Baraka Obama is a smart president ametawala 8 years. Msishabikie kitu kama hiki kuongeza ukomo wa Rais nikufukua makaburi tutakayo yakuta tusiseme hatukuambiwa. Yes we need Magufuli but we need to grow new leadership. Nayeye awe mshauri.
Pia, Baraka Hussein alikuwa anaongoza nchi ambayo tayari imeshaendelea.
USA haiitaji Mtu wa kuleta maendeleo kwa maana maendeleo tayari wanayo.
USA inahitaji mtu wa kusimamia Sera, Katiba na Mipango ya nchi.
Tanzania tu nahitaji Rais atakaetuletea maendeleo ambae pia awe na uchungu na nchi.
Tumeona Mkwere alivotumia nafasi ya Urais vibaya, aliendelea kuuza nchi pale alipoishia Mkapa. Familia yake isiyokuwa na muunganiko ilituharibia nchi.
Magufuli alipoingia akaanza kufanya Retention ya madini yetu.
Akajenga na ukuta kabisa kuonesha thamani mali zetu.
Mradi wa NSSF chini ya Mkwere na daraja lake la kigamboni, JPM kasimamisha huu mradi sababu uligubikwa na Ufisadi wa Hali ya juu.
Vyeti fake Kwenye taasisi za umma. Zaidi ya Bil 5 zilikuwa zinalipwa kila mwaka kwa watumishi hewa, si kwamba Mkwere alikuwa hajui, ni ukosefu wa uzalendo.
Makusanyo ya kodi yalikuwa yapo chini huku mali za watu zikipotea bila majibu.
Familia ya Mkwere na washikaji zake waliifanya Bandari yetu kuwa ni Mali yao. Simu zilikuwa zikitoka state house, RUHUSU HUO MZIGO HARAKA.
Nchi ilioza ikawa inatoa HARUFU.
Leo hii Bandari imekuwa ni sehemu ya heshima na inaleta pato la nchi.
Zile ;We dogo unachelewesha huo mzigo, unanijua Mimi nani , hazipo tena.
Hata kama utekelezaji wa ndege umesua sua, but the idea was magnificent, ni kufanya maboresho endelevu tu .
Mradi wa Reli za Kisasa ni akili kubwa nyingine ya JPM, ujenzi Daraja la Salenda, Ujenzi wa Daraja Chato Muleba kuokoa wale wananchi, ni akili kubwa nyingine, kuhamisha mji dodoma, ni akili kubwa nyingine.
Wanyama wetu walikuwa wanasafirishwa wazima wazima , huku pembe za tembo zikiwa ni dili. Biashara ambazo zilikuwa zinafanywa na viongozi wakubwa wa nchi.
Yaani ni mengi , hatutomaliza; sasa mtu anawezaje kusema JPM hakuna alichofanya?
Je term extension kwake ni mandatory ili kufanya finalization ?