Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 18,875
- 29,421
Tafsiri ya uzalendo ya Awamu ya 5 ni tofauti na ile ya kwenye kamusi ya kiswahili. Sasa hivi Mzalendo ni mtu anayemsifia JPM kwa kila kitu hata pale anapokosea. Mzalendo ni yule ambaye kila sentensi akitamka lazima ataje majina manne yote ya Magufuli.Nina weza kuwa bora but Sio Mzalendo. Angalia aliyofanya JPM na pima kulinganisha na his predecessors
Hivi kweli kwa akili yako unataka kuniambia JPM kuweka taasisi za kitaifa Kijijini kwake Chato ndiyo uzalendo? We have to reddifine this word uzalendo.
Hivi kumfuta mkataba wa kazi CAG anayehoji matumizi mabaya ya Tsh 2.4 Trillion ndiyo uzalendo?
Kuwafuta kazi wenye vyeti feki na kuwaacha akina Makonda na Mwigulu Nchemba ndiyo uzalendo?
Kumshindilia Lissu risasi 38 kisa ana shauri njia bora ya kumalizana na Barrick ndiyo uzalendo?
Kuficha data za watu wanakufa kwa COVID 19 ndiyo uzalendo?