Hivi hawa mabwana (TISS) hawana wavuti?
Kutotangazwa kwa nafasi za TISS ni u pu u z i! Hizi nafasi za kazi zinazotakiwa ziwe wazi kwa kila MTZ na sifa ziwe zinajulikana!
FBI na CIA wanatangaza wazi nafasi zao kwa wa Marekani why not Tanzania?
watu wapo wapo tu,watu wenye uwezo wapo tu,wasiotaka maSLAHI MBELE ZAIDI WAPO.labda nikupe mfano mm nna rafiki yangu ambaye tangu msingi alikua na hulka na mkakamavu,mkimbia riadha,mrusha tufe jasiri,anatii anachoagizwa sio anaongeza na yako,anajua mipaka yake na hana utashi binafsi kwenye maslahi ya kazi,yupo huko hakufaulu shule kubwa ila alikwenda shule za kawaida,sasa ana degree km nne na anaruka ndani na nje ya nchi km unapotoka dar kwenda moshi.Mkuu,
Mawazo yako ni mazuri sana,
Ila nina swali je, nchi itapataje watu wa kufanya hii kazi kama wewe utatoa nasaha kama hivyo!?
Baada ya kusoma kitabu cha E. Chahali SHUSHUSHU......nimejifunza mengi sana sasa..hata hilo swali nililouliza hapo mwanzo nimepata jibu lake.Haaa haaa Haaa haaa teeeh teeeh.
Mkuu,
Nenda pale , Magogoni au ukiona rais siku anahutubia mahala popote pale wewe waendee wale jamaa walio huku karibu na wananchi wenye viwaya masikioni kisha waombe utapewa anuwani ya wavuti yao mubashara kabisa bila chengachenga.
Baada ya kusoma kitabu cha E. Chahali SHUSHUSHU......nimejifunza mengi sana sasa..hata hilo swali nililouliza hapo mwanzo nimepata jibu lake.
Nadhani kibiti itasaidia kuwanoa tena wana itelijensia maana ni aibuUmefanikiwa kupata?
Yaani mpaka hapo hiyo kazi sahau tafuta kazi nyingine tuu.......hakuna kazi hapo.Umofia kwenu wanajukwaa. Mada hapo juu yahusika. Nimekuwa nikihangaika kujiunga na Idara hii nyeti ya Taifa tangu mwaka 2014. Nilianzia mkoani kwetu kwa kuonana na Ofisa usalama wa Taifa mkoa ambaye alinihoji ofisini kwake kwa muda na baadae kufurahishwa na Mimi kuipenda kazi yao na kunielekeza nikaanzie wilayani kwetu. Nilifanya hivyo kwa kukutana Ofisa usalama wa Taifa wilaya ambaye baada ya maongezi tuliachiana namba za Simu kuwa atanitafuta nafasi zikitoka. Kila nikimpigia simu anasema hakuna nafasi zilizotangazwa makao makuu Taifa kuja wilayani. Tumeendelea kuwasiliana lakini majibu hayohayo. Mimi nimekuwa nikitaka kujiunga na Idara hii nyeti tangu nikiwa mtoto. Sasa naona ndoto yangu inapotea. Mwenye kujua jinsi ya kujiunga anielekeze kwani nimepoteza tumaini na ofisa huyu wilayani. Mbona majeshi mengine nafasi zinatoka na watu wanajiunga? Karibuni kwa ushauri na maelekezo. Natanguliza asante kwenu.