Wanajf habarini za asubuhi.
Leo asubuhi nilipokea sms kutoka kwa mwanaJF mwenzetu Tutor B. katika ujumbe wake aliandika kuwa anaumwa sana.
Baada ya kusoma ujumbe huo nilimpigia akakata simu, akaandika tena sms akisema nisimpigie ila nitume sms kwa kuwa anaumwa sana kichwa na kwamba amezuiliwa kuongea na simu kwa muda wa siku 90.
Lakini sasa kitu ambacho sijamuelewa ni hizi sms zake ambazo ambazo alinitumia kwa mfululizo, Hapa nitazinukuu.
1.Wajulishe wanaJF, unisaidie kuwaaga
2.Waage kabisa, taarifa zingine mtapata kwa redio na TV
3. Waambie tuonane ulimwengu wa roho
Nikamuuliza swali, ina maana hutaingia tena JF? akanijibu:
4. Nitaingiaje wakati naenda kwa baba? Nasikitika kuondoka...
5. Najisikia kuhama ulimwenguni kuna sehemu nyingine nzuri zaidi
6. Vipi mbona unaguna? Pole kwa kunipoteza.
Na bado hadi muda huu anaendelea kunitumia sms za kuwaaga wana JF
Nimeona tu niweke huu uzi hapa maana, simuelewi huyu member kwa haya anayonitumia kwenye sms.
UPDATES

NAHUJA .... ahsante sana kwa kuwajuza ndugu wa JF kuhusu kuhumwa ...
Mlionitakia pole, nawashukuru sana mlikuwa sawa!
Mliopost kwa namna mlivyoona - ni vyema na haki!
Mlionijulia hali hata kwa simu - ahsante sana!
Naendelea vyema japo maumivu bado yanasumbua.
Wanaoogopa kufahamiana JF wachunguze mienendo yao; kwangu mimi nafurahi kuongeza marafiki kila iitwayo leo kuliko kuongeza maadui.
Kuishi ndani ya mioyo ya watu ni pamoja na kuwasiliana nao hata kama wakiwa mbali na upeo wa macho yako.