Kuitwa Dkt kumekuwa fashion za kisiasa. Wananchi tunahitaji matokeo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,754
Najua Tanzania kuanzia wakati wa Kikwete imekuwa kama sifa kuwa na PHD hata kama ni za kupewa, kupendelewa au kununua. Kwa wanajua elimu huwezi na ni vigumu kuweza kupata PHD ya kweli wakati wewe ni waziri. Kuna mawili kama umepata PHD yako kama waziri kwanza inawezekana hufanyi kazi yako vizuri ya uwaziri au hufanyi utafiti wako vizuri wa PHD.

Ijulikane tu kwamba PHD miaka 2 ni ya utafiti na kupata PHD ni utafiti wa ugunduzi fulani sasa ni lazima uwe na muda wa kutosha wa kufanya tafiti na huwezi kukaa ofisini ukapata PHD ya ukweli. Kinachotokea Tanzania hizi reseach nyingi zinafanywa na hao hao walimu yaani Professors ndiyo wanafanya kazi na hawa waheshimiwa wanafundishwa tu zile reaseach na kupeteshwa. Kwa wale wanasiasa ambao wanaogopa hili wanatumia njia ya PHD za heshima.

Kiukweli kwenye siasa PHD yako inawezekana inasaidia kwa sasa lakini wananchi wakijua kwamba PHD ni tafiti tu na mara nyingi hazina uhusiano wowote na maisha ya kila siku watakuja kugundua kama wenzetu wa nchi zilizoendelea kwamba PHD yako sio chochote kwenye siasa. Mara nyingi wanaochukuwa PHD ni kwasababu ya kuwa walimu wa vyuo na kuwa watafiti kwenye kampuni. Kwenye tafiti nyingi za PHD unatakiwa kusoma vitabu 90 sasa ni wanasiasa wangapi tena wenye uongozi wanaweza kusoma vitabu 90?? .

Wananchi wanataka maendeleo na sio PHD hizi fake ambazo hazisaidii chochote zaidi ya kujikweza. Hata uncle wangu Magufuli ingawa alikuwa kipanga sana alipata PHD kwenye utafiti wa korosho lakini yeye ndiye kaharibu utaratibu na bei za korosho Tanzania huo ndiyo ukweli. Bashe ambaye ni streer smart ndiye anaenda kutafuta suluhu ya bei!! hii ina onyesha PHD na kubadilisha maisha ni vitu viwili tofauti

Tanzania tunahitaji viongozi ambao ni wabunifu, wachapa kazi, wasio wala rushwa na wanaojua jinsi ya uchumi wa mtaji unavyoenda. Sio hawa wabunge fake, wenye PHD fake na kuongoza demokrasia fake.
 
Ngoja nijitaidi kubeti siku nikimla mzungu naamini na mimi nitapewa Hiyo PHD🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom