Nawaza Nje ya Box.... CCM ni ileile.

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,984
2,587
Nawaza nje ya box...CCM ni ileile.

CCM ni waoga sana kutoka madarakani, inapokuja hoja inayotishia uwepo wao madarakani watafanya lolote hata ikibidi kudhulumu ili wabakie.

Wakati CUF inajipantia nguvu Zanzibar miaka ya 92 kwenda 95 walieneza habari nchi nzima kuwa CUF ni chama cha dini flani. Sisi wa bara enzi hizo mfumo wa vyama vingi ndio umeingia tulibebwa na ujinga huo. CCM walitumia propaganda hizo ili kuwagawa wazanzibari kwa misingi ya dini wapate kura japo hawakushinda wakaiba kura.

Mwaka 2001 kulitokea fujo Zanzibar baada ya uchaguzi kwa CCM kuiba ushindi wa CUF na waliopinga Mkapa akawanyoosha hadi wakakimbia. Yote ilikua kulinda CCM isitoke madarakani.

2010 CCM wakaona ngoma imekua ngumu. Wakaona katiba ya zanzibar ibadilishwe kuwe na serikali ya umoja wa kitaifa. Hili lililenga kupoza joto la upinzani na CCM waendelee kupora madaraka. Hii yote kuibakiza CCM madarakani.

2010 hiyo hiyo CCM wakawaahidi wanzanzibari kuwapa mahakama ya kadhi. Bila kujali lile jambo la kidini lilikua na impact gani kwa umoja wa taifa. Walipopata madaraka wakaitupilia mbali hoja hiyo maana walishapata walichokitaka. Hii yote ni kuhakikisha CCM inabakia madarakani.

2015 uchaguzi wa Zanzibar ukafutwa baada ya CCM kuona imeshindwa waziwazi....Yote kulinda CCM isitoke madarakani.

Nawaza nje ya box. Mjadala wa bandari Ccm wameshindwa kuuzima. Wapinzani wameibeba hoja na inaonekana wanakubaliwa zaidi kwa hoja zao. CCM waoga wa hoja wataendelea kukaa kimya? Wamezunguka nchi nzima haijasaidia. Samia anasema ameamua kunyamaza, si kwa hiari yake, hana hoja ya kuwaprove wrong wanaopinga mkataba. Atasema nini ambacho Kinana na CCM nzima hawajasema?

Hii hoja inatishia usalama wa madaraka ya CCM huko mbele. Wanavyopenda madaraka hawatakubali. Watafanya lolote hata kudhulumu, kuleta mgawanyiko na kadhalika ili mjadala ufe.

Kanisa katoliki huwezi kulitenga na siasa za dunia tangu kuanzishwa kwake. Ndio maana wana muwakilishi hadi UN. Je CCM watashindwa kuwatumia katoliki? Iwapo katoliki wananifaika na uwepo wa CCM hawawezi kutumiwa kutuvuruga? Nawaza nje ya box.

Huu waraka wa TEC ni kazi ya CCM wenyewe. Wameuleta mahsusi ili ionekane mjadala wa DPW unatishia amani ya nchi kwa kuanza kuwa na mlengo wa kidini. Wanatafuta sababu ya kuuzima maana njia za majukwaani zimefeli. Nawaza nje ya box.

Nawaza nje ya box. CCM hii ambayo 2015 walisema hata kwa goli la mkono watafanya ili waingie madarakani. Ni samia huyu huyu akiwa mbeya kwenye kwenye kampeni za uchaguzi 2020, baada ya kuona maji yanazidi unga akautangazia umma kwamba hata wakipigia upande mwingine wao (CCM) ndio wataunda serikali.

CCM ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia ni ileile. Wako tayari kufanya uharamu wowote ili walinde madaraka yao. Hawa wanatofautiana majina tu. Linapokuja suala la madaraka CCM ni moja. Ndio maana CCM hawakumkemea mkapa alipopiga watu kule Zanzibar 2001.

Ni CCM hiyo hiyo ilibariki uchaguzi halali kufutwa. Ni CCM hiyo hiyo ilipiga makofi Magufuli alipovuruga uchaguzi 2020.

TEC wametumiwa na CCM. Nawaza nje ya box.
 
Ok, Rudi ndani ya box haraka.

Uhai wa kinyonga wa KIJANI na manjano hautozidi 2026.
 
Ccm ni ile ile.
Wanasema Vatican ndo majasusi wa kidunia.
Rais alienda kutana na viongozi wote wa dini.
Ghafla Dr.Slaa akasema kupindua nchi.
Akakamatwa.
Waraka wa wale waliokaa na Rais ukatolewa hasa na TEC .
Ghafla ishu ya Bandari inakaa kidini na sio kiupinzani Tena.
Ghafla Rais anasema hakuna mwenye ubavu.
Inawezekana CCM wanatuchezea eti!
Hii ajenda ya Bandari huenda imepitishwa hapa tunachezewa..
Kauli ya TEC ndo itakuwa inajadiliwa mitandaoni na sio CHADEMA Tena.
Hapa Kuna Game sio bure.
 
Back
Top Bottom