SoC03 Kujiajiri vijana inahitaji mabadiliko ya mfumo wa elimu nchini

Stories of Change - 2023 Competition

Milesmontego

New Member
Jul 16, 2023
2
0
Kujiajiri vijana inamanisha vijana waliohitimu vyuoni waanzishe kazi au biashara zao wenyewe kutokana na elimu waliyonayo au waliopata vyuoni.

Kwa maoni yangu hili ni wazo zuri saana lakini linahitaji wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni wapate kusoma na kufanya vitu ambavyo kiuhalisia vipo katika jamii tangu wanapokua na umri kuanzia miaka 17 ili kuepuka kusoma kwa nadharia na baadae kuja kufanya kazi kwenye uhalisia katika maisha ya kila siku ambapo kuna changamoto nyingi.

Kwa fikra zangu ili kuwawezesha vijana kujiajiri yafuatayo ni muhimu kuzingatiwa;

ELIMU KWA VITENDO, Kwenye mambo ambayo yanatusumbua vijana wengi tuliosoma ni hili, wakati tukiwa shuleni muda mwingi tunasoma kwenye vitabu kwamba kitu hiki kinatengenezwa namna hii au kama kuona basi kuona tu muundo wa namna kifaa flani kinavyotengenezwa lakini ukifika kwenye kifaa chenyewe unakuta ni tofauti kabisa, sasa ili kuhama kutoka kuajiriwa kwenda kujiajiri kwanini serikali isiwekeze kwenye elimu kwa kuleta uhalisia halisi kwenye elimu mifano kama ni kujifunza namna transformer inavofanya kwenye redio wanafunzi waletewe redio apo waone transformer na wazisuke wenyewe na kuunganisha apo mtoto anaweza kujifunza kuhusu capacitor, resistor na namna ya kuziunganisha na hata baada ya kuhitimu masomo yake walau ata kidato cha nne anaweza kua fundi redio, simu hata tv bila kusubiri ajina.

ELIMU YA KUJITEGEMEA, Kwenye shule nyingi watoto wanalima mashamba ya shule lakini hawajifunzi ni namna gani ya kuzalisha mazao mengi na mwisho unakuta hata shule wanalima kilimo cha kawaida cha mazoea na wanafunzi wanaona kilimo hakina faida, wanafunzi wanalisha mifugo ya shule lakini wakati wanasoma ufugaji wanaishia darasani tu kwanini wasifundishwe kua ufugaji wa namna hii ndio wenye faida hivyo waanze ufugaji hapo shuleni kwa ile njia ambayo inatoa mazao mengi na faida kubwa ili wakutane na hizo changamoto ili wajue namna ya kutatua changamoto na kupata mavuno makubwa hii itawafanya vijana au wanafunzi wanaohitimu kuendeleza ufugaji wenye tija na hata bila kusubiri ajira, kama ni ufugaji wa kuku ambao mtu anaweza kuanza na mtaji mdogo mwanafunzi ajifunze kwa vitendo njia nzur ya kuzalisha vifaranga wengi kwa wakati mmoja na kuwakuza kwa kifupi somo la stadi za kazi ndio muhim kwenye kuwezesha vijana kujiajiri.

Haya yote yafundishwe darasani na kwa vitendo liwepo shamba la shule kufundishia kilimo na ufugaji na watendaji wakuu wawe wanafunzi wakitazama njia bora za kilimo.

MASOMO YA UFUNDI KILA SHULE YAWEPO; Hii itasaidia vijana wanaohitimu masomo yao waweze kujiajiri Kwenye ujenzi kupaua, technolojia,kupuka rangi na hata ufundi cherehani ambapo vijana wanaweza kujipatia kipato kikubwa hata kabla ya kuajiriwa.

MSINGI WA BIASHARA, biashara nyingi zinahitaji mtaji mkubwa kwa maoni yangu wanafunzi wangeruhusiwa kujihusisha na biashara ndogo ndogo wakati wanasoma na pia kuajiriwa kwa muda ambao sio wa masomo ili kuwatayarisha vijana hawa na maisha ya badae na wawe wanajua wanasoma ili kufikia malengo yao yakua na elimu fulani na kua na ujuzi fulani ila wasisome kwaajili ya ajira kwanamna hii wanafunzi wetu wanaweza kuajiriwa kwenye sanaa kulingana na vipaji vywao kama vile uchezaji mpira, usanii wa muziki, uchoraji pia hata uchongaji na ushonaji.

Kwa njia hizo hapo juu itakuwa rahisi kwa vijana wa Tanzania kujiajiri na hivyo kuondoa mgogoro wa ajira na hii itaimarisha uchumi wa nchi kwasababu kila kijana awe ameajiriwa au hajaajiriwa atakuwa anazalisha kitu na hakutakuwa na malumbano ya kwanini Serikali haitoi ajira za kutosha na pia pato la Serikali litaongezeka kwa kuongezeka vyanzo vya mapato.

Nchi ya namna hii itaimarisha uchumi kwasababu kila sekta itakua na wataalamu wazoefu ambao wanaweza kutumia uzoefu wao kuishauri serikali namna ya kuongeza vywanzo vya mapato kupitia sekta fulani.

Kwahiyo ile tuseme vijana wajiajiri ni muhimu kuwatengenezea mazingira rafiki na kwauhakika kama vijana wataandaliwa na kukuzwa kwenye mazingira ya kujiandaa kujitegemea au kujiajiri hakutakua na tatizo lolote lile ajira. Hivyo kujiajiri ni muhimu sana kwasababu ajira serikalini ni chache pia hata kwenye sekta binafsi.

Kwa kifupi kabisa vijana ni muhimu sana kujiajiri hatakama umeajiriwa inabidi ujiandae kujiajiri ili ajira isikufanye mtumwa wa mtu au viongozi waliopo serikalini na kutukanwa kwasababu mtu au taasisi imekuajiri, tunashuhudia waajiriwa wengi wakidhalilishwa na waajiri wao mfano mzuri viongozi wa serikali akifika kwenye taasisi anawafokea waajiriwa huku akiwatishia kuwafukuza kazi au kuwahamisha vituo huu ni utumwa tuukatae KABISA.

Ningependa kusisitiza zaidi na zaidi ajira nyingi nchini kwetu ni utumwa hakuna haki ya mwajiriwa kwasababu siku zote mwajiriwa anaogopa kufukuzwa kazi na mikataba ya kazi watu wanaikubali ili tu kupata ajira lakini mikataba mingi inakandamiza mwajiriwa mfano mzuri ni Feisal Salum ambapo timu yake ilikubali kuvunja mkataba kwasababu ya Mh rais lasivyo asingepata haki yake"VIJANA TUJIAJIRI ILA SERIKALI ITUWEKEE MAZINGIRA RAFIKI TANGU TUKIWA SHULENI" angalia video hii kutoka @djsniper


 
Back
Top Bottom