Ngambili Ngenja
Member
- Mar 1, 2008
- 44
- 21
Nyie wakirsto, mbona sisi hatuwaingillii katika mambo yenu. Kuna kipindi hapa mawakala wa kanisa katika vyombo vya habari na viongozi wengi hasa wakirsto, mlilivalia njuga na kulipigia debe sana saula la Mchungaji wa Kanisa la Kiinjiili la Kilutheli nchini(KKKT), Ambilikile Mwasapile juu Dawa yake aliodai ameoteshwa na Mungu maarufu kama kikombe cha Babu. Mlidhani kua ndio mnainua Ukristo. Matokeo yake mkasababisha watu wengi kufa.
Niliwahi kuulizwa na Kinyozi Mmoja nilipokua Salon, Nini maoni yangu juu ya Kikombe cha Babu, Nilimjibu yule Kijana, Time will tell.
Nadhani matokeo yake mliyaona. Lakini sisi Waislamu hatukuwagusa. Iweje leo Muingilie Mambo yasio wahusu?.
Ulianza kuchangia vyema mpaka nikahisi una kaupeo lakini hapo juu umenifanya niyaone dhahiri matokeo na madhara ya kukaririshwa, pole sana. Kwa taarifa, waislam wengi ndo walikuwa wateja wa Babu na wengi wao wakitokea hapa nyumbani, Kenya na Uganda.