Kuhusu MwanaJF mwenzetu Tutor B

Kuhusu MwanaJF mwenzetu Tutor B

Status
Not open for further replies.
Wanajf habarini za asubuhi.

Leo asubuhi nilipokea sms kutoka kwa mwanaJF mwenzetu Tutor B. katika ujumbe wake aliandika kuwa anaumwa sana.

Baada ya kusoma ujumbe huo nilimpigia akakata simu, akaandika tena sms akisema nisimpigie ila nitume sms kwa kuwa anaumwa sana kichwa na kwamba amezuiliwa kuongea na simu kwa muda wa siku 90.

Lakini sasa kitu ambacho sijamuelewa ni hizi sms zake ambazo ambazo alinitumia kwa mfululizo, Hapa nitazinukuu.

1.Wajulishe wanaJF, unisaidie kuwaaga
2.Waage kabisa, taarifa zingine mtapata kwa redio na TV
3. Waambie tuonane ulimwengu wa roho
Nikamuuliza swali, ina maana hutaingia tena JF? akanijibu:
4. Nitaingiaje wakati naenda kwa baba? Nasikitika kuondoka...
5. Najisikia kuhama ulimwenguni kuna sehemu nyingine nzuri zaidi
6. Vipi mbona unaguna? Pole kwa kunipoteza.

Na bado hadi muda huu anaendelea kunitumia sms za kuwaaga wana JF


Nimeona tu niweke huu uzi hapa maana, simuelewi huyu member kwa haya anayonitumia kwenye sms.
Kwenye redio na tv tutajuaje kama ni yeye? Labda aanze kutupatia jina lake halisi, pia hiyo isijekua kuna mhuni mmoja anakuchezesha akili ili baadae aombe msaada wa matibabu,
USHAURI:Nenda kamuone anakoishi ili ujue anaetuma sms ni yeye au laah!
 
H
Kwenye redio na tv tutajuaje kama ni yeye? Labda aanze kutupatia jina lake halisi, pia hiyo isijekua kuna mhuni mmoja anakuchezesha akili ili baadae aombe msaada wa matibabu,
USHAURI:Nenda kamuone anakoishi ili ujue anaetuma sms ni yeye au laah!

Hapana mkuu ni yeye
 
Kwanini usifanye utaratibu wa kupata Namba hata ya MTU alienae karibu? Unaweza kuta kaibiwa simu watu wanachezea tu contacts zake.
Ni yeye maana nimepiga namba zake zote ujumbe wake ni huo huo kuwa nimuagie wanaJF. hajaomba hela zaidi ku insisit kuwaaga wanaJF kuwa anakufa. halafu anatuma mameseji mengine hata hayasomeki
 
Bado hajafika mbinguni? anatumia usafiri gani mbov namna hiyo? au kuna Jam? Inawezekana kaibiwa simu...kwa sababu maelezo yana utoto mwingi, kwanza ukiumwa kichwa ki ukweli hata hiyo device huwezi kuangalia..we mwambie tu hakuna haja ya kuaga mara 10000 Huko aendako JF ipo...akifika atutaarifu kama alivyotutaarifu wakati anaenda...REST IN PEACE
 
Swali langu limelenga kwenye dondoo namba 2; bado hujanijibu. Ila nakushauri ukienda kumwona usiende peke yako, huyo mtu ana stress asijetumia huruma yako kukutafuna kirahisi.
Jioni nikitoka hapa kwenye shughuli zangu, nitapita kwake. Ahsante kwa ushauri wako mkuu
 
Mkuu yani unajua hadi ananitisha. Nimemuuliza swali, kuwa anavuta bangi? akanijibu kwa kifupi kuwa hata South Africa inaruhusiwa. yaani hadi muda ninavyotaipu hii comment bado sms zinaendelea kuingia za kuwaaga wanaJF!!
Una uhakika ni yeye? Siku hizi kuna wakora wengi. Subiri atakapokubomu hela ya kulipia bill hospitali
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom