Kujiuzulu kwa Ndugai: Bunge ladaiwa kufuta taarifa kwa umma ilizochapisha katika tovuti yake na ukurasa wake wa Twitter

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
2,993
5,210
Kufuatia kuibuliwa mahakamani kwa barua ambayo inadaiwa iliandikwa na Job Ndugai aliyekuwa spika wa bunge kwenda kwa Katibu wa Bunge ikimtaarifu kuwa anajiuzulu uspika kuanzia tarehe 06.01.2022, bunge la JMT limefuta taarifa kwa umma iliyozitoa tarehe 07.01.2022 kukiri kupokea nakala ya Barua ya kujiuzulu iliyoawasilishwa na Job Ndugai kwenda kwa Katibu Mkuu wa CCM.

Pia taarifa nyingine kwa umma ilikuwa ikiwataarifu wabunge kuwa shughuli zote za bunge zinasimama mpaka pale atakapochaguliwa Spika wa Bunge. Taarifa zotehizo ziliwekwa katika tovuti ya bunge yaani parliament.go.tz na pia katika ukurasa wa twitter wa bunge la JMT utumiao jina la bunge_tz .

Barua hiyo ya Ndugai kwenda kwa Katibu wa Bunge iliibuliwa katika Lesi ya kikatiba Na. 02 ya 2022 iliyokuwa Mahakama kuu ya Tanzania - Dar es Salaam ambayo nayo imetupiliwa mbali leo tarehe 28.01.2022 kwa kuonekana haina mashiko.

Taarifa walizofuta ni kama zinavyoonekana hapa chini kabla hawajazifuta kwenye twitter account. Unaweza kuthibitisha kwa kubonyeza hapa

Screenshot_20220128-125335_Chrome.jpg

Screenshot_20220128-125346_Chrome.jpg
 
Wamefuta kwa kuwa taratibu zilikiukwa na kinyume na Katiba. Kwa nini Katibu wa Bunge na mwanasheria Mkuu wa Serikali awakushauri utaratibu sahihi na kumtaka Ndugai aelekeze barua yake kwa Katibu wa Bunge. Au Ndugai alifanya makusudi ili kutengeneza mgogoro wa kikatiba!!!?
 
Unajua ndio kipimo cha watu wanao tuongoza, hajafanya makusudi ila ni kwamba hajui utaratibu.
 
Kuna sheria wali pitisha za kutokushtakiwa wakistaafu, sasa mtu una jiuliza una ogopa nini?
 
Kiukweli hii nchi tumekaa kishamba sana.

Inaakuwaje mtu anajiuzuru bila kufata utaratibu?

Hata hivyo basi, Inakuwaje mtu anajiuzuru bila kuandika sababu ya kujiuzuru?

Vizazi vijavyo vitakuta historia gani?

Naomba Barua iandikwe upya.
 
Kufuatia kuibuliwa mahakamani kwa barua ambayo inadaiwa iliandikwa na Job Ndugai aliyekuwa spika wa bunge kwenda kwa Katibu wa Bunge ikimtaarifu kuwa anajiuzulu uspika kuanzia tarehe 06.01.2022...
Noma sana !
 
Katiba ya nchi hii ni kama gazeti la kufungia maandazi!
Mkuu katiba ipo poa kwa baadhi ya segments tatizo linakuja kwa baadhi ya wanaobanwa na hiyo katiba ndiyo wanaisigina na kuonekana haina maana. Mfano issue ya Job katiba ipo wazi but kuna kundi linajiaminisha kuwa na nguvu kuliko katiba huku wnanchi tumeiacha katiba ijitetee yenyewe wakati sisi wananchi ndiyo wenye kuitetea kwa nguvu zote.
 
Ni kweli,ndio maana nikasema ni Katiba nchi hii ni kama gazeti la kufungia maandazi!Yaani wanaikunja na kuisigina watakavyo!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom