SoC03 Mapendekezo mapya ya elimu yakayoweza kusaidia kufikia soko la ajira nchini Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

jayboy

Member
May 26, 2023
19
15
Elimu ni maarifa na ujuzi anaokuwa mtu kuhusu jambo fulani, hivyo kusaidia katika kufanya kazi Fulani kwa ufanisi na matokeo ya kazi hiyo kuwezesha mtu kuinua hali yake ya kimaisha.

Elimu ni sekta muhimu katika kuzalisha wataalamu na wahudumu mbalimbali wenye ufanisi na stadi mbalimbali ambazo husaidia katika kuchangia uzalishaji wa bidhaa na huduma bora za kijamii katika nchi, hivyo basi ili nchi yoyote iweze kuendelea kijamii, kisiasa, kiuchumi na kitamaduni lazima iwekeze vyema katika sekta ya elimu ili kuzalisha wataalamu wa kutosha wataoweza kuhudumu katika nafasi mbalimbali za uzalishaji mali Kama vile shambani, viwandani, migodini, mahakani, jeshini, ofisini na sehemu nyingine.

Kwa nchi Tanzania elimu inayotolewa ni rasmi kwa sababu inafuata mitaala ya ifundishaji ya silabasi Kama nchi nyingine, hivyo kwa kiasi kikubwa inasaidia katika kuandaa wataalamu mbalimbali ambao wanahudumu katika nafasi Kama vile sheria,utabibu,utawala na uongozi, uhasibu, usimamizi wa mali za umma na binafsi pamoja na elimu yenyewe.

Hivi karibu ni kumekuwa na ongezeko kubwa la wataalamu ambao hawana ajira ,hivyo wamekuwa wakijitolea kufanyakazi katika taasisi mbalimbali za serikali na binasfi bila malipo yoyote hali ambayo inawakatisha tamaa wanafunzi kutoka vyuoni kutofanya vizuri katika masomo yao kutokana na kozi zao kutokuwa na solo katika ajira kwani wengi wao hukaa miaka mingi bila kuajiriwa yakribani miaka mitatu wakiwa wanasubiri ajira.

Kukosekana kwa ajira ni tatizo kubwa kwa nchi za Afrika na duniani kwa ujumla ,hali hii inawasukuma wasomi wengi kutupia lawama Serikali kushindwa kuwaajili kwa wakati na idadi yao ,katika kuliona hili Serikali imekuwa ikifanyamaborsho mbalimbali kuhusu elimu katika kuboresha elimu elimu ya Tanzania ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za sekta za elimu nchini, sekta ya elimu tangu uhuru hadi Leo imekuwa ikikabiliwa na changamoto Kama vile uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi, vitendea kazi, malimbikizo ya madeni kwa walimu na wafanyakazi, kuvuja kwa mitihani ya darasa la nne, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita hali ambayo huitia hasara Serikali katika kuandaa mitihani upya, walimu kuhama mara kwa mara vituo vya kazi,uhaba wa pesa za kuendeshea mikutano na vikao mbalimbali vya wataalamu wa elimu,uhaba wa shule zakutosha, maabala za kisasa na maktaba.

Kutokana na changamoto sekta ya elimu imekuwa ikipoteza ubora kila siku,wataalamu mbalimbali wa elimu wametoa mawazo yao juu ya changamoto ya elimu ya Tanzania ni kutokana na kuwekeza zaidi katika kumkaririsha mwanfunzi badala ya kumuelesha kujibu mitihani ili kumjengea uelewa wa kufanya kazi na kufikiria kwa umakini zaidi, vile vile kutumia njia za zamani mbadala ya kutumi njia za kisasa za kufundishia ili kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, muda mrefu wa mafunzo ambao unaonekana unapoteza muda mrefu wa kujifunza wakati kuna uwezokano wa kutumia muda mchache wa mafunzo na kuhitimu. Kupitia changamoto mbalimbali za elimu ya sasa wadau na wataalamu mbalimbali wamekuwa wakishauri serikali juu ya namna bora ya kulifikia solo la ajira nchini Kama ifuiatavyo;-

(I) Kupunguza muda wa masomo shuleni ili kupunguza muda mwingi wa kukaa shuleni ili kuwawezesha wanafunzi kujishughulisha katika kazi kazi za uzalishaji mali Kama vile ufugaji,kilimo,uvuvi,ulinaji asali na kazi nyinginezo,hali hii itawasaidia vijana wengi kujiajiri mapema na hivyo kuepukna na hali ya utegemezi kwa familia na jamii kwa ujumla, vijana wengi wanaomaliza chuo wamekuwategemezi kubwa kwa familia zao na serikali mpaka pale watakapo ajiriwa hali yakuwa wanauwezo wa kujiajiri wenyewe.

(II) Kuanzisha masomo ya ziada ya kujiajiri,ubunifu na stadi za maisha kwa vijana ili kuwezesha kubuni na kutengeneza vitu Mbali Mbali Kama vile viti,meza,stuli,viti na vitu vingine hali hii itasaidia kutengeneza ajira kwa vijana wenyewe Kupitia kubuni vitu mbalimbali ambavyo solo lake la ajira lipatikana hapa hapa.

(III) Kufanya utafiti juu ya miradi mbalimbali ya uweshaji kwa vijana ili kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi midogo na mikubwa ya uzalishaji mali katika jamii,vijana wanapaswa kutumia akili zao na maarifa yao yote katika kubuni mawazo chanya juu ya uwekezaji wa miradi na biashara katika maeneo ya mitao ya simu(trade online) ili kutafuta masoko ya uhakika nje.

(IV) Kuunga mkono jitihada mbalimbali za wataalamu wa uchumi kuhusu masuala ya masoko na ajira ili kuweza kujitathimini namna ya kuliteka soko la ajira na bidhaa kwa uhakika ili kufaidika vizuri watakapo jiajiria au kuajiriwa.

(V) Kuelekeza mafunzo ya kila elimu katika utendaji kazi na uzalishaji ili kuwaandaa vijana katika misingi mizuri ya kufanyakazi kwa ufanisi kazini na matokeo ya kazi hiyo kusaidia ukuaji wa sekta hiyo.

Katika kuweka mipango sawa ya upatikanaji wa masomo katika ajira serikali haina budi kutumia mbinu mbalimbali za utawala bora katika kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu Kama vile Afisa elimu wa wilaya, Afisa elimu wa mkoa, Makatibu elimu, Vyama vya walimu, Wizara ya elimu na wataalamu na wadu wa elimu katika kufanya tafiti mbalimbali kuhusu elimu na kutunga Sera mbalimbali za usimamizi wa mitihani ufundishaji na maelekezo mbalimbali ambayo husaidia Sana katika kuboresha huduma ya elimu nchi Tanzania katika sehemu za vijijini na mjini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom