.
Serikali iliyopo iliingi madarakani kwa njia za udanganyifu, hatushangai kuona inaendelea kufanya udanganyifu katika kila kitu
 
Back
Top Bottom