Kuibiwa kwenye Daladala

Nimewahi kuibiwa mara mbili kwenye daladala, pamoja na kujifanya mtoto wa town wa jamaa wakikuotea utalia peke yako....
Siku ya kwanza , gari la Tandika - Muhimbili , nilitoka kukopa kwa mshikaji chuoni Tsh elfu 20, nikatumia elfu 2 ikabaki elfu 18, nipo kwenye gari naenda zangu saloon kupunguza nywele, nimeshuka pale bora nikaingia saloon vizuri nikanyoa, nadaiwa hela wallet sioni, wajanja wamesepa nayo....
Siku ya pili gari la Mbagala- Tandika, nilipigwa na usingizi wa nusu kaputi, tumefika mwisho nipo peke yangu kwenye gari, fedha, vitambulisho , passport size. Vyote vimeenda kichwa kiliuma, mara kizunguzungu ... usiombe yakukute
 
Aisee hela ya kukopa bado ikapigwaa daah....!!
 
ha ha haah daah huu uzi nimecheka sana,nahisi utakuwa mrefu sana,sibanduki,ngoja nijibanze hapa nicheke niongeze siku za kuishi,ila huyo aliyeibiwa na kuwekewa mche wa sabuni katisha kuliko wote!
Mi nlweka lotion
 
Umenikumbusha ka tecno kangu akilivyochapwa pale ubungo mawasiliano enzi bado mgeni mgeni.
Speaking of kuibiwa nilienda taifa kuangalia mechi kati ya gor mahia na everton na katiketi kangu ka vip ka elfu saba. Watu walikua wengi sana kiasi kwamba baada ya mechi kuanza excitement ya mechi ilikua kubwa maaskari wakashindwa ku control zile entry gates watu wakawa wanaingia free ..aisee mfukoni nina wallet na mfuko wa pili nina simu, wakati tunasukumana kuingia nikahisi mkono kwenye suruali yangu nikageuka fasta mtu wa kwanza kumkamata ni huyo huyo, Kombat karate nilizocheza Jkt zilifanya kazi pale nilimbinya jamaa kama dakika 10 hivi na maaskari wakiwa wanaona maana niliwaambia mi askari mwenzao JKT wanaidiss tu lakini kuna faida nyingi sana kupita huko maana ningerudi ghetto kwa miguu maana ilikua na laki moja na Ids zote ndani.
 
Duuk Kilo moja sio mchezoo
 
Kokoto kilo 2??? Mkuu unajua maana ya kokoto?
 
Mimi ilibaki kidogo teja anichomolee simu huku nagombania daladala maeneo ya mwenge. Machale yalinicheza kugeuka nyuma naona mtu kachomeka vidole kwenye mkoba nilimkata jicho alivyozuga nikabaki kucheka.
Kama nakujua vile unakaa Sinza au ?
 
Kosa ni hapo kuweka kwenye bahasha yao. Ukikomaa kuishika hivyo hivyo wanakurudishia hela yako
 
Walitaka kunitaimu pale ubungo kwenye foleni, siti za nyuma kwenye gari nlikua nimeweka laptop na power bank. Sasa sina hili wala lile na milango sijaloki, nashangaa anakuja dogo mmoja upande wangu anaanza kuniongelesha kumbe Kuna mwenzake nyuma anafungua mlango ili apige kituo. Kilichotokea ni moja ya matukio adhimu sana na kila nikikumbuka hua najisemea moyoni, "yes, I'm the man"
 
last time nmeibiwa ilikiwa ni 2015 mwanzoni... nilienda kkoo kununua laptop, nikapita bank nikachomoa kama 400k hivi... maana nilikuwa nataka nichukue laptop used, basi bhana...

Nikaenda duka la kwanza nikaangalia pale nikaona kuna lennovo moja jamaa anauza 400k, ila alinidanganya specs, nikamuona mzushi japo alisema angenifungia 4gb ram na hdd 500gb, lkn nikaona haina maana,

Nikaenda duka lingine nikatutana na toshiba moja hivi nikaipenda na jamaa alikuwa anaiuza 280k tu, basi nikaitest pale nikaona iko poa kabisa, nikatoa wallet yangu mfukoni nikalipia hela, baada ya hapo nadhani sikuirudisha ile wallet mfukoni nikaiacha palepale(maana vitu vingi huwa navisahau kwa mtindo huo...)

basi bhana... before sijaondoka, nijisachi... nikajikuta sina wallet na hela yote kama 121k ndo ilikuwa mle, plus kitambulisho cha chuo na bima ya afya,

ilipona tu kadi ya bank sababu baada ya kutoa hela sikuirudiaha kwenye wallet nikaiweka kwenye bag...

aisee hiyo siku nilitembea ya mguu kutoka kkoo mpaka mabibo maana kila atm ya crdb niliyokiwa napita nilikuwa nakuta haina hela au mtandao unasumbua....

baada ya hapo ikawa nikitembea na bulk cash basi lazima bag lihusike...
 
Aise ulifanyajee mkuu
 
Sasa si ungemkomalia anaeuza laptop yulee???
 
Sasa si ungemkomalia anaeuza laptop yulee???
dah, nilishindwa maana hata yeye mwenyewe alikuwa analalamika kwamba kuna mteja kampa aangalie laptop halafu huyu mteja haonekani... maana huyo muuzaji alikuwa anaingia ndani na kutoka....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…