Kuiba Trillion 2 halafu kesho yake unamwambia mtu lipa kodi kwa maendeleo ya taifa ni matusi, hii inauma sana

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,066
40,725
Kuna wakati leo nimekaa natafakari sana jinsi tunavyobanwa katika kila angle ili tulipe kodi, hasa hasa hili suala la tozo za miamala, linaumiza sana.

Halafu unakuja kuambiwa watu wanaiba pesa tulizolipa kodi, nasikia kuna hadi trillion 2 zimelambwa. Hapa nimetoka kutuma pesa haifiki hata laki 5, imeondoka karibu 7k makato tu ya ajabu ajabu, nimejikuta moyo unaniuma sana, yaani moyo unaniuma nyieee.

Rais tuliyempa dhamana ya kutulinda na kutuvusha salama hadi 2025 yupo na anaona na anasikia, the best she can do ni kusema ‘Stupid!’ basi? Madame president is that the best you can do?

You people up there Ikulu, who do you think you are? Hivi mnadhani mnaongoza nguruwe? Mnataka kitokee nini ndio mjue kuna watu wanapaswa kubadilishwa? Please, mi naumia sana, kweli naumia, hizo pesa zinaniuma mno!

Kulipa tozo hadi mnakamua watu damu, halafu mnaiba tu like nobody’s business, hakuna anaechukuliwa hatua, maana yake nini? Hii dharau ya aina gani hii, halafu mnatuambia mambo ya kulipa kodi? Kweli, what do you take as for?

Hivi kwani uwaziri ni jina la ukoo kwamba mtu hawezi kubadilishwa? Mnatukatisha tamaa. Kwani nyie viongozi wetu mnahitaji kuiba kiasi gani ndio mridhike? Si muwe mnaiba hata milion 100 then maisha yanaendelea, sasa kweli unaina trillion 2 halafu iweje? Makusanyo ya watu milioni 60 kwa muda wa miezi miwili wewe unachukua unatia mfukoni?

Mna mioyo ya chuma kwani jamani? Waoneeni huruma watoto wa binadamu wenzenu jamani, ibeni ila angalieni na urefu wa kamba, tuibe kwa huruma, kwani hamna dini nyie, yaani trillion 2 hata siamini. Yaani moyo unaumaa, hivi nyie Watanzania trillion 2 mnazichukukije kwani? Nchi zingine hai wahusika wangekuwa wananing’inia kwenye mti, mfano China huu ujinga huwezi kufanya.

Sasa nasemaje, hizo trillion 2 zirudi, otherwise 2025 tutaondoka na kichwa cha mtu, sisi sio nguruwe, ni binadamu!

484D1FE3-DC01-45BC-9FAC-3A020B9A2745.jpeg
 
Hii nchi hatuna Rais, suala la Karikaoo kimya mpaka sasa Rais hajasema kitu. Ripoti ya CAG kimya mpaka sasa.
Kila kitu ni kimya mzee...no, amepandisha dau, ananunua goli moja kwa 20m plus ndege litakalo wasubiri

WaTZ wanachukulia maisha serious sana, yeye alikuwa anasubiria zake uzinduzi...kila mtu ale kivyake, mtajua wenyewe
 
Kuna wakati leo nimekaa natafakari sana jinsi tunavyobanwa katika kila angle ili tulipe kodi, hasa hasa hili suala la tozo za miamala, linaumiza sana.

Halafu unakuja kuambiwa watu wanaiba pesa tulizolipa kodi, nasikia kuna hadi trillion 2 zimelambwa.
Hapa nimetoka kutuma pesa haifiki hata laki 5, imeondoka karibu 7k makato tu ya ajabu ajabu.., nimejikuta moyo unaniuma sana, yaani moyo unaniuma nyieee..

Rais tuliyempa dhamana ya kutulinda na kutuvusha salama hadi 2025 yupo na anaona na anasikia, the best she can do ni kusema ‘Stupid!’ basi?! Madame president is that the best you can do??!!!

You people up there Ikulu, who do you think you are? Hivi mnadhani mnaongoza nguruwe? Mnataka kitokee nini ndio mjue kuna watu wanapaswa kubadilishwa? Please, mi naumia sana.., kweli naumia.., hizo pesa zinaniuma mno!

Kulipa tozo hadi mnakamua watu damu, halafu mnaiba tu like nobody’s business, hakuna anaechukuliwa hatua.., maana yake nini,?! Hii dharau ya aina gani hii.., halafu mnabana pua kutuambia mambo ya kulipa kodi?, kweli, what do you take as for..,

Hivi kwani uwaziri ni jina la ukoo kwamba mtu hawezi kubadilishwa? Mnatukatisha tamaa. Kwani nyie viongozi wetu mnahitaji kuiba kiasi gani ndio mridhike? Si muwe mnaiba hata milion 100 then maisha yanaendelea, sasa kweli unaina trillion 2 halafu iweje? Makusanyo ya watu milioni 60 kwa muda wa miezi miwili wewe unachukua unatia mfukoni?

Mna mioyo ya chuma kwani jamani? Waoneeni huruma watoto wa binadamu wenzenu jamani, ibeni ila angalieni na urefu wa kamba.., tuibe kwa hurma, kwani hamna dini nyie.., yaani trillion 2 hata siamini. Yaani moyo unaumaa, hivi nyie Watz trillion 2 mnazichukukije kwani? Nchi zingine hai wahusika wangekuwa wananing’inia kwenye mti, mfano China huu ujinga huwezi kufanya.

Sasa nasemaje, hizo trillion2 zirudi, otherwise 2025 tutaondoka na kichwa cha mtu, sisi sio nguruwe, ni binadamu!
Mimi hua najiuliza hivi hii mijizi haina dini basi tuseme dini tumeletewa na wazungu na waarabu basi haina hata ubinadamu wa kuona kuna umuhimu wa kusimamia rasilimali za watu
 
Na kamwe hayawezi kupitisha sheria za kunyonga wezi kwa sababu yatanyongana yenyewe..

Kama wangekua na nia ya dhati kukomesha wizi, ufisadi, rushwa n.k kwa maslahi ya hili taifa kwa nini wanapata kigugumizi kuandaa miswada yenye sheria kali na kuipitisha? CCM koo la wezi
Au tuanzishe Taliban ya bongo. Ukikutana na waziri mzigo na mwizi unampa za kichwa tu. Haleti maendeo jimboni,za kichwa. Anakesha Dar es salaam na Dodoma Miaka mitano harudi jimboni,za kichwa.

Jana nimemwona waziri wa Twitter amepost picha yake na jezi ya Yanga ametanua mikono Kama ana majipu kwapani anasema "wananchi tunashangilia kibingwa Kama hivi" nikasema Yani wafanya biashara k'koo wanalalamika yeye anajitanya mikono huyu alipaswa achezee za kichwa tu.

Maana mama hawatumbui mawaziri mizigo na wezi.
 
Wakati mama anaapishwa wengine machozi yalitoka,si kwamba tunadharau wanawake ama tunadharau wazenj NO,ni sababu tunawajua wanawake vizuri.
Hii nchi ilimshinda JK mwanamume mpaka akazira ikapigwa vizuri mno,ijekuwa huyu mama???

Nchi imejaa wahuni,watu wa fulsa,matapeli,watu wenye uchu na na ashki ya pesa,wasiolitakia mema taifa na wananchi hata chembe,ukiwapa kisogo tu unakuta damage isiyotizamika.

Mama hataki lawama wala ugomvi na mtu,E2 naskia ni kama yuko frustrated hata akikasirishwa na walinzi tu wa getini anatishia kujiudhuru,kwanini??haoni hata maana ya cheo chake,wa kutubeba alikuwa E 4 lakini nayeye sijui kafungwa nini miguuni wadau.

Mgomo Kkoo unawezafungua njia ya migomo mingine,migomo sio uzalendo,migomo sio uungwana,ila watu wanafanyaje sasa
 
Ila huyo Singida United lazima aachie kamba, maana ameshindwa kula kwa urefu wa kamba.., kidogo imani inaweza kurudi
 
Hii nchi ni ngumu sana kwa watu wa kipato cha kati, na cha chini.

Only Mafisadi, wapiga dili, wala rushwa, wafanyabiashara wakubwa wenye connection na wanasiasa; ndiyo wanaofaidi. Mimi kwa kweli nikipata upenyo wa kukwepa kodi, siwezi kujiuliza mara mbili.
 
Majuzi nilikuwa maeneo ya ukonga nikawa nimesimama karibu na kijiwe cha bodaboda ikapita Range rover, bodaboda mmoja akaonyesha kukasirishwa akawa anaongea maneno kwamba huyo aliyepita na range anawadhihaki kwa gari ya gharama iliyonunuliwa kwa pesa zetu wanazofisadi na kuapa kwamba ipo siku.

Nilivyojaribu kumdadisi kuhusu hoja yake alionyesha kabisa kuchukizwa na kujiapiza kwamba ipo siku tu.

Sasa hao wahusika ni vizuri wakatafakari haya mambo, chuki kwenye jamii kwa watu wa daraja la chini ni kubwa sana wanaona wanaonewa na mfumo uliopo.

Labda huenda wao na familia zao wameshajiwekeza kwamba kikinuka watakimbilia ughaibuni ndo maana wake zao wanaenda kujifungulia huko marekani.​
 
Nimetoa bank jana na leo hayo makato Mungu ndo anajuaa
Nikifikiri huyu mama yuko mpk 2030 basi namstakia Mungu tuu

Basi heri tulatwe pesa zisimamiwe kazi zifanyike matokeo yake zinaliwaa ht njia za kurudia majumban mbovu mbovuu

Maji mtaan kwangu ni week sasa hakuna matank binafsi yameishaaa,,,ni vingi jmn

Eeh Mungu ww
 
Na kamwe hayawezi kupitisha sheria za kunyonga wezi kwa sababu yatanyongana yenyewe..

Kama wangekua na nia ya dhati kukomesha wizi, ufisadi, rushwa n.k kwa maslahi ya hili taifa kwa nini wanapata kigugumizi kuandaa miswada yenye sheria kali na kuipitisha? CCM koo la wezi
Huo ndio uzuli wa Magufuli,wabunge wote waliomo bungeni walipata ubunge kwa mguvu za magufuli hawakuchaguliwa ulitegemea nn?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom