Mahakama ya kadhi iko chini ya usimamizi wa waislamu wenyewe.
Ili kutenda haki bila kuathiri haki nyingine na misingi ya utu wa mtanzania na Haki za Binadamu, Serikali yetu haiamini katika dini.
Serikali yetu Imeshajitosheleza na mahakama zake. Zisizoegemea upande wowote wa dini. Na zinafanya kazi kama kawaida.
Sasa kama mahakama ya ya kadhi (uislamu) haiwezi kumshurutisha kijana wa kiislamu aliyekataa kutii mahakama ya kidini, ni wazi basi huyo kijana sio muislamu halisi. Hampendi Allah wala Mtume wake mohammad SAW. Muislamu wa kweli ni mujibu atii viongozi wake na dini yake na koran na hadithi zote za mtume. Hata hivyo Swala la imani ni la MTU binafsi.
Inashangaza kuona mnahofia waislamu kukataa kutii dini yake, mpaka serikali iingilie kati kumshurutisha nwislamu!. Kwani maagizo ya mtume hayako wazi?
Hii ndio itapelekea machafuko na fujo zaidi has a kati ya jamii na serikali..
Serikali haina haki ya kumlazimisha MTU kuamini ama kufuata asichoamini. Serikali inabakia kuwa neutral.
Wanandoa wana haki ya kuamua kuchagua njia waitakayo ili kupata haki zao za msingi.
Isitoshe kama Shida ya Dada yangu ni kupata haki, na kama anaweza kuipata HAKI katika mahakama za kiserikali zenye uwezo wa kushurutisha What the fuzz is all about?
Mahakama ya kadhi ni kwa waislamu wanaoufuata uislamu. Na sio kwakila MTU kwakuwa tu anajina la kiislamu.
Wewe
crabat Ikatokea Dada yako amebakwa na uislamu unataka ushahidi wa watu wanne wakiwemo viongozi wa dini.
Kama Dada yako atashindwa kuleta shahidi ambaye ni kiongozi wa kidini katika mahakama ya kadhi atakosa haki zake.
Na hapa haja ya yeye kwenda mahakama za serikali ambapo angepata haki yake Kirahisi inazidi kuwa na mashiko Manake kule hata mashahidi wa 3 wanatosha, pia sio lazima shahidi awe kiongozi wa dini na vipimo vya hospital vinatumika pia Ili Kumbaini mtuhumiwa wa unabakaji.
Tena mahakama za serikali ziko very effective . kwakuwa wanaoperate kwa motto usemao ignorance of the law is not an excuses....
Pia mahakama za serikali zinamlinda mwanamke na kumpa heshima yake hapa duniani bila Dr itikadi yake.
Mfano;
kuna sheria ya kupinga Ulawiti(usodoma/kumwingilia mwanamke kinyume na maumbile) kwa mwanamke hata kama ni mkeo. Hii sheria inaweza kumlinda Dada yako aliyeolewa.
Mahakama za serikali zinaweza kumsaidia mdogo wako wa Kike ama mtoto wako wa kike kujihakikishia kupata Elimu badala ya kuolewa akiwa mtoto.
Mahakama za serikali zinaweza kumlinda mdogo wako wa kike na ubakaji, kwa visingizio vya kuolewa katika utoto wake.
Mahakama za serikali zinamlinda mtoto wako wa kike/ dada yako ama mama yako mzazi dhidi ya unyanyasaji wa kupigwa na mumewe ama baba yako.kwahiyo utaona mahakama za serikali
Bado ni effective kulinda haki, utu wa jamii.
Vilevile si vyema kumsema MTU unayetofautiana naye mawazo kuwa ana chuki na wewe. Nakushauri attack concept na sio personality ya MTU. Wanaokataa Kadhi; miongoni mwao wako wakristo, wenye imani zao za jadi, wahindu, Atheists, Rastafari, na kundi kubwa la waislamu. Sasa haiwezekani makundi yote haya yakawa na sababu za chuki na kikundi cha waislamu wachache wenye kuitaka mahakama ya kadhi.
Serikali hii sio Mali ya kikundi cha waislamu peke yao. Ni makosa makubwa sana, kwamtu Kutaka waislamu na wasio wasilamu wachanganyike kwenye mahakama kusimamia uislamu na mirathi. Ni sawa na kuchakachua uislamu.
Isitoshe yapo mambo yanaweza kuonekana ni makosa kwa msingi ya uislamu.lakini lisiwe baya kiserikali ama kwa wasio waislamu.
Mfano mtoto wa kike kukataa kuolewa kwasababu ya umri wake. Na wazazi wamekula mahari.
Ama kupitia kadhi, ugawaji wa mirathi unaweza kumpunja mwanamke mjane wa kiislamu. na akakimbilia serikalini kupata haki zake kwa msingi ya sheria za nchi.
Kadhi inaweza kuleta maçhàfuko katika jamii.
Hasa katika intermarried ya dini tofauti na namna ya kugawana haki kati ya wanandoa.
Inaweza kuzuia Uhuru mtu kuchagua na kuhama imani ya uislamu kwa hiyari yake.
Kwanza sijui kwanini najadili wakati mahakama wenyewe imeshakuka.
ban na serikali?
Huu ulikuwa mtaji wa wanasiasa uchwara wa CCM ili wapate kura za waislamu. Ndio maana wanaipenda sana CCM.