TRA ya Kitilya imeoza kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA ya Kitilya imeoza kwa rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by the circus, Dec 30, 2011.

 1. t

  the circus Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana Jf nimeikuta hii michuzi lakini mwenyewe kaweka mambo huwezi kucopy text toka kwenye blog yake
  [​IMG]


  By US Blogger

  Ankal Michuzi, naomba unipe nafasi kuandika kidogo juu ya mambo niliyokumbana nayo ili wa-Tanzania hasa waishio nje ya nchi waelewe hali halisi jinsi inavyosikitisha na kukatisha tama.


  Viongozi wamekuwa na safari za kila siku na wamekuwa wakihalalisha gharama za safari zao ya kwamba wanahimiza uwekezaji na sisi wana diaspora tumekuwa tukiambiwa tujenge nchi kwani hakuna tuliyemuwachia nchi atujengee.


  Kwa heshima na taadhima baadhi yetu tukaitikia wito. Mimi nikajikusanya na wenzangu ili tuanzishe mradi ambao ulikwa na malengo ya sisi wanasiriamali tupate faida kwa ajili ya juhudi zatu na pia wenzetu wa nyumbani wapate ajira. Tulifanya utafiti wa kisayansi na mtu yoyote amabaye angeona business plan yetu na ni mtalamu wa biashara angeamini kabisa tumejitahidi. Biashara yetu ilikuwa ijishughulishe na ununuzi wa bidhaa kutoka mbalimbali na kupeleka nyumbani.


  Wakati tunasafarisha mzigo tulishafanya utafiti wa viwango vya kodi, TRA wenyewe walishatupa makadirio ya kodi kutikana na invoices zetu. Baada ya mzigo kufika Dar es Salaam biashara yote iligeuka na kuwa janga, kwanza TRA walitupatia viwango vya kodi kama jinsi tulivyotarajia, baada ya siku 2-3 clearing agent wetu anatuambia ya kwamba wame ‘uplift’ thamani na hivyo kodi inaongezeka kwa asilimia 100, tukahoji kwa nini iwe hivyo tukaambiwa ya kwamba tathmini ya kwanza hailingani na ‘minimum values’ za TRA wakati ni haohao TRA ndio waliotoa makadirio ya kodi ya awali (preliminary).

  Agent wetu anasema hakuna namna kwani hata mtu uki appeal inachukua muda mrefu, nilivyojaribu kuangalia online namna yak u appeal harakaharaka hakuna maelezo yoyote, nikajaribu kuwasiliana na watumishi wa TRA ninaowafahamu nao pia wakasema kama kuna mtu ame uplift hakuna namna. Sasa kama bidhaa inatarajiwa kupatya faida ya kama 20% utawezaje kupata faida endapo kodi inapandishwa kimchezomchezo.


  Tukasema haya maji tumeyavulia nguo sasa tunaoge, tukakubali kulipa hiyo kodi. Kam hiyo haitoshi wakati wa kukagua hakuna lolote jipya lakini mkaguzi naye akasema anaongeza kodi. Pia tulikuwa na bidhaa chache amabazo thamani yake haizidi hata $150, bidhaa hizo zilikuwa kama sample kwa wateja wetu kwa hiyo hatukuziweka kwenye invoice, jamaa wa TRA wakadai hilo ni kosa na adhabu yake ni dola $10,000. Hawa jamaa hawana hata ubinaadamu, wao lengo lao ni kukomoa tu na kujifanya Miungu watu. Wana ubinafsi wa hali ya juu na wala hawajali ya kwamba wakimfilishi mjasiriamali atawacha kufanya biashara na wao mapato yatapungua, wanaangalia wakomoe leo bila ya kujali mapato ya kesho.


  Yote haya wanayafanya kwa lengo la kushawishi rushwa na online hakuna namna ya kuwasiliana harakaharaka na wakubwa ili waingilie kati. Matokeo yake ni kwamba tumejikuta tumelipa asilimia 500 ya makodi kulinganisha na mahesabu yetu wakati timu yetu ya biashara ina mpaka wahasibu wanaofanya kazi marekani katika taasisi muhimu. Yaani elimu ya mtu haina thamani yoyote katika kufanya biashara Tanzania, ili ufanikiwe inabidi uwe mtoa rushwa vinginevyo ni kupoteza muda.


  Nimewasiliana na baadhi wa wafanyabiashara waliofanikiwa na kuwasimulia na wanasema hayo ndio mambo ya kawaida na kwamba ‘huku hakuna formula’. Sasa nchi ambayo mambo yanakwenda kijanjajanja sisi diaspora tutawezaje kuchangia maendeleo kama TRA kazi yao ni kukomoa tu watu. Nimejikuta nalipa kodi zaidi ya hata gharama za kununulia bidhaa.

  Mimi nashauri viongozi waache mara moja kushawishi wajasiriamali kuwekeza nchini na kupoteza hela za safari za nchi mpaka hapo vyombo husika vitakapokuwa tayari kufanya kazi na diaspora.

  Katika nchi za ulaya na marekani ukinunua chochote hata kama ni gari ama nyumba unapata makadirio ya kodi na wakati wa kulipa unalipa mpaka cents kama jinsi ilivyo makadirio, kufanya hivyo hakuhitaji fedha kwa hiyo umasikini sio sababu, tatizo letu ni kwamba hakuna utamaduni wa uadilifu na watumishi wa Serikali wameweka ubinafsi mbele na uwajibikaji pia hakuna.

  Leo tumesoma ya kwamba Serikali inataka kukopa fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, kama TRA kazi yao ni kuuwa biashara kwa nini Serikali isifilisike?

  Ujanja unaofanywa na TRA sio kubadilisha rate ya kodi kwani rate inapangwa na sheria, wanapowakaba watu ni kwenye thamani ya mali, nunua mali ya $1 lakini ikifika kwenye kupiga hesabu za kodi wao wanakwambia tunaanzia na $5 na unajikuta unalipa mara tano ya ulichotegemea ama unalazimika kuacha mzigo wago uwe mali ya TRA ili wapige mnada na hapo wanashirikiana na marafiki zao kupata makontena ya watu kwa bei ya kuokota wakati mwenye mali ameshakula hasara

  Ushauri wangu wa bure kwa wajasiriamali wanaoishi nje ya nchi hasa wale ambao wana matatizo ya moyo ama blood pressure ni kwamba kama kama rushwa kwako ni mwiko na ni dhambi usipoteze muda wako na biashara za Tanzania zinazohusu kuingiza bidhaa, TRA watakuliza na wanaweza kukuua kwa heart attack.

  Usblogger11@gmail.com


  Kuna Maoni 26 mpaka sasa.

  MICHUZI: yale yaleeeee.....TRA Inanuka Rushwa!
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  CCM oyeeee!
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  wenzenu TRA wanawatangazia kuwa wamevuka malengo ya kukusanya kodi........unafikiri viongozi wetu vilaza watawapigia kelele tena hao TRA?
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  alafu tunaambiwa ndani ya TRA kuna askari wa usalama wa taifa wa siri! System nzima ni mfu.usalama wa taifa kazi yao nini! Tunajengaje uchumi imara namna hii!
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  Utawala ukiwa lege lege system nzima inaharibika! Na bado a lot to come,kuna mabomu ni muda tu haujatimia! Rushwa inakoelekea inakuwa very complicated,sio ya kuomba tena bali ndani ya system,urasimu!
   
 6. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This is too much....i swear this is too much...we have to do something to stop this...
   
 7. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Moja ya sababu kubwa sana ya umaskini, ukwasi wa pesa na matatizo ya uchumi ni TRA kuwa na mfumo mbovu wa kukusanya mapato nafikiri kuliko nchi sana Africa na pia wafanyakazi wameoza kwa rushwa hapo TRA na sijui PCCB inafanya nini? Vigogo na wafanyabiashara wakubwa hawalipi kodi
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kitilya na genge lake wana loyalty kwa Basil Pesambili Mramba ; mpaka hapo kesi yake ya rushwa itakapotupiliwa mbali wanakinyongo na Mkweree ndio maana wanahujumu mapato kwa kuendekeza mambo ya rushwa!! Mstaafu Luhanjo alikuwa anafaidika na genge hili na ndio maana akamuingiza mkenge mkweree kwa kumshauri amuongezee muda wa miaka miwili ya contract Kitilya!! Pole sana wadanganyika.
   
 9. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Imeandikwa watoza ushuru hawatauona Ufalme wa Mungu...
   
 10. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #10
  Dec 31, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndg pamoja na kwamba mzigo wote tunaitwisha CCM/Serikali kwa uzembe, lakini wanaofanya haya ni mimi na wewe tuliokalia hizi office.
  Manjonjo ya dini zao na vyama vyao wakifika ofisini wanaweka pembeni ni rushwa kwa kwenda mbele.

  Tubadilikeni jamani, tuanze sisi wenyewe kama si hivyo watoto wetu tutawaridhisha nchi hipi? Rushwa, tamaa, ubinafsi, uzembe na matumizi mabaya ya madaraka ni janga tunaitaji kubadilika.
   
 11. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Country of lazy bones will never change.
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Mkuu,
  Kwa level ya uchafu ilipofikia kwa sasa, kurekebisha inahitaji muda mrefu, moyo na akili kama ya mwendawazimu, ingawa inawezekana. Ni suala ambalo inatakiwa lichukue investment ya muda mrefu sana, kwa maana ya kufundisha uzalendo kwa nchi toka ngazi ya shule za awali kabisa. Uzalendo wa nchi hii umekwisha kabisa, na kwa hali ilivyo sasa Tanzania, ukionekana unafanya jambo kinyume na mazoea (vile inavyostahili lifanyike) , kila mtu anakushangaa. Nakuunga mkono, tuanze sasa mabadiliko hayo
   
 13. J

  John W. Mlacha Verified User

  #13
  Apr 4, 2016
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Mambo yote haya yalikuwa yanafanyika geti namba ngapi vile??
   
 14. libeva

  libeva JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2016
  Joined: Mar 25, 2015
  Messages: 2,358
  Likes Received: 791
  Trophy Points: 280
  Dah uzi wa kitambo una madini
   
Loading...