Maziko ya babu yake mwanajf sipo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maziko ya babu yake mwanajf sipo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PakaJimmy, Nov 23, 2009.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ndugu WanaJF,kama mlivyoona hiyo introduction hapo juu, ni kwamba muda huu ndo nawasili mjini Arusha tokea eneo yalikofanyika mazishi ya Babu Mpendwa wa mwanaJF wetu mahiri, SIPO.

  Mimi kama mjuavyo niko huku Arusha, na baada ya kukutana na thread hiyo hapo juu, nilim`PM huyu bwana SIPO nikimsihi anijulishe kuhusu tarehe na Eneola mazishi mara atakapowasili Arusha, ambapo kweli alinifahamisha kwamba wangemzika leo [j3,23/11/2009], katika eneo liitwalo Bangata, umbali wa KM10 toka Arusha mjini, miguuni mwa Mlima Meru.

  Nami bila ajizi nimeaga kazini kwangu mapema, na kuelekea pande za eneo hilo geni kwangu, huku nikijiamini kuwa naenda kuiwakilisha JAMII-FORUMS katika mazishi hayo, japo kwa uhakika simjui kabisa kwa sura mwenyeji wangu SIPO!

  Kikwetu wanasema "Nyumba yenye matanga haijifichi"! Kwa Neema za Mungu niliwasili mahala huko baada ya kuulizia njia kwa kila niliyemwona usoni akikatiza!

  Misa rasmi ya kumwombea Marehemu huyo, Mzee Michael Tomito(81), ambaye alikuwa pia Mchungaji wa KKKT, ilianza mida ya saa 7mchana katika kanisa dogo la kijijini hapo, ambapo ilihudhuriwa na Maaskofu wa2, Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Arusha na Askofu Akyoo wa Meru. Pamoja na wakuu hao, alikuwepo pia EL, Wachungaji tele toka mji mzima wa Arusha, na ujumbe wa vyama vya siasa na wa kiserikali.

  Lakini kikubwa zaidi nilichoshuhudia na kupigwa nacho butwaa ni umati wa watu, ambapo kwa hesabu za haraka walizidi 2000.

  Baada ya Misa hiyo, Msafara wa kuelekea Kaburini umeanza, ambapo ni shambani kwake Marehemu, na muda wa saa 9.00mchana Mzee huyo amepumzishwa mahala pake pa kudumu, na kuachana moja kwa moja na dhiki za dunia hii!

  Aidha, Mzee huyo Mchungaji Veterani hapa Arusha ameacha watoto 7, wajukuu 16(INCLUDING SIPO), na vilembwe 2, ambapo mkewe alishatangulia kunako haki mwaka2007.

  Katika salamu za rambirambi zilizotolewa na vikundi, mbalimbali vya kijamii, vimeeleza kuwa Mzee huyu aliyezaliwa mwaka 1928 alikuwa msomi wa wakati wake, na kabla ya kuanza kusomea Uchungaji katika chuo cha Makumira, alisomea na kufanya kazi katika fani za Kilimo, Afya Chama tawala na sekta nyingine lukuki.

  Aidha ameelezewa kuwa alikuwa Mfano wa kuigwa katika jamii na Taifa kwa ujumla.MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU MZEE HUYU!

  Hadi najipanga kuondoka eneo hilo, kwa hakika sijafanikiwa kumfahamu Mwanaharakati SIPO, japo nimesalimiana na watu kadha MBAPO HUENDA MMOJAWAPO NDIYE. Anyway, labda ndiyo raha/Karaha ya JF!

  Lakini naamini nimetimiza wajibu wangu kama MwanaJF, wa KUWAWAKILISHA, ipasavyo, na nadhani wanaJF mtanisupport na kunipa BIG-UP kwa kazi hiyo!.

  NAWASASILISHA .
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kweli JF nimeikubali... asante PJ kuhudhuria mazishi haya laiti kama ningekufahamu ningekuona...sikujua kama msiba huu ndio wa SIPO maana unanihusu hata mimi!!
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Nov 23, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  asante kwa moyo wake, hii ndio maana ya jamiiforums.
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  PJ hongera sana umemtendea haki SIPO. Kweli inatia moyo nakuona tunaishi kama familia.
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asante Mkuu, hopefully Sipo atajisikia faraja baada ya kuja kuisoma hii kwamba miongoni mwa waombolezaji alikuwepo at least (kwa maana huenda mlikuwa wengi) mwana JF mmoja.
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  That is the Spirit PJ!!! Be blessed always
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Good move ndugu...your courage is the lesson to many
   
 8. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu nimekukubali na ndo maana JF siku zote ni wanafamilia moja japo tunapishana kwa maoni na mawazo humu ndani. Shukurani PJ kwa kutuwakilisha.
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  PJ asante kwa kujitoa kwako kutuwakilisha. Mungu akubariki sana sana.
  JF inatia moyo sana hata kwa mambo kama haya msiba tunatiana faraja sana. Ni familia isiyo ya mtandaoni tu.
  Mwaka jana mwezi wa kumi na mbili nilifiwa na baba yangu mzazi na yupo mwana jf alikuja msibani kuniona na kunifariji. Anaitwa Omulangi.
  Mungu ibariki jf.
   
 10. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkurugenzi,I salute you.Asante kwa kutuwakilisha.To be honest umefanya jambo kubwa sana.Muumba akuzidishie na uendelee kuwa na moyo huo huo.
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nawashukuruni saana nyote kwa Thanks zenu, maana nyie ndo mnaounda kundi hili kubwa, na ndio mlionitia hamasa ya kuwawakilisha.

  Tuzidi kuwa wamoja katika mambo ya kijamii.
  Thanx again.
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  Ahsante sana dada VC.

  Kwa hakika miminiko reachable kabisa, na ni rahisi kunifahamu, ni suala la kutafutana kwa udi na uvumba tu.

  Sikujua kama SIPO anakuhusu kwa ukaribu kiasi hicho!

  Ni nani kwako?
   
 13. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  PJ kazi nzuri umeonesha mfano wa kuigwa na wana jamii.
   
 14. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Poleni sana , Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
  Pj for every good deed you will be blessed.
   
 15. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  "Heri kuiendea nyumba yenye matanga,kuliko kuiendea nyumba yenye harusi"
  Ubarikiwe na Bwana.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  PJ MWENYEZI MUNGU AKUJAALIE KWA MOYO NA UPENDO ULIOUONYESHA
  HII INAONYESHA NI KIASI GANI jf INAVYOWEZA KUWAFANYA WATU MKAFAAMINA ,NA MKAPENDANA KAMA NDUGU
  MIMI BINAFSI NIMEFARIJIKA NA HILI NA KUONA KAMA TUKO PAMOJA
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kwanza hongera sana PJ kwa kuonyesha upendo na charity ya kuiwakilisha JF

  Pili,VC is more than a forum, iko sehemu zote!!!! Naiheshimu sana aisee!!

  Tatu, Ushirikiano kama huu ndio unaotakiwa na wanaJF

  Pole Sipo, lakini natumaini kuwa utafarijika sana na umoja na upendo ulioonyeshwa na wanajamii
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndio hata mimi najaribu kupata picha katika wajukuu za marehemu SIPO ndio yupi.
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Laa... ni ajabu na kweli.

  Mtu unajibishana nae kila siku katika hii forum, na una dalili ya mahusiano ya kinasaba huko nje ya forum, lakini bado hujui kuwa ndiye yupi exactly?

  Sa si umtumia PM ili mjuane kikweli?...Kwa wale vijana niliowaona pale jana ambao ndo wajukuu wanaonekana ni wapole sana, na walikuwa wameguswa kwa njia ya pekee na msiba ule! Nilijaribu kutumia elimu yangu ya Saikolojia hata kumhisi tu SIPO, maana niliamini kuwa hata sura yake ingeonyesha uanaharakati ambao anauhubiri hapa jukwaani, lakini niligonga mwamba(miserably)!

  Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza!
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hatuhitaji kujua nani ni nani JF... im sure huko uraiani tunakutana na tunajuana vizuri tu lol.
  Kweli..umdhaniae ndiye siye... sura ya uanaharakati JF siyo sura halisi kwenye maisha...
   
Loading...